Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live

MCHUMBA ALIYEUA NA KUJIUA ILALA, CHANZO PICHA ZA UTUPU.

$
0
0
Stori: Waandishi Wetu, Dar es Salaam na Mwanza
MAPENZI ni sanaa tata sana, inawaumiza wengi,

inavunja mioyo ya watu, inakatisha tamaa ya maisha, inaleta umaskini, inasababisha mauaji lakini siyo rahisi kuachana nayo na kwa mantiki hiyo, matukio mengi yataendelea kujiri.

Tukio la Gabriel Munisi kuua watu wawili kisha naye kujiua kwa kisa cha mapenzi, ni mwendelezo wa ‘sinema machafuko’ za mapenzi.
Nyuma ya tukio hilo kuna mengi yanazungumzwa, ila gazeti hili limenasa habari kuwa picha za utupu na SMS za mapenzi ni chanzo cha kila kitu.

NINI HASA CHANZO?
Gazeti hili limebaini kuwa tukio hilo la mauaji, lililochukua nafasi alfajiri ya Jumanne iliyopita, chanzo chake ni Gabriel ‘Gaby’, kunasa picha zinazomuonesha mchumba wake, Christina Newa akiwa na mwanaume mwingine.
Habari zinaeleza kuwa Gaby alichukua kompyuta mpakato (laptop) ya Christina na kuikagua, ndipo akakuta picha ambazo mchumba wake huyo alikuwa katika hali ya kustarehe na mwanaume mwingine.
“Kwanza ile laptop ilikuwa inafunguliwa kwa namba za siri (password), ikabidi Gaby awatafute wataalamu wa kompyuta waweze kumsaidia kuifungua.

“Laptop ilipofunguliwa, Gaby aliikagua na kukuta picha ambazo Christina alikuwa ufukweni na mwanaume mwingine.
“Kuanzia hapo, Gaby akawa analalamika kwamba zile picha ni mbaya sana, ni za utupu na kwamba mchumba wake amemfanyia kitendo kibaya sana,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Kama ndugu au hata jeshi la polisi, wangesoma alama za nyakati, pengine yale mauaji yasingetokea maana dalili zilijionesha waziwazi mapema.”


DALILI ZA MAUAJI
Chanzo chetu kilisema kuwa wakati Gaby anaziona picha hizo, alikuwa nyumbani kwake Mwanza, wakati Christina alikuwa Dar es Salaam.
“Kutokana na hali hiyo, Gaby alimpigia simu Christina aende Mwanza. Bila kujua anaitiwa nini, Christina alifunga safari na kwenda Mwanza.
“Christina alipofika Mwanza Gaby alimnyang’anya simu zote mbili alizokuwa nazo, akapitia SMS zote na kubaini kwamba zipo za mapenzi.

“Gaby akaunga matukio na kudai kwamba mtuma SMS za mapenzi ndiye mwanaume anayeonekana kwenye picha na Christina.
“Christina alisema kuwa hakukuwa na ubaya wowote kwa sababu zile picha siyo mbaya ni za ufukweni tu na wanafunzi wenzake,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Utetezi huo haukumsaidia chochote, maana kuanzia hapo aliendelea kupokea kichapo kila mara, kufungiwa ndani na kupewa kila aina ya mateso.”

KILICHOTIBUA NI MASOMO YA ULAYA
Habari zaidi zinasema kuwa Gaby alikuwa anawaambia marafiki zake kuwa kinachomuuma kuhusu Christina ni kumgharamia masomo kwenye Kisiwa cha Cyprus barani Ulaya.
“Alikuwa akilalamika kuwa kama asingempeleka Cyprus kusoma, yote yasingetokea, maana akiwa huko ndiko alipata mwanya wa kujirusha na mwanaume mwingine na kupiga picha alizozikuta kwenye laptop,” kilisema chanzo chetu.

Habari zinaongeza kuwa sekeseke zima lilitokea wakati Christina akiwa amerejea nchini kwa likizo.
“Aliporudi nchini aliamua kwenda Mwanza kumsalimia mpenzi wake Gaby, baadaye akaelekea Dar lakini kule Mwanza aliacha laptop ambayo iliibua kasheshe nzima,” alisema mtoa habari wetu.

DADA ASIMULIA KISA CHA LAPTOP, PICHA NA SIMU
Caroline ambaye ni dada wa Christina, alipozungumza na waandishi wetu, nyumbani kwao, Ilala, Dar, alifafanua kiundani kisa cha laptop, picha na simu, huku akisema kuwa marehemu shemeji yake (Gaby) ni katili.
Caroline, aliye Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), alisema: “Julai mwaka huu mdogo wangu alikuja likizo akitokea chuoni Cyprus. Gaby ndiye alimpokea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na moja kwa moja walikwenda Mwanza bila kupitia nyumbani.

“Baada ya wiki mbili, Christina alimuomba Gaby ampe ruhusa ya kuja Dar kwa ajili ya kumsalimia mama yetu, alimkubalia lakini akamtaka achukue vitu vichache ili asikawie kurudi Mwanza.

“Christina alikubaliana naye na kuchukua vitu vichache, vingi aliviacha ikiwemo laptop aliyokuwa anatumia chuoni. Alipoondoka Gaby alichukua laptop yake na kuipeleka kwa fundi ili amfungulie kwa sababu ilikuwa na password, alipofanikiwa alikutana na picha zinazomuonesha Christina akiwa amevaa nguo za kuogelea,” alisema Caroline.

Hata hivyo, Caroline alipingana na madai kuwa Christina alipiga picha za utupu na mwanaume mwingine, badala yake alisema:
“Christina alipiga akiwa beach na wasichana wenzake huko Ulaya na hazikuhusiana na suala la kimapenzi.”
Caroline akaendelea: “Gaby hakusema kilichokuwa kinaendelea badala yake alimpigia simu na kumtaka arudi Mwanza kwani amemkumbuka. Alimkatia tiketi ya ndege na kumtumia, kweli Christina akaenda Mwanza.
“Kufika Mwanza ndiyo ugomvi ulianza. Gaby alimnyang’anya Christina simu zake mbili kisha akaanza kumpiga huku akiwa amemshikia bastola.

“Christina alimwambia Gaby kuwa kama kupiga picha na nguo za ufukweni ni tatizo basi wawasiliane na mama yetu mzazi, naye aseme maana ndivyo tulivyolelewa lakini hakuelewa.
“Gaby alimfungia ndani Christina na kumpa mateso makali ambayo yalimsababishia majeraha na kudhoofu mwili. Aliendelea kuteseka bila kutujulisha ndugu zake, maana simu zote Gaby alizishikilia.
“Kila SMS iliyoingia, alipokea na kuijibu akijifanya yeye ndiye Christina. Kutokana na mateso kuzidi kuwa makali, Christina alishauri waende kwa wazazi wa Gaby kwa usuluhishi lakini kule nako hawakusuluhishwa, baba yake Gaby alisema wavumiliane kwani hayo ni mambo ya mapenzi.

“Akiwa amefungiwa ndani, siku moja Christina alipanda dirishani na kumuona kaka mmoja akipita barabarani, akamwita, akamtajia namba ya simu ya mama yetu ili awasiliane na amwambie jinsi anavyoteseka.
“Yule kijana alipiga simu, baada ya taarifa kufika kwetu ilibidi tuongee na askari wa Kituo cha Polisi Kitangiri lakini wakatujibu hawaingilii mapenzi ya watu.
“Baadaye Christina alifanikiwa kuzungumza na watoto wa mwenye nyumba ambayo Gaby alipanga ambayo ndiyo Christina alifungiwa ndani, akaomba msaada wa kuokolewa.

“Mama mweye nyumba alimpigia simu mumewe ambaye naye alimpigia Gaby, akamwambia amepata taarifa kuhusu Christina, akamweleza kama wameshindana bora waachane kuliko kumtesa.
“Gaby alikanusha, akasema hayo maneno hayana ukweli. Hata hivyo mateso yaliendelea, kitendo kilichotufanya tumweleze ndugu yetu mwingine anayeishi huko Mwanza atoe taarifa polisi, askari hao walienda na kumchukua Christina na Gaby hadi kituoni. Hiyo ilikuwa Agosti 14, mwaka huu.

“Agost 17, Christina alirejea Dar huku akiwa hana chochote, maana kila kitu kilibaki kwa Gaby. Baada ya hapo tukasikia Gaby alikuwa anazunguka kule Mwanza kwa marafiki zake na ile laptop, akionesha zile picha za Christina.
“Tukasikia Gaby anatangaza kwamba ataua familia yetu yote, sisi tulitoa taarifa Kituo cha Polisi Pangani. Kumbe Gaby alikuja Dar na kupanga kwenye Hoteli ya MM ambayo inapakana na nyumba yetu.

“Kwa maana hiyo, akiwa ghorofani akawa anatazama kila kilichokuwa kinaendelea kwenye nyumba yetu.
 “Gaby akawa anampigia simu Christina kumuomba msamaha. Christina akamjibu atafute kwanza daktari wa saikolojia amtibu, kisha baada ya miezi mitatu ndipo watarudiana. Akamshauri pia aende kanisani akatubu kwa dhambi alizomfanyia. Gaby alikubali.

“Jumanne iliyopita ambayo ndiyo siku ya tukio, ilikuwa ndiyo siku ya Christina kwenda chuoni Cyprus. Basi akawa anasindikizwa na mama, Alpha ambaye ni mdogo wetu wa kike na mume wangu, Kapteni Francis Kiranga, walipofika getini walimwona Gaby anakuja upande wa getini, alipowakaribia, alichomoa bastola. Mume wangu (Francis)  alipomuona, alishuka kwenye gari kwenda kumzuia asifanye jambo lolote baya.
“Bahati mbaya Gaby alianza kumshambulia mume wangu kwa risasi tano, kisha akampiga Alpha na Christina kabla ya kujilipua mwenyewe.

VIFO BILA HATIA
Mungu ana siri kubwa sana, maana pengine dhamira ya Gaby ilikuwa kumtoa uhai Christina lakini mhusika akapona, ila wasio na hatia ndiyo waliaga dunia.
Francis ambaye ni mume wa Caroline alifariki dunia siku mbili baada ya tukio akiwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili wakati Alpha, mauti yalimkuta eneo la tukio, huku Christine na mama yake, wakipata majeraha ya risasi na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.

MUNGU AWALAZE PEMA MAREHEMU
Marehemu Alpha aliagwa Jumamosi iliyopita, nyumbani kwao Ilala, Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda Goba, Bagamoyo kwa mazishi.
Mwili wa Francis, unatarajiwa kusafirishwa leo Jumanne kwenda kwao Nairobi nchini Kenya.

MWANZA WAMZUNGUMZIA GABY
Habari zinasema kuwa maisha ya Gaby kwa jumla yalikuwa ya kibabe na alikuwa mwepesi kuchomoa silaha kumtishia mtu aliyegombana naye.
“Tuliwahi kumnyang’anya bastola mara tatu, sijui kwa nini alikuwa anarudisha ile silaha yake,” kilisema chanzo chetu ndani Kituo cha Polisi Kati, Mwanza.
Hata hivyo, wapo ambao walisema Gaby alikuwa mtu mzuri na wanashangazwa na tukio zima lilivyotokea.

TAHADHARI YA WANAWAKE
Gaudencia Eliona (si jina lake halisi) ambaye amejitambulisha kuwa ni mke wa mtu, alisema kuwa matukio ya wanaume kuua kwa visa vya kimapenzi, yanaibua mengi ambayo yanafichika kwenye nyumba nyingi.

“Binafsi sina amani kabisa, mume wangu kila mgogoro kidogo anatishia kunipiga na bastola,” alisema Gaudencia na kuongeza:
“Mume wangu anao marafiki zake wanne, wote wanamiliki bastola, wawili kati yao ni wakorofi sana kwa wake zao. Jamani tunateseka, tunaishi roho mkononi.
“Katika hao marafiki wawili wakorofi, siku mmoja wao alikorofishana na mkewe, akamtishia kumpiga risasi, baadaye akaweka bastola chini ya mto, basi siku hiyo yule mke wake hakulala kwa woga.”


USHAURI KWA SERIKALI
Wakili maarufu na aliye pia Mwenyekiti wa Zamani wa Chama cha Wanasheria Tanzania, Constantine Mutalemwa, alisema kuwa anashangazwa na taratibu zinazotumika ili mtu kuweza kumiliki silaha.
 “Umefika wakati kuangalia upya sheria ya umiliki silaha nchini, kwani baadhi ya wamiliki wamekosa elimu ya matumizi ya silaha,  hivyo kusababisha matukio ya mauaji ambayo siku za hivi karibuni yamekuwa yakiongezeka,” alisema Mutalemwa.

NI KAMA UFOO SARO
Tukio la Gaby, limekuja ikiwa bado Watanzania wanakumbuka lile la Anthery Mushi, kumpiga risasi mchumba wake Ufoo Saro na mama yake, Anastazia Saro kisha naye kujilipua na kufa papo hapo.
Katika tukio hilo, Ufoo alipona, huku Anastazia akifariki dunia.

Imeandikwa na Gladness Mallya, Makongoro Oging’, Issa Mnally, Dar es Salaam na Mashaka Baltazar, Mwanza.


Credit:GPL.

MWANAMUZIKI AMANI KUTOKA KENYA AFUNGUKA NA KUSEMA AM IN LOVE.

$
0
0
Amani has been one of the most dominant women in the Kenyan music industry, lately dominating the
airwaves with her collabo with Ugandan duo Radio & Weasel 'Kiboko Changu'.

She has also kept her private life very private until now that she reveals that she has indeed fallen in love. She shared the news with her fans on her Facebook page in two short words, leaving them speculating on the who and what this means....




AMANI WAIRIMU
about an hour ago
In love.
Like ·  · Share


Who is the lucky fellow?
 

ATEMBEZWA UCHI MTAANI BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WA MTU HUKO TEGETA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

Stori: Makongoro Oging’
WANASEMA za mwizi arobaini, ikiongezeka moja mshukuru Mungu! Novemba 16, mwaka huu ilikuwa siku ya aibu kwa bosi Hussein Shaban (35)
kufuatia kudaiwa kufumaniwa katika nyumba ya kiongozi mmoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) huko Tegeta jijini Dar es Salaam.

Hussein Shaban akiwa amevuliwa nguo na kupewa kichapo baada ya fumanizi.

Sakata hilo la aina yake lilitokea katika kitongoji cha Nyeishozi, Tegeta kwa kumuhusisha Hussein ambaye ni mfanyabiashara na mke wa kigogo huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa.

CHANZO CHA FUMANIZI, KUTOWEKA AMANI
Akisimulia tukio zima mwanzo hadi mwisho, kiongozi huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema miezi miwili iliyopita alianza kuhisi ndani ya ndoa yake kuna jambo lanaloendelea kwa siri baada ya nyumba yake kupoteza amani, mke alibadilika tabia ghafla.

Bwana Hussein akitembezwa mitaani.

“Siku moja nilikuwa natafuta nyaraka za kazini ambazo nilikuwa nimeziweka kwenye begi la kubebea kompyuta mpakato (laptop), lakini sikuzikuta.
“Niligundua vitu vyangu vingi havipo ndani kama vile mashati, suruali, redio ndogo na saa ya ukutani. Nilimuuliza mke wangu akanipa majibu rahisi.

UCHUNGUZI WA KINA WAANZA
“Nilianza uchunguzi, niliwahoji shambaboi wangu kuhusu tabia ya mke wangu ambapo waliniambia kila siku nikitoka kwenda kazini nyuma kuna mtu huingia nyumbani kwangu na kukaa na mke wangu kwa muda mrefu ndani.
“Kwa kidokezo hicho, siku moja nilichukua simu ya mke wangu ya kijanjani, nikaipekua na kugundua namba moja ambayo amekuwa akiwasiliana nayo mara kwa mara. Hii namba aliisevu kwa jina la Mwajuma Jumanne.

...Wananchi wakimpiga picha Hussein aliyefumaniwa na mke wa mtu.

“Ajabu ni kwamba, kwa namba hii nilikuta ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wa mapenzi kati ya mke wangu na huyo Mwajuma Jumanne. Nilianza kuhisi kuna jambo.
“Moja ya meseji ilisema yeye (Mwajuma) hana mke! Nikajua huyo Mwajuma ni mwanaume niliyeambiwa na shambaboi kuwa huwa anakuja nyumbani kwangu.

“Pia upelelezi wangu uligundua kuwa mwanaume huyo ama huwa anamuibia vitu mke wangu au alikuwa anapewa.
“Niliwahi kuambiwa kuwa kuna siku mke wangu alimpa mwanaume huyo shilingi elfu sitini (60,000/) na akarudia tena hivi karibuni kumpa kiasi hichohicho,” alisema kiongozi huyo.

Hussein akijikinga sehemu za kichwa wakati akipewa kichapo na wananchi.

POLISI WAPEWA TAARIFA
Alisema kufuatia mambo yote hayo, aliamua kwenda Kituo cha Polisi Wazo, Dar kutoa taarifa ya kupotelewa na vitu akimtaja mwanaume huyo kwamba ndiye anayemtuhumu. Kwa ujasiri mkubwa, kiongozi huyo aliwaambia polisi kwamba mtu huyo angemtafuta mwenyewe, likafunguliwa jalada namba WP/RB//7720/2013 WIZI.

MUME AANDAA SAFARI YA UONGO
Akiendelea kusimulia mkasa huo, kiongozi huyo anasema:
“Siku ya tukio, nilijifanya nasafiri kwenda Dodoma kikazi ili kumpa mwanya mgoni wangu kujitawala, niliondoka nyumbani alfajiri huku nikiwa nimeweka wapelelezi wangu.

“Ilipofika saa tano asubuhi, Hussein aliingia nyumbani kwangu na kuanza kujimwaga kama kwake bila kujua arobaini yake ilikuwa inatimia siku hiyo.

.

..akizidi kutembezwa mtaani.

FUMANIZI LATIMIA
“Mimi na wapelelezi wangu tulivamia nyumba, tukagonga mlango, mke wangu akafungua. Aliponiona ni mimi alianguka kwa kiwewe. 
“Nilichungulia ndani kupitia dirishani nikamwona mgoni wangu akivaa shati. Alitoka mbio kuelekea getini. Nilichomoa bastola na kupiga risasi moja hewani, ikampagawisha, akataka kupanda ukuta.

“Nilipiga filimbi watu wakaja, walipojua kisa, walimvua suruali na kuanza kumpa kipigo huku wakimtembeza mpaka moja ya sehemu anazofanyia biashara zake za kuchemsha supu na kukaanga chipsi, bahati yake aliokolewa na polisi,” alisema kiongozi huyo.
Alipoulizwa alipo mkewe kwa sasa, alisema: “Nilimtimua mbio, kaondoka zake.”


Hussein akiwa ndani ya gari la polisi waliofika kumnusuru.

KAKA WA MTUHUMIWA
Kaka wa damu wa Hussein aliyejitambulisha kwa jina la Tambwe alisema kitendo alichokifanya mdogo wake ni cha aibu ila anapinga adhabu aliyopewa ya kutembezwa uchi.
“Hili tukio alilofanya mdogo wangu ni baya, hata baba yetu mdogo hapa mjini siwezi kumwambia kwa sababu linaweza kumpa presha,” alisema mtu huyo ambaye alimuwekea dhamana polisi mgoni huyo.

Kaka mwingine wa mtuhumiwa, Hamis alisema mama yao mzazi (hakumtaja jina) na bibi yao waliopo Tabora walizimia baada ya kusikia tukio hilo na wameongea kwa simu na mtendewa ili amsamehe mgoni wake.

MKE WA MTUHUMIWA
Mke wa mtuhumiwa, Pili Muhammed akizungumzia fumanizi la mumewe kwa njia ya simu akiwa Rufiji, Pwani alisema: “Mume wangu si mkweli katika mapenzi yetu tangu siku nyingi ila niliamua kuvumilia nikiamini atabadilika lakini badala yake sasa amekamatwa ugoni.”

Aliongeza: “Siku ya tukio mtoto wetu mchanga alikuwa anaumwa, nilipomuomba mume wangu anisindikize hospitali aliniambia hajisikii vizuri, akabaki nyumbani kulinda nyumba.
“Niliporudi sikumkuta na mpaka giza linaingia hakurejea, baada ya muda kidogo nikaambiwa amekamatwa ugoni yupo Kituo cha Polisi Tegeta (si Wazo). Ndiyo nikawapigia simu kaka zake wakaenda kumdhamini.”

PICHA ZA RAYUU ZENYE UTATA ZASAMBAA MTANDAONI..

$
0
0



Haijajulikana Kama walikuwa wana Act movie ama ndio mambo yaleeeeeeeeeeeee

P SQUARE WAMUUMBUA DIAMOND PLATNAM..!!KUMBE HATA HAWAMJUI,HAYA NDIYO WALIYOSEMA.

$
0
0
Mwanamuziki wa P square, Peter Okoye ameoneshwa kushangazwa na taarifa kwamba mwanamuziki wa bongo fleva Naseeb Abdul
alihudhuria harusi yake hivi karibuni nchini Nigeria na kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali akiwenmo msukumba gozi wa Totenham Hotspurs Adebayor.

Awali kupitia blogs mbali mbali kulisambaa taarifa kuwa dimond alikua mwanamuziki pekee afrika mashariki aliyealikwa katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na tajiri nambari moja afrika, Aliko Dangote.

Blogs hizo zilikwenda mbali kwa kumpamba diamond kwa vyeo vya ajabu ajabu ikiwemo Michael Jackson wa afrika mashariki jambo ambalo lilisababisha wengi kumponda.

Akihojiwa na kituo cha EATV mara baada ya kuwasili jijini Dar kwa ajili ya shoo iliyopigwa viwanja vya leaders club, Okoye alishangazwa na taarifa za dimond kuhudhuria katika harusi yake.


Okoye alikua akijibu swali aliloulizwaa na mtangazaji wa kipindi cha HotMix Adrian Hilary kuhusu diamond kuhudhuria harusi hiyo ambapo alionesha kushangazwa na jina hilo na kuhoji Diamond ni nani?

Kushangaa huko kulimaanisha licha Diamond kujichezesha mbele ya Okoye siku ya harusi yake lakini mwanamuziki huyo hakua akijua aliyekua akimzungushia viuno vya ngololo ni nani. 

FOLENI ZA DAR ZAMSABABISHA HUYU MBUNGE WA SINGIDA MJINI KUPANDA BODA BODA.

$
0
0
“The traffic in Dar is crazy,I was so fed up sitting in the car, I had to rent a(Boda Boda) 2 make it 4 a meeting, I guess I need a chopper,” alitweet.
Huenda wazo la kununua chopper akalifikiria kwa nafasi kubwa zaidi ili kuepukana na foleni kali wakati mwingine na hivyo kushindwa kuhudhuria mikutano ya maana.

AKATWA MIKONO NA MIGUU BAADA YA KUCHOMA SINDANO YA KUONGEZA MAKALIO.STORY NA PICHA ZIKO HAPA.INAUMA.

$
0
0

http://www.theclicktz.com
Imetokea huko Amerika Dada mmoja anayeitwa Apryl Michelle Brown, ambaye alienda kuchoma sindano ya kuongeza makalio kwenye kituo fulani cha urembo na afya huko marekani alifanya hivyo kwakuwa hakuwa ameridhika na ukubwa wa makalio yake na kufanya uamuzi wa kutafuta mbinu ya kuyaongeza.

Dada huyo baada tu ya kuchoma sindano hiyo alikaa mwezi mmoja nakuanza kupata maumivi makali kwenye miguu yote miwili na mikono alifanyiwa uchunguzi na kubainika kuwa sindayo aliyochoma haikuwa sahihi na matokeo yake ni kusababisha sumu mwilini, wataalamu waliongezea kuwa sindano hizo huchomwa kulingana na Mwili wa mtu pia aina na uwezo wa chembe chembe zake za damu. Inasemakana aliyechoma hakuangalia ni aina gani ya sindando ambayo ingeweza kuendana na mwili wa dada  huyo. Hivyo kumpelekea dada huyo kutopata nafuu nabadae wataalamu kuamua kumkata Mikono yake na miguu. Dada huyo akilezea vyombo vya habari kuwa " nitajutia maisha yangu yote kwa jambo nililo fanya". INASIKITISHA: WAKIDADA HILI NI FUNZO KWENU..!! 


source:The clicktz

MWAIGULU NCHEMBA ANENA MAZITO KUHUSU SAKATA LA ZITTO KUVULIWA MADARAKA.

$
0
0
Jisomee Mwenyewe Hapo Juu ....Dahhh 

DIAMOND PLATNUMZ AAMUA KUJIITA 'DOMO' INSTAGRAM.

$
0
0
Diamond Platnumz aka Prezident wa WCB ametoa kali na mpya kwa kuamua kujiita 'DoMo' kupitia
ukurasa wake wa Instagram kama unavyo ona hapo chini. Yawezekana amefikia hatua hiyo baada ya watu wengi kumkashifu mara nyingi sababu ya mdomo wake. 

SERIKALI YA ANGOLA YAZUIA DINI YA KIISLAM NA KUVUNJA MISIKITI YOTE.

$
0
0
Angola bans Islam and shuts down all mosques
across the country because it 'clashes with state religion of Christianity'

Minister of culture described Islam as a 'sect' which is banned as counter to Angolan customs and culture
Nation's president said: ‘This is the final end of Islamic influence in our country'

Angola has reportedly declared Islam illegal and ordered for all of the country’s mosques to be closed down.

Minister of culture Rosa Cruz e Silva said that mosques in the largely Christian country would be closed until further notice.

She described Islam as a ‘sect’ that would be banned as counter to Angolan customs and culture.

Angola (capital, Luanda, pictured) has reportedly declared Islam illegal and ordered for all mosques to be closed

There are unconfirmed reports that mosques across the African country are being destroyed, according to the International Business Times.

President Jose Edurado dos Santos reportedly told the Osun Defence daily: ‘This is the final end of Islamic influence in our country.’
Along with Islam, which is a religion associated with less than 1 per cent of the population of 19 million, 194 other ‘sects’ have been banned in the nation, where more than half the population is Christian.

Ms Cruz e Silva said: ‘The legalisation of Islam has not been approved by the Ministry of Justice and Human Rights [and] their mosques will be closed until further notice.’

Clashes between Christians and Muslim people are frequently reported in the local media.

source.Angola bans Islam and shuts down all mosques | Mail Online 

Video:Angelina Jolie amnunulia Brad Pitt kisiwa chenye umbo la moyo.

$
0
0
Angelina amechagua kisiwa hicho chenye umbo la moyo linaloashiria upendo, lakini pia hii inaweza kuwa zawadi bora zaidi kwa Brad Pitt kwa kuwa kuna nyumba mbili katika kisiwa hicho ambazo zimekuwa designed na mbunifu majengo Frank Lloyd Write ambaye amekuwa akipendwa  zaidi na Brad Pitt.
Chanzo kimoja kimeiambia The Mirror kuwa Angelina alikifukuzia kisiwa hicho mara tu aliposikia kuwa kiko sokoni kwa kuwa alijua kimekaa kimahaba na kinaweza kuwa sehemu nzuri ya kuishi familia yake kwa kuwa kimejitenga vizuri kwa maisha binafsi.
Kisiwa hicho kiko katika eneo la kisiwa cha Petra, Miles 50 kutoka katika jiji la New York. Ina eneo la ekari 11, na vitu vingi vya luxury.
Angalia video hapa:

Jokate Mwegelo feki Awatapeli Watu kwa njia ya Mtandao.

$
0
0
j3Licha ya faida ambazo watu maarufu wanazipata kupitia social media lakini hii ni moja kati ya hasara kubwa wanazozipata pia kupitia mitandao hii ya kijamii.

Leo hii @jokatem amewapa habari fans wake kuhusu account feki iliyopo kwenye instagram kwa jina la Jokate Urbun Mwegelo ambapo taarifa kutoka kwa Jokate ni kwamba ushafanyika utapeli kupita hiyo account.
“Poleni kwa wale waliotapeliwa laki tatu,simu etc. Hii ni account  fake na sipo kwenye insta message. Samahani kwa usumbufu wowote uliojitokeza. Waambie na wenzenu napata wasichana wengi wanalalamika na ahadi hewa zinazotolewa kupitia account hiyo”. Hii ni tafsiri ya maneno aliyoaandika Jokate.
j1
Hapo chini ndiyo account feki ya Jokate Instagram anatumia jina la JokateM
j2


MAMA MMOJA TOKA MAREKANI AMEPIGIWA SIMU NA SHETANI NA KUPOKEA SMS 48 ZA SHETANI.STORY NZIMA NA PICHA IKO HAPA.

$
0
0
Mama mmoja toka Colorado nchini Marekani alipokea simu ya ajabu usiku mmoja wa manane kutoka kwenye namba 1-666-666-666 na ndani ya masaa machache alipokea meseji nyingi sana kutoka namba tofuti tofauti na zote zikiwa zimeandika ‘Satan’ kwa maana ya 'Shetani'.

Mwanamke huyo, Jenn Vest kipindi kipindi anatumiwa meseji hizo alikuwa anasinzia wakati akiwa bado anaendelea kumnyonyesha mtoto wake na ndipo aliposikia simu inaita ikipigwa kutoka namba 1-666-666-666.

Ahukumiwa Kifo cha Kupigwa Mawe Mpaka Kufa Mara Baada ya Kumbaka na Kumpa Mimba Dada Yake.

$
0
0
Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 30 aliyefahamika kwa jina la Umar Mohammed Kandahar amehukumiwa kifo cha kupigwa mawe mpaka kufa na mahakama ya Upper Sharia ya Bauchi mara baada ya kumbaka na kumpa mimba mdogo wake wa kike.

Alikuwa Mwanaume na Sasa Amejibadilisha na Kuwa Mwanamke.

$
0
0

Huyu ni modo na mwanamuziki toka nchini Nigeria ambaye pia ni Miss saHHara, alizaliwa akiwa mwanaume kamili.


Jana kupitia makala moja ikiwa ni katika maadhimisho yao alielezea kwa vile alivyonyanyasika kwa kufungwa na hata kufikia hatua ya kutishiwa kuuwa ila kwa sasa anafurahi kwa kujiona yupo huru.

Dunia yetu ndio hii...!

MFANYABIASHARA MAARUFU DAR AFUMWA AKILA URODA NA DENTI WA PRIMARY.

$
0
0
MZEE mmoja kigogo wa biashara ya kuuza mbao jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alinaswa kitandani
ndani ya chumba akiwa na mrembo aliyedaiwa ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi Tegeta Wazo, Dar.Mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kyando, anasemekana amekuwa na ukaribu na denti huyo anayeitwa Fatty kwa siku nyingi, kitu ambacho kiliwapa maswali baadhi ya majirani wa nyumbani kwa msichana huyo.

Katika harakati za kuchunguza ukaribu wa msichana huyo na mtu mzima huyo, mama mdogo wa binti aligundua kuwa wawili hao wana ukaribu usiofaa.

Ikaelezwa kuwa, mama mdogo wa mwanafunzi huyo aliponyetishiwa ishu hiyo, aliandaa mtego unaofyatuka kwa kasi kuliko ule wa panya ili kumtia mikononi mzee huyo mpenda kukaa na watoto wa wenzake.

“Mtego mkali uliandaliwa, siku ya siku, ma mdogo huyo alijifanya anakwenda mbali na nyumbani, binti akaona dakika tisini za mchezo lazima aibuke kidedea wa mahaba, alimwita mwanaume huyo na kumkaribisha chumbani, kumbe arobaini zao zilikuwa zimetimia,” kilisema chanzo.
Mashuhuda wa sakata hilo walidai kuwa mama mdogo na watu wengine waliwanasa wawili hao wakiwa juu ya kitanda kama walivyozaliwa, bila kufafanua walichokuwa wakikifanya.


Ili kushika ushahidi mkononi, mama mdogo wa binti huyo na wapambe wake walipiga picha za mnato na za video kisha wakaanza kumuuliza maswali ‘mlalamikiwa’ ambaye inaaminika ni mume wa mtu.

Haikuelezwa wazi ni maswali ya aina gani aliyokuwa akiulizwa lakini inadaiwa yalihusu historia ya kujuana kwao.

 Aidha, inadaiwa kuwa mama mdogo huyo alitaka kumtwanga ndoa ya mkeka mfanyabiashara huyo lakini chondechonde zake nyingi zilimwokoa na kuahidi kurejea siku inayofuata kwa ajili ya kukata mshiko wa fidia baada ya kuambiwa binti huyo bado anasoma na shuleni kulilipwa fedha nyingi.

Habari nyingine zinadai kuwa wawili hao walifahamiana miezi kadhaa nyuma kupitia lifti ya gari ambayo mshitakiwa alimpa mrembo huyo maeneo ya Boko, jijini Dar.

KIJANA MIAKA 32 ANASWA NA BIBI KIZEE MIAKA 80.

$
0
0
Stori Kutoka Global Publishers
KUNA mengi ya kushangaza duniani lakini hili la kijana Hamad Issa (32) kunaswa faragha na bibi kizee Adela Mkalau (80) linaongeza rekodi ya mambo yanayoshangaza, Risasi Mchanganyiko lina kila kitu.
Hamad Issa (32) akiwa amejilaza kitandani kwa bibi Adela Mkalau (80).
Tukio hilo la kustaajabisha limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita, nyumbani kwa bibi huyo, Yombo –Buza, jijini Dar es Salaam ambapo wajukuu wa bibi huyo ndiyo waliomnasa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wajukuu wa bibi huyo walifedheheshwa na kitendo hicho hivyo kuwawekea mtego na kuwanasa kisha kumfikisha Hamad katika Kituo cha Polisi Chang’ombe kwa tuhuma za ubakaji.
Bibi Adela Mkalau (80) akiwa katika pozi.
BIBI: SIJABAKWA
Katika kutafuta uhakika wa madai ya wajukuu hao, polisi wa Chang’ombe waliagiza bibi yao aitwe ili athibitishe madai hayo wakati upelelezi mwingine ukiendelea.
Sosi wetu alisema kuwa bibi aliwaacha hoi polisi baada ya kufika kituoni hapo na kukataa maelezo ya wajukuu zake, huku akisisitiza hakubakwa bali walikubaliana na Hamad.
Baada ya bibi huyo kuondoa utata, polisi walikubali kumuachia Hamad kisha wajukuu wakafunguliwa kesi ya kushambulia na kudhuru mwili iliyoandikishwa kituoni hapo kwa jalada namba CHA/RB/10629/2013.
Hamad Issa akiwa kitandani, pembeni kulia ni bibi Adela Mkalau.
BIBI NA RISASI
Risasi Mchanganyiko lilifunga safari hadi nyumbani kwa bibi huyo na kuzungumza naye kuhusu tukio hilo ambapo alisema: “Sijabakwa na nimekasirishwa sana kwa kitendo cha kumpiga kijana wangu. Wawe na heshima kwa babu yao. Sisi tunapendana, kwa nini wanatuingilia?”
Alisema: “Siku hiyo Hamad wangu alikuja nyumbani kwangu tangu mapema. Nikaandaa chakula cha jioni, tukala pamoja kisha tukalala.
“Tukiwa usingizini, nikasikia mlango unagongwa. Kwenda kufungua, wajukuu zangu wakaingia na kuanza kumpiga Hamad na fimbo na magongo, wakisema eti amenibaka. Hamad atanibakaje? Kwani mimi ni mtoto mdogo?
“Isitoshe wanamfahamu vizuri sana Hamad. Nipo naye  mwaka mmoja na nusu sasa, leo inakuwaje wanajifanya hawamjui? Siku hizi mambo yamebadilika. Mdogo anaweza kumpenda mkubwa na mkubwa akampenda mdogo. Hakuna kosa.”
Adela Mkalau akiwa kwa bibi.
MSIKIE DOGO
Mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwa Hamad ambapo alimkuta akiwa hoi kitandani kwa majeraha ambapo alisema: “Ni kweli bibi ni mpenzi wangu... na wale wajukuu zake wananifahamu vizuri sana. Wamenipiga sana, eti nimembaka bibi yao. Siyo kweli. Sisi ni wapenzi.”
Alipoulizwa anajisikiaje kuwa kwenye uhusiano na kikongwe huyo, alijibu: “Hata mimi nashangaa sijui imekuwaje nikampenda. Nimejikuta nipo kwenye uhusiano naye na kwa kweli tunapendana sana.”
WAJUKUU WANASEMAJE?
Mmoja wa wajukuu wa bibi huyo, Margaret Cheba, akizungumza na gazeti hili kuhusu tukio hilo alisema bibi yao amewadhalilisha sana na wanaona aibu kupita mitaani kwa kitendo cha kutembea na Hamad.
“Hili jambo limetufedhehesha sana sisi wajukuu zake halafu hata kimila ni tatizo, hairuhusiwi kabisa. Mbaya zaidi, bibi yetu ni mgonjwa. Anasumbuliwa na moyo... sio wa kufanya kitendo kama kile kabisa na sisi ndiyo tunamsaidia lakini inashangaza polisi wametubadilikia kabisa,” alisema Cheba.

Papa Francis Akabidhiwa Jezi Namba 10 Yenye Jina Lake Mgongoni na Rais wa FIFA

$
0
0
Rais wa FIFA, Sepp Blatter hivi karibuni alimtembelea Pope Francis ndani ya Vatican, na
katika ziara yake hiyo alimkabidhi Papa huyu maarufu jezi ya FIFA yenye namba 10 huku ikiwa na jina lake mgongoni.

Papa mwenye umri wa miaka 76 ni mmoja kati ya watu wanaopenda sana mpira wa miguu, alizaliwa ndani ya Argentina, kama mtoto wa wazazi wenye asili ya Italia.

"ATAKAYESHIDWA KUMUDU GHARAMA MPYA ZA UMEME ATUMIE KIBATARI" KAULI HII YA NAIBU WAZIRI WA NISHATI YAMPONZA.

$
0
0
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemtaka Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene, kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kutoa kauli ya kukatisha tamaa.

Simbachawene,  juzi alitoa kauli ya serikali ya kupandisha bei ya umeme kama Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), lilivyoomba hivi karibuni kutaka kuongeza gharama za nishati hiyo kwa asilimia 68.
  
Alisema ni ukweli usiopingika kuwa hata TANESCO ikiongeza gharama za umeme hadi kufikia sh 800 kwa uniti bado bei hiyo itaendelea kuwa nafuu ukilinganisha na  gharama za kununua mafuta ya taa.

Simbachawene alitoa tahadhari kwamba endapo kuna mwananchi yeyote atakayeona gharama za umeme ni kubwa ni vema akaamua kuwasha kibatari au akae gizani.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano jana, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba, alisema kuwa kauli hiyo inaweza kusababisha vurugu kutokana na suala la umeme kumgusa kila Mtanzania.

Alisema kuwa hivi sasa viongozi wamekuwa wakitoa kauli za kuudhi ambazo ni hatari kwa ustawi wa taifa.

“Tunakumbuka kauli za kuudhi zinavyozidi kushamiri wakti ule aliyekuwa Waziri wa Fedha Basili Mramba alipowaambia Watanzania wajifunge mikanda kubana matumizi hata ikibidi kula majani watakula, lakini ndege ya rais lazima inunuliwe; akaja Waziri wa Ujenzi John Magufuli aliyewaambia wakazi wa Kigamboni kuwa kama hawawezi kulipa ongezeko la nauli mpya basi wajifunze kupiga mbizi, ili kuvuka kwa kuogelea, wanaporudi vijijini au wazunguke kupitia Kongowe sasa hii ya vibatari!”alisema.

Alisema kuwa ni muhimu viongozi wakahakikisha wanatoa kauli zilizo na hekima ili kuepusha migogoro.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa baada ya serikali kupandisha gharama hizo, muathirika mkubwa ni mwananchi wa chini.

Alisema kuwa wamiliki wa viwanda wanachoangalia ni faida hivyo kupanda kwa bei ya umeme kutasababisha gharama za bidhaa kuzidi kuwa juu zaidi.

“Nchi za wenzetu hakuna jambo linaloweza kufanywa bila kushirikisha wananchi lakini hapa kwetu wanaamua tu na mbaya zaidi wanakuja na kauli za kuudhi na kukatisha tamaa kwa kuwa Watanzania ni wapole,” alisema.

Dk. Bisimba alisema kuwa ni lazima wafahamu kuwa upole wa Watanzania utafikia kikomo na hiyo inaweza kusababisha hatari kwa taifa.

Wiki hii wadau mbalimbali wa umeme likiwamo Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC), walipinga maombi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ya kuongeza gharama za umeme kwa asilimia 67.8.

Walisema ongezeko hilo ambalo limelenga zaidi viwanda vikubwa na vya kati litasababisha kupanda kwa bei za bidhaa za viwandani.

Mjumbe wa Bodi ya CTI, Samuel Nyantahe, alisema kabla TANESCO haijapandisha gharama hizo ingekusanya madeni yote na kuziba mianya ya wizi wa umeme.

Naye Mjumbe wa CCC Thomas Mnunguli, alisema ongezeko hilo ni kubwa na linakosa uhalali hivyo TANESCO ijitathmini na kujipanga upya na ilenge kutoa huduma bora na nafuu.

-Tanzania Daima

UKWELI WA ISHU YA SNURA NA MRISHO NGASSA.

$
0
0
Ni picha ambazo zimekua zikizungumziwa kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye mitandao
mingine ya habari nchini Tanzania zikimwonyesha mchezaji wa Yanga Mrisho Ngassa akiwa mapenzini na mwimbaji Snura wa bongofleva.

Snura anasema mwanzo wa hizi picha kusambaa ni baada ya kupoteza simu yake, namnukuu akisema ‘hizo picha hazina uhusiano wowote unaounganishwa kimapenzi kati yangu na Ngassa ila ni sehemu ya vipande vya movie yangu inaitwa ‘Majanga’ ambayo nimeanza kuifanya na Ngassa amecheza ndani yake kwenye scene za mapenzi, yani Snura kwenye movie amecheza kama binti mrembo anaerukiarukia Wanaume’

‘Simu yangu ilipotea ndio maana wamezipata hizo picha, wakati tunashoot tulikua tunapigapiga tu hayo mapicha, mi sikuwa nataka kuzitoa kabisa manake movie yenyewe bado naifanya nusunusu kutokana na kukosa muda, hii ishu imeniletea sana matatizo manake mwingine anakua haamini unachokiongea na hakuna kitu kinauma kama kuongea ukweli alafu mtu anasema unadanganya’ – Snura

Kwa kumalizia Snura anasema ‘Ngassa alinipiga muda mfupi tu baada ya picha kuanza kusambaa akauliza mbona hizi picha zinasambaa hivi Snura? nikamwambia usinielewe tofauti babaangu kwa sababu mimi mwenyewe sikutaka zitoke, picha nilizopiga nyinginyingi tu wakati tunatengeneza movie ila naona watu wameona hizi ndio nzuri kwa skendo’ 
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live