
Bila shaka umewahi kusikia ama kwa bahati mbaya kushuhudia mtu aliyeamua kujitoa uhai ama kumtoa uhai mpenzi wake kwa sababu ya mapenzi.
Wapo wanaoandika ujumbe wa sababu zilizopelekea yote yatokee baada ya kushindwa kuvumilia mabaya na maumivu ya penzi walilotarajia lingekuwa tulizo la moyo wao.
Sylvester Paul, yeye ni mtaalam wa saikolojia na mahusiano, mtanzania aliyesomea mambo hayo nchini Afrika Kusini na baadae kurejea nchini ambapo ameweza kuandika vitabu kadhaa vinavyohusu mahusiano ya mapenzi, kama vile ‘Moyo Ulioumizwa Kimapenzi’, ‘Mtambue Mwanamke’, na vingine.
Mtaalam huyu ameelezea sababu za kisaikolojia zinazopelekea mtu kuamua kujiua ama kumuua mwenzi wake chanzo kikiwa mapenzi:
“Watu wanakufa kwa sababau Love imekamata uhai wa mtu, ambao unaitwa soul au nafsi. Sasa nafsi imegawanyika katika sehemu tatu, kwenye nafsi kuna mind, kuna emotion na kuna will. Kwa hiyo love ile inaendaga kwenye mind ambayo ni ufahamu, inamvuruga mtu kabisa. Baadae inatoka kwenye ufahamu inaenda kwenye emotion (hisia), mtu anaanza kufanya vitu sasa vitendo. Hapakaliki ofisini, kachanganyikiwa, yaani maisha yote yanakuwa magumu kwake, sometimes anashindwa kulala.
“Ikishatoka kwenye ufahamu, inaenda kwenye ‘will’, yaani nguvu ya maamuzi, unakuta mtu sasa anachukua gari anaanza kusafiri. Mpaka mtu anafikia hapo ujue ameshaumia, love imeshamtesa sana kwenye ufahamu, ikaenda kwenye ufahamu hadi kwenye nguvu ya maamuzi. Kwa hiyo akaamua ku-sacrifice.
“Sasa kinachoweza kumfanya mtu amuue mtu mwingine, ni kwa sababu amekubali kutoa upendo wake na maisha yake na mtu mwingne. Love ni kugawana maisha, wewe hamsini, mimi hamsini. Na ndio maana tunasema Love is a strong feeling of deep affection. Ina maana huyu mtu tayari ameshakuwa affected, ameathirika kisaikolojia, ameathirika katika mambo yote, spiritually na mentally huyu mtu amekufa.
“Vitabu vingine vinasema love is stronger than death, upendo una nguvu kulio mauti. Unaposaini kumpenda mtu umesaini na kifo. Ndio maana tunasema love is stronger than death. Yaani unapompenda mtu umeunganisha na kifo.
“Ukiingia kwenye love umeingia kwenye agano, ndio maana mtu anasema nimekufa kwa ajili yako. Halafu wewe leo unaenda kumbemba mtu ambaye nimekufa kwa ajili yake.
Chanzo: Kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm.