Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live

WASTARA ANAJUTA KUMFAHAMU HUYU MWANAMME.

$
0
0
Juzi na jana kulikuwa na habari katika gazeti na mitandao mingi kuwa Wastara na Bond Bin Suleiman ni wapenzi na wamekuwa wakifanya siri sana huo uhusiano wao. Habari ambazo zilinukuu chanzo kimoja zilieanda mbali zaidi zikisema huenda Bond ana tabia ya kufanya mapenzi na mwanamke kotekote kwani aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Lulu Semagongo(Anti Lulu) alidaiwa kuwahi kukaririwa akisema kuwa anapenda sana kufanya mapenzi kinyume na maumbile na hawezi kuacha tabia hiyo. 

Baada ya habari hizo kusambaa ilibidi blog yetu  kuwatafuta mastaa hao wawili na wa kwanza kupatikana alikuwa ni Wastara na alikana kuwa katika penzi na Bond ila alisema wanafanya kazi pamoja kwani kwasasa wanashuti filamu mpya ya Bond inaitwa Uaminifu Dhaifu. Aliongeza kwa kusema kuwa Bond ni kama kaka yake. "sina mahusiano na Bond zaidi ya kikazi tu na zile picha zote ambazo unaziona ni wakati tupo location tukiandaa filamu yake inaitwa Uaminifu Dhaifu, huo ndiyo ukweli, bora mume wangu angekuwepo haya yote yasingetokea

Baada ya hapo ilibidi kumgeukia Bond ambaye yupo location wakimalizia filamu hiyo na alipoelezewa hayo alisema hana uhusiano wa kimapenzi na Wastara na picha zinazodaiwa kuwa ni wapenzi ni za filamu mpya ambayo tuliweka hata hapa katika blog yetu, alisema kuwa huyo Anti Lulu anatafuta kuandikwa tu kwenye magazeti ndiyo maana anatoa habari hizo zisizo za kweli ili kujipatia umaarufu "Sio kweli ni picha za kazi tu ambazo hata wewe nilikutumia magazeti yanazigeuza, Lulu achana nae anatafuta kuandikwa, tulishachana kitambo wala hatuna mawasiliano. 

Adam Juma amjibu Nisher, amwambia asitafute ustaa kwa chatu aliyelala.

$
0
0

Muongozaji mkongwe wa video, Adam Juma  ameamua kujibu ujumbe wa kejeli alioandikiwa na muongozaji wa video aliyekuja juu nchini, Nisher.

Nisher alipost picha yenye maneno yanayoonekana kuwa dongo kwa Adam Juma ambaye anaaminika kuwa na mchango mkubwa katika kubadilisha muonekano wa video za muziki za Tanzania.
Kwenye picha hiyo, Nisher aliandika: I’m not next level, I’m a new game’.
‘Next Level’ ni jina la kampuni ya Adam Juma.
Ujumbe huo ulimkera Adam aliyesema kuwa Nisher anamtafuta na kumwambia kuwa asianzishe vita ambayo hawezi kuimaliza.
“Afanye kazi yake asitafute ustaa kwa chatu aliyelala. Ajitahidi wasanii wasiende Ogopa basi. Changamoto my ass. Ukimya si upuuzi but ni busara, sijapenda hii msg, but anyway I got something for you,” aliandika Adam kwenye Instagram.
“On that note atafute mchiriku na mduara mmoja tuone creativity. In the end if you good I will respect you.” Aliongeza Adam Juma.

MAAJABU!! MAITI HUFUKULIWA MAKABURINI ILI KUBADILISHWA NGUO KATIKA KISIWA CHA SULAWESI HUKO INDONESIA.

$
0
0


KILA mwaka huko kaitika kisiwa cha Sulawesi, Tana Toraja, Indonesia, wafu (au maiti) hufukuliwa kutoka makaburini ili kubadilishwa nguo na kuwatembeza kijini hapo. Watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila ya ajabu inayoiitwa Ma'nene  ambayo wanaamini mtu akifa bado yuko nao kwa hiyo inawalizimu kufanya mambo hayo kama kuwabadilisha nguo.

Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.
Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”.

Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.

Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”.

HAYA NDIO MANENO MAZITO YA MH ZITTO KABWE JUU YA MAREHEMU AMINA CHIFUPA.

$
0
0

Hii picha ni ya May, 2011 kipindi ambacho Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe alienda
kutembelea kaburi la rafiki yake kipenzi Marehemu Amina Chifupa aliyekuwa Mbung wa CCM Kupitia Vijana Alipotembelea Kijiji Cha Lupembe, Mkoani Njombe. Mbunge huyo anaendela kumkumbuka Amina kila siku kwa ujasiri wake na matendo yake yakutaka mabadiliko nchini. Na hivi leo kupitia ukurasa wake wa facebook ameandika maneno haya:



HAPANA CHEZEA KIROBA WEWE!! ONA ILIVYOMFANYA HUYU MWANAJESHI.

MH SUGU,MBUNGE WA MBEYA MJINI AIPONGEZA CHADEMA KWA KUMVUA MADARAKA ZITTO KABWE.ASEMA ENOUGH IS ENOUGH.SOMA MWENYEWE ALICHOPOST.

Mbunge anayelelewa na wake zake mama ntilie.

$
0
0

 Aliyekuwa mbunge wa Songea mjini, Abdulrabi Ali Yusuph(66) akizungumzia maisha yake baada ya kufungwa jela akiwa nyumbani kwake hivi karibuni. Picha na Lauden Mwambona. . 

Aliyekuwa Mbunge wa Songea mjini kuanzia Oktoba 1985 hadi Aprili 1988 alipofungwa jela miaka 11, Abdulrabi Ali Yusuph (66), amesema tangu atoke gerezani hadi sasa anaomba aonane na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ama Rais Benjamin Mkapa na hata Rais Jakaya Kikwete lakini hajafanikiwa hadi leo.
Amesema aliomba nafasi ya kumwona Rais Mwinyi akiwa madarakani ili amweleze ya moyoni, lakini hakufanikiwa na aliendelea kuomba amwone Rais Mkapa hakufanikiwa na sasa anaomba amwone Rais Kikwete bado hajajaaliwa.
Alisema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea ambako anaishi akiwa kwenye nyumba chakavu ya urithi na wake zake wawili pamoja na watoto kadhaa.
Mahojiano ya mwandishi na mbunge huyo yalianza hivi.
Mwandishi: Mheshimiwa habari za siku nyingi. Nimefika hapa kwa niaba ya jarida la Ndani ya Habari linalochapishwa na gazeti la Mwananchi, lengo hasa ni kukujulia hali. Watu wangependa kujua unaendeleaje hasa baada ya kifungo chako. Ningependa kupata maelezo yako juu ya masuala ya maisha ya gerezani na ya sasa ukiwa huru.
Mbunge. Kwanza kabla ya yote. Wewe upo hapa ili uuze gazeti na upate fedha. Je, mimi unanieleza vipi kuhusu mapato hayo.
 Mwandishi: Kazi ya mwandishi siyo biashara, bali ni  ya kijamii. Kazi ya mwandishi ni kuelimisha, kufundisha, kuibua kero na kutaarifu jamii. Kazi ya mwandishi inaweza kukusaidia ama kukuharibia kwa kuibua mambo ambayo unaweza kufanya kwa kuvunja sheria na kuitisha jamii.
Mbunge: Kwa maneno yako haya ni kwamba mimi sina lolote la kufaidika leo?
Mwandishi: Ni kweli sikuja hapa kibiashara bali kukusalimu na kupata hisia zako ama kauli yako baada ya kufungwa jela kwa miaka 11  ukiwa mbunge na sasa upo nje, hivyo tunapenda kujua uliishi vipi jela na jamii inakuonaje baada ya kutoka?
Mbunge:Basi kwa kuwa umefika hapa, nitasema machache, lakini kama utakuja baada ya kujipanga, nitaeleza mengi  mno. Mimi ninazo kero na mambo mengi baada ya kuishi gerezani na kwa kweli nina masikitiko mengi ambayo yananisononesha sana.
Mwandishi:Nashukuru Mheshimiwa, naomba udokeze hisia zako walau kidogo.
Mbunge: Kwanza  ninayo masikitiko mpaka leo kwa viongozi wakuu wa taifa hili. Nasikitika mpaka leo kwa kunyimwa nafasi ya kuonana na walau mmoja kuanzia Rais wa  awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na hata awamu ya nne Jakaya Kikwete.
Mimi ninayo mambo mengi sana kwa viongozi wetu, Serikali na hata kwa taifa, lakini nasikitika kuona waliokuwa viongozi wenzangu wamenitenga kana kwamba mimi ni shetani’’ anasema.
Mimi nilibambikiwa meno ya tembo na hatimaye nilifungwa jela, nilichojifunza cha kwanza ni kwamba jamii  ina tabia ya kuwanyanyapaa waliowahi kufungwa jambo ambalo hata viongozi wa taifa nao wanatekeleza kwa vitendo juu yangu. Wapo viongozi wenzangu ambao wakati ule tulicheka pamoja, tulikula pamoja na kucheza pamoja, lakini baada ya mimi kwenda jela  hawaonekani.
Kufungwa kwangu kulipangwa
 Mwandishi:Unasikitika kwa  kufungwa kwako ama kunyanyapaliwa?
Mbunge:Mimi baada ya kufika gerezani nilijiuliza swali  la kwanini nimefungwa? Maana ukweli ni kwamba meno ya tembo siyo yangu. Baadaye nilipata jibu kwamba nilifungwa ili nikaone mambo maalumu magerezani. Mambo niliyoyashuhudia  yanatisha. Lakini la kwanza ni kwamba siyo wote wanaofungwa wanatenda makosa waliyoshtakiwa nayo. Pili niligundua kwamba askari magereza si wabaya wakiwa kazini, bali wabaya ni waliokupeleka kwao.
Pia nilijifunza kwamba askari magereza wanafanya kazi katika mazingira magumu kiasi kwamba wanafika hatua ya kuomba msaada kwa wafungwa. Pia niliona wazi kwamba wapo wafungwa wanaorudi gerezani kwa kupenda huku wengine wakirudishwa gerezani kwa hila za udhalimu.
Nilishuhudia kunyongwa kwa wafungwa 11 na nilishiriki kusafisha vitanzi vyao, miongoni mwao, wapo walionyongwa huku wakikana kutenda makosa waliyoshtakiwa nayo.
 Mwandishi: Maisha yalikuwaje gerezani?
Mbunge:Baada ya kuhukumiwa kufungwa nilitoka gereza la Songea kwenda gereza la Lilungu Mtwara,  baadaye nilipelekwa  Ukonga Dar es Salaam na hatimaye  Gereza la Maweni Tanga. Cha kushangaza katika magereza yote mimi nilikuwa mnyapala mkuu na pia imamu wa kuswalisha Waislam waliofungwa.
Aporwa mke baada ya kufungwa
 Mwandishi:Ukiwa jela , je uliifikiriaje familia yako?
Mbunge:Kwa kweli nasema wazi kwamba suala la kufungwa kwangu lilipangwa na watu mbalimbali. Nasema hivi kwa sababu baada ya miezi mitano hivi , kiongozi wa dini ya Kilokole alinifuata nikiwa Gereza la Lulindi na kuniambia kwamba mke wangu alimbadilisha dini na kuwa mlokole na aliamua pia kumuoa.
Mpaka leo mke wangu wa kwanza ambaye nilizaa naye watoto sita hatujarudiana na amesababisha baadhi ya watoto wangu wawe walokole hadi leo
Mwandishi: Kwa hali hiyo huna mke mpaka sasa?
Mbunge. Hapana, kwa sasa nina wake wawili na watoto, watoto, eeeh nina watoto kadhaa.
Mwandishi: Ulifungwa  miaka tisa nwaka 1988 , lakini ulikata rufaa ambayo ulishindwa na hatimaye kufungwa miaka mitatu zaidi, lakini ulitoka kwa msamaha wa Rais ikiwa imebaki miezi minne, je ulijisikiaje?
Mbunge: Nakumbuka nilitolewa siku ya Ijumaa. Basi nikaanza kuifikiri sana siku hiyo kuwa ina maana kubwa kwangu. Nasema hivyo kwa sababu nilizaliwa Ijumaa, nilikamatwa kwa tuhuma za meno ya tembo siku ya Ijumaa, nilihamishwa kutoka Songea kwenda Lulindi siku ya Ijumaa na hatimaye kuachiwa siku ya Ijumaa. Jambo hili lilinipa wasiwasi  na kujiuliza mara kadhaa maana yake ninni. Lakini mama yangu mzazi aliyefariki mwaka juzi nakumbuka alinisihi nimshukuru sana Mungu kwa siku yake ya Ijumaa kuifanya kuwa ya matukio makuu.
Mwandishi:Ukiwa gerezani kuna mambo gani unaoyakumbuka zaidi.
Mbunge: Kwa kweli nayakumbuka yaliyokuwa yakitokea nje ya gereza juu yangu. La kwanza linalonisikitisha sana ni taarifa ya Kiongozi wa Bunge (anamtaja jina) ambaye aliwahi kulitangazia Bunge na Taifa kwa ujumla kwamba aliyekuwa mbunge na kufungwa jela Abdulrabi Ali Yusuph amefariki dunia.
Jambo hili lilinisikitisha sana. Nilimwambia Marehemu Dk Laurence Gama akiwa mbunge jambo hilo kwamba nilikerwa sana na alinihakikishia kulimaliza.
Jambo la pili  lililonishtua ni kauli ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi alipotamka kwamba Serikali yake haina upendeleo katika masuala ya dini akitoa mfano kwamba padri Erio aliyekamatwa kwa makosa ya kuvunja sheria aliamwaachia, lakini ameamua Muislam mwenzake akitaja jina langu aendelee kusota jela. Kauli ile ilinihuzunisha kwa vile kwanza kosa lilikuwa la kubambikiwa na pili kiongozi mkuu anatangaza kuniacha nisote jela.
 Mwandishi: Pamoja na kwamba unasema jamii ina mwelekeo wa kuwanyanyapaa wanaofungwa, je wapiga kura wako nao walitekeleza hayo?
Mbunge: Baada ya kutoka gerezani,  wapo  wana CCM waliofika na kunitaka niwe kiongozi ngazi ya wilaya, kata na hata mtaa, lakini nilisita sana ingawa baadaye nilikubali kuwa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mfaranyaki hadi mwaka jana. Kwa ujumla utendaji wa CCM kwa sasa umebadilika sana. Hauna shukrani hata kwa waasisi wake. Mimi nina historia ndefu ya Chama hiki. Baba yangu marehemu  Abdulrabi Yusuph ndiye aliyekuwa Katibu wa kwanza wa Chama cha TANU. Baba yangu ndiye aliyefanya kazi na Nyerere kwa dhati.
 Mwandishi: Viongozi wa Serikali wanaweza kukusahau, je wale wa CCM nao?
Mbunge: Nakueleza baada ya kufungwa, wana CCM walinisahau kabisa , lakini siku moja dada yangu alikwenda Uwanja wa Majimaji alipotembelea Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi na kumwangukia miguuni.
Askari na vyombo vya usalama vilitaka kumfunga dada yangu, lakini Rais aliagiza mwanamke huyo afike Ikulu Songea ambako alikwenda na kuomba Serikali isaidie kuwasomesha watoto wangu wawili ambao alikuwa akiishi nao mimi nikiwa jela.
 Basi nashukuru Mwinyi aliagiza CCM iwasomeshe watoto wawili ambao kweli walisomesha hadi kidato cha nne wakati mimi nikiwa jela.
Credit:Mwananchi.

HUYU NDIO MSANII WA VITUKO SHOW ALIYEPIGWA NA MKE WAKE KIPIGO CHA PAKA MWIZI.

$
0
0
HUYU ndiye msanii  niliyemzungumzia wiki iliyopita kuhusu kichapo alichopewa kama mnavyomuona hapo pichani.


Anatambulika kwa
jina  ''Kazi Kijeba''.. MSANII kutoka kundi la BONGO SUPERSTAR'S COMEDY linalorusha kipindi chake maarufu hapa nchini (VITUKO SHOW) Kinachorushwa katika runinga ya CHANNEL TEN Kundu  hili limeweka kambi ya takribani miaka miwili mkoani Tanga.

Nafikiri chazo cha habari cha wiki iliyopita hakikufafanua kisa kwa kina, Leo tarehe 27/11/2013 Website ya Masai Nyotambofu iliweza kuongea na msanii huyu na kugundua kwamba aliyemdunda kumbe alikuwa mpenzi wake anaeishi maeneo ya usagara Jijini Tanga, Na sio mara moja alishawahi kumpiga tena mara ya kwanza wakaachana baadae kama mnavyojua mapenzi, Si wakarudiana tena?.. Ila hii ya sasahivi hakuwa na nia njema maana alimpigia kelele za mwizi hatimaye msanii huyu kunusurika kufa aliokolewa na muuza bucha baada ya kukimbilia buchani..! Ama kweli wanawake wa sikuhizi noma...! Yani weka jiwe niweke kigingi.

Sina mengi ya kuongea msikilize msanii mwenyewe alivyofunguka .

AUDIO HII HAPA CHINI



Credit:Masainyotambofu.

HAYA KWELI MAAJABU YA DUNIA!! NYOKA WAMFANYIA MTU MASAJI KWA GHARAMA YA DOLA 47

$
0
0

UNAPENDA kufanyiwa masaji na nyoka? Unaweza kukaza roho na usiogope kung’atwa? Kama ndio basi nenda nchini Indonesia utaipata kwa raha zako.


Masaji hiyo inapatikana Bali Heritage Reflexology and Spa huko Jakarta, Indonesia ambako wanaweza kukuondolea uchovu wako wa siku nzima kwa massage ya nguvu inayofanywa na nyoka mkubwa.



Masaji hiyo inafanyika kwa nyoka huyo kuwekwa juu ya mwili wa mteja na mengine huachiwa yeye nyoka afanya yake. Ili kupata huduma hii mteja hutakiwa kulipa dola 47 ambazo ni zaidi ya shilingi 76,000 za Tanzania.

MTOTO AVUNJWA KIDOLE NA MWALIMU WAKE BAADA YA KUINGIA DARASANI NA NYWELE NDEFU.

$
0
0

Wiki ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto ikiwa imeanza kuadhimishwa duniani Novemba 25 mwaka huu bado vitendo hivyo vimezidi kushamiri Mkoani Mbeya ambapo mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Aiport Kata ya Iyela jijini Jacline Staniely [9] ameumizwa mkono wake wa kushoto.


Jacline akiongea kwa ridhaa ya mama yake amesema alipigwa kwa kutumia ubao na mwalimu wa shule hiyo Novemba 19 mwaka huu na mwalimu Kanyika kwa kosa la kuwa na nywele ndefu.
 
Mwanafunzi huyo amedai kuwa siku ya tukio alipigwa vibaya na kumsababishia maumivu makali ambapo siku hiyo mama yake alikuwa safarini Nairobi Kenya hivyo hakupata matibabu ambapo alilazimika kumwambia mwalimu jirani[Bibi]ambaye alimpeleka hospitali kutibiwa.
 
Picha  ya  X ray ikionesha  kidole kilichovunjika :
 
Hata hivyo Jackline amesema kuwa kutokana na maumivu makali alilazimika kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne bila kupata matibabu ya kutosha.

Baada ya kurejea kutoka safari mama yake mzazi aitwae Rehema Adamson Ndeje[28] mkazi wa Block T jijini Mbeya amesema baada ya maumivu ya mwanae usiku ilimlazimu kwenda shuleni ili kujua kulikoni,ndipo alipoonana na mwalimu Kanyika baada ya kukutanishwa na Mwalimu mkuu.

Mama Jackine amesema hicho ni kipigo cha tatu kukubwa kwa mwanae kupigwa na mwalimu huyo ambapo alionesha makovu yaliyodaiwa yalitokana na vipigo vya mwalimu huyo miguuni akidai majeraha hayo yalidumu kwa miezi mitatu.

Hata hivyo Rehema aliamua kwenda Polisi Mwanjelwa kutoa taarifa za tukio na kila alipoitwa mwalimu huyo hakutokea ndipo jalada likapelekwa kituo kikuu cha kati ambapo mwalimu alikamatwa na mhanga kupewa PF 3 kwa ajili ya matibabu ambapo alipigwa picha na kuonekana moja ya kidole cha kati cha kushoto kimeathirika kutokana na kupigwa kwa kutumia ubao.
PF3
Mzazi huyo amesema hana nia mbaya na mwalimu Kanyika lakini kitendo cha kumwadhibu mwanae mara kwa mara ndicho kimemtia shaka hata kuamua kutoa taarifa Polisi ili sheria ichukue mkondo wake.
 
Mwandishi wa habari hii alipofika shuleni ili kujua mustakabali wa suala hili, mwalimu alimtoa nje  akidai yeye ana majukumu mengine .

Mwandishi alimtafuta mmoja wa wanaharakati wa kijinsia ambaye alikiri kupokea lalamiko hilo ingawa alijibu kwa mkato kuwa mtoto huyo kaumia kidogo tu na ni usanii mtoto huyo kufungwa POP na kwamba bado PF3 haijajazwa kitu hivyo hawezi kuzungumzia lolote.

Kumekuwa na malamiko mengi katika Dawati hilo kutokana na matukio kutochunguzwa kwa wakati , hali inayotoa mwanya kwa vitendo hivyo kuibuka mara kwa mara na wahalifu kutoroka mkono wa sheria .
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya ameahidi kulifuatilia suala hilo na ikibainika mtuhumiwea atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Na Ezekiel Kamanga 
Mbeya yetu

VIDEO:TUNDU LISSU AKIMSOMEA MAKOSA 11 ZITTO KABWE YA KUPANGA KUKIPINDUA CHAMA CHA CHADEMA.

HII NDIO HABARI KUHUSU GARI JIPYA KABISA LINALOJIENDESHA LENYEWE.

$
0
0
YMo_system_rear_0826

Taarifa ikufikie kutoka Samukawa, Kanagawa Japan ambako stori kwenye headlines ni kampuni ya Nissan kupata furaha kubwa baada ya kufanikiwa kwa jaribio la gari 

walilolitengeneza ambalo linajiendesha lenyewe.
Unaambiwa limetembea umbali wa kilometa 2.3 likijaribiwa kwenye mikikimikiki ya aina mbalimbali barabarani kama vile kuovertake, kufata alama za barabarani, taa za kuongozea magari na hata sehemu za watu kuvuka barabara.YMo_system_rear_0826Nissan wamesema wanalengo la kuanza kuliuza hili gari miaka saba kutoka sasa, hiyo itakua mwaka 2020 ambapo gari hili lina kamera maalum pamoja na sensors zinazofanikisha kulipa taarifa ya tukio husika kwa wakati huo ndio maana linaweza kufanya kama inavyotakiwa mfano kushika breki, kukanyaga mafuta na vitu vingine.
Kingine cha kushangaza, kwa mfano kwenye miji mikubwa ambayo parking ni tatizo unaweza kuliacha likajiendesha lenyewe kwenda kutafuta parking wakati wewe unawahi mahali alafu ukimaliza shughuli zako unalikuta linakusubiri likiwa limepaki vizuri kabisa.nissan 4Baada ya kutazama hizo picha hapo juu, unaweza kutazama hii video kujiridhisha kikamilifu aisee japo hii video sio ya majaribio yaliyofanyika saa kadhaa zilizopita..

Download Na Sikiliza Wimbo Mpya Wa Belle 9 - Wanitaka.

KUTANA NA MAREHEMU KANUMBA NA SHAROMILIONEA KATIKA KIPANDE HIKI CHA MUVI.INAUMA SANA ILA TUKUMBUKE KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.

CHIDI BENZI KAVURUGWA,ONA ALICHOPOST.

$
0
0

Hakuna tena kitu kizuri kwa Chidi Benz siku hizi. Kwa muda mrefu rapper huyo ambaye hivi karibuni ametokea kukubalika sana nchini Kenya (thanks kwa mashavu anayopewa na Nonini) ameonekana kutoa yake ya rohoni yanayomuumiza kupitia Twitter.

Yeye na Wakazi kuna tatizo?
Picha lilianza jana, baada ya Wakazi kutweet: Na ningependa kusema pia AY, Dimpoz, Ally Kiba, FidQ, Shaa, Cpwaa, Black Rhino, Remi Ongala, Profesa Jay & Lady Jaydee ni other Local heros!
Baada ya kuona ujumbe huo wa Wakazi, Chidi alimuuliza kishari ‘nini?’
Wakazi alichuna. Chidi akaamua kuandika: Hujui kuongea huwezi muoga..unaweza kuandika hapa twitter. Nyie ndio mkianza kushindwa mnasifia maadui.#umal** tuu.”
Ujumbe huo ulivuta hisia za watu wengi akiwemo Madee aliyeuliza: Rasheeed nani tena kazingua?  Chidi alijibu: Mazafanta wanahisi wanajua kuliko wewe wakati mwenyewe saa zingine unaona hujijui..2
Hata hivyo hatuwezi kuthibitisha kama maneno hayo yalikuwa yakimlenga Wakazi ama mtu mwingine kwakuwa kabla ya hapo tayari alikuwa ameanza kuandika tweets za hasira.
“Game ilipo now na propaganda zake inaua vitu vingi tu.sisi tunaonekana tunalalamika ujinga but hatuna maisha mabaya. Viongozi wa nchi sio lazima mdil na bongo freva..haiongezi wewe kufatwa but unatuongezea uadui usio na lazima. Mi natangazwa kwa ubaya tuuuuu.ila nina marafiki bado na wengi wanaongezeka hata hapa.#nakaza roho,” aliandila Chidi.
Kunani?

Mshindi wa EBSS kutotumia zawadi kwa mapenzi yake, atatakiwa kuwekeza kwenye muziki pia.

$
0
0
Mwanzilishi wa show hiyo ambaye pia ni jaji mkuu, Rita Paulsen aka Madam Rita, amesema wameamua kufanya hivyo kwakuwa washindi wamekuwa wakizitumia fedha wanazopata kwa mambo mengine na kusahau muziki.
Ameongeza kuwa wameamua kufanya hivyo kuondoa lawama za watu kuwa washindi hupotea mapema.
“Tumegundua kwamba wasanii hawawezi kutumia hizo hela kujijenga. Wanaweza kutumia kwa vitu vingi ambavyo ni mahitaji pia sijui nyumba, gari,” amewaambia waandishi wa habari leo.
“Management company inaleta proposal, tunatengeneza video kadhaa, tunatengeneza promotion ya wimbo wako. Kutakuwa na mwanasheria na yeye mwenyewe anaauthorise ile hela inaenda kufanya hivyo vitu.”
Fainali ya shindano hilo itafanyika November 30, jijini Dar es Salaam.

Shetta amshirikisha Diamond kwenye wimbo wake wa kufungia mwaka 'Mama Qaylla'

$
0
0
Shettta amesema kuwa tayari ameshafanya ngoma nyingine na Diamond Platinumz inayoitwa Mama Qayllah na umetayarishwa na Shedy Clever wa Burn Records.
“Kwanza kabla ya yote ningependa kutoa shukrani za dhati kwa mashabiki wangu kwa kuipokea vizuri video ya wimbo wangu 'Sina Imani',kwa sasa nipo katika maandalizi ya wimbo wangu mwingine mpya kabisa humo ndani nipo mimi pamoja na Diamond,wimbo unaitwa Mama Qayllah. Bado upo katika hatua za mwisho za kufanyiwa mixing na Sheddy Clever  wa Burn Records.” Sheddy Clever ameeleza.  
Shetta ama Baba Qayllah kama anavyopendwa kuitwa amesema huo utakuwa wimbo wake wa mwisho wa kufungia mwaka 2013.

Bamboo akiponda kiwanda cha muziki Kenya, asema ni 'fake'

$
0
0
Hitmaker huyo wa Compe, aliyeokoka September mwaka huu amesema wokovu wake ni kitu cha ukweli zaidi alichokifanya katika maisha yake.
“Wokovu wangu ni halisi. Mpaka sasa umekuwa poa. Nachukua tu muda kukua. Hata hivyo simiss nyimbo za kidunia hata kidogo.
Ni kupitia rehema za Mungu nimeweza hata kuwa mbali na marafiki zangu kwenye muziki wa dunia kama Abbas na mdogo wangu  Kimya.
Badala yake nimekuwa na mawasiliano na wasanii wa gospel kama Mr Googz, Mr T na Pastor Eric Mwangi. Ukweli ni kwaba hata rafiki yangu wa karibu, Abbas, aliacha kuongea nami siku niliyookoka, sijui kwanini,” Bamboo aliliambia gazeti la The Star.
Bamboo amesema hatoweza kushirikiana na wasanii wanaofanya muziki wa kawaida. Tangu aokoke, Bamboo aliachia wimbo uitwao Solja, na anatarajia kuachia wimbo mwingine uitwao Decisions.

Forbes yatoa orodha ya waigizaji wa TV wanaliopwa zaidi duniani.

$
0
0

Mtandao wa Forbes umetoa orodha ya waigizaji wa TV walioingiza fedha nyingi zaidi mwaka 2013. Nafasi ya kwanza imekamatwa na Sofia Vergara ambaye katika kipindi cha June mwaka 2012 hadi June 2013 aliingia dola milioni 30.

Vergara, anayeigiza kwenye tamthilia ya Modern Family, hulipwa sawa na waigiza wa kiume kwenue show hiyo kwa takriban $175,000 kwa kila episode.
Tazama orodha kamili:

2. Ashton Kuchter - $24 million (Two and a Half Men)
3. Jon Cryer - $21 million (Two and a Half Men)
4. Ray Romano - $16 million (Everybody Loves Raymond)
5. Mark Harmon - $15 million (NCIS)
6. Neil Patrick Harris - $15 million (How I Met Your Mother)
7. Patrick Dempsey - $13 million (Grey’s Anatomy)
8. Tim Allen - $11 million (Last Man Standing)
9. Kaley Cuoco - $11 million (The Big Bang Theory)
10. Mariska Hargitay - $11 million (Law & Order: Special Victim's Unit)

Mikoa 11 kuingizwa kwenye mfumo wa dijitali ndani ya miezi3-8 ijayo, yasema TCRA.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania Profesa, John Nkoma alikuwa akiongea kwenye maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo na kuelezea ratiba hiyo.
Mpaka sasa makampuni ya StarTimes Media Limited, Basic Transmission na Agape Associates Limited ndiyo yanayohusika na utoaji wa huduma ya matangazo hayo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Makame Mbarawa, alisema ndani ya miezi mitatu hadi minane mikoa mingine itahamia dijitali pia.
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live