Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Filamu aliyoigiza Ben Pol 'Sunshine', kuzinduliwa February 20, Ben Pol amsifia Bi Kiroboto.

$
0
0

Filamu aliyoigiza mwimbaji wa RnB, Ben Pol na mchekeshaji maarufu, Bi Kiroboto, iliyoandaliwa na kamupni ya Swahilihood itazinduliwa rasmi February 20 mwaka huu.

Mratibu wa Swahilihood, Hassani Mrope ameiambia tovuti ya Times fm kuwa filamu hiyo ya Sunshine itazinduliwa pamoja na filamu nyingine mbili ambazo ni ‘Mdundiko’ na ‘Network’. Filamu hizo zitazinduliwa kuanzia saa kumi na mbili jioni, Century Cinemax, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Nae Ben Pol aliingelea filamu hiyo katika kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm na kumsifia muigizaji huyo wa kike aliyecheza nae kama mama yake, Christina Mbunda aka Bi Kiroboto.
Mwimbaji huyo alieleza kuwa mbali na kuigiza vizuri kama mama mwenye moyo mzuri anayejali familia yake, hata katika uhalisia ni mama bora anayejali.
“Yaani mimi nimeienjoy sana, nilikuwa nafeel kama ni mama yangu mzazi”, alisema Ben Pol.
“unajua bi Kiroboto, ukitoa upande wa kazi wa kuigiza, yaani ni mama mmoja very humble. Yaani ni mama…anaiele feeling ya mama ile…unajua hata kama mko kwenye set kichwa kinauma au nini, yaani ana ile care ya mama. Yaani mpaka nammiss.” Aliongeza Ben Pol.
Kwa mujibu wa Ben Pol, filamu hiyo ilishutiwa kwa muda wa mwezi mmoja.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles