Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Mwanaume aliyempa ujauzito Lil Kim ajitokeza, ni rapper wa New York, ataja jinsia na mwezi watakaopata mtoto.

$
0
0

Wiki iliyopita mashabiki wa rapper wa kike na member wa zamani wa Junior M.A.F.IA, Kimberly Denise Jones aka Lil Kim walikuwa surprised baada ya rapper huyo kuweka wazi kuwa anaujauzito na kuonesha picha, “I can’t wait to be a mom”.

Lakini swali kubwa lililobaki kwenye mabano ni kuhusu jina ama kumfahamu baba mtoto wake ajaye, suala ambalo lilizua tetesi nyingi na majina mengi kutajwa kwa kubahatisha.
Hata hivyo majibu yamepatikana tayari ambapo rapper wa New York anayejulikana kwa jina la Mr. Paper amefunguka kwenye interview aliyofanya kwenye ‘The Rickey Smiley Morning Show’ kuwa yeye ndiye baba mtoto wa Queen Bee.
“Tuko pamoja. Kila kitu kiko poa. Huyo ni mke wangu na huyo ni mtoto wangu.” Alisema Mr. Papers na kuongeza kuwa Lil Kim ana ujauzito wa miezi takribani sita na kwamba wanatarajia kupata mtoto kati ya mwezi May au June.
Rapper huyo aliiweka wazi jinsia ya mtoto huyo kwa kutumia kiwakilishi cha jina kinachomaanisha kuwa ni mtoto wa kiume na kumsifia kuwa atakuwa ‘Gemini’, yaani mtoto aliyezaliwa katikati ya mwezi May na June lakini mbunifu na mwenye akili.
Hata hivyo hakutaka kutaja jina la mtoto walilolichagua, “ila tutawafahamisha wote hivi punde.”
Rapper huyo alikuwa katika mahusiano kwa muda mrefu na Lil Kim japo katika kipindi cha hivi karibuni hawakuwa wazi kuhusu kinachoendelea katikati.
Mwaka 2012, Lil Kim aliwahi kutweet kuwa yeye na rapper huyo wameachana, “As of 2night me & Papers are officially over. No malice or bad blood. I’ll see U guys soon #DaysofXmas.”
Paper naye akajibu akimwambia Lil Kim asishindane na nafsi yake, “@LilKim don’t be so mad you fighting with ya self…Get ya facts str8 lol.” Lakini baadae waliyamaliza na kurudiana, huku wakishirikiana kufanya Remix ya wimbo wa Rihanna ‘Pour It Up’, na kuonekana wote kwenye video ya wimbo huo iliyotoka mwezi March.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles