Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live

KIJANA WA MIAKA 22 ASHIKILIWA NA POLISI KWA KESI YA MAUWAJI BAADA YA KUMUUA BABA YAKE MZAZI.

$
0
0

22-year-old Olalekan Adetoyinbo, has been arrested by the Police and is in the homicide section of the

State Criminal Investigation Department of the Osun State Police Command for allegedly killing his own father, 56-year-old Mr Ayodele Adetoyinbo by hitting him with a concrete block.

Olalekan, a 200-level student of Osun State College of Education, was on Wednesday, November 13, arrested by a team of police detectives from ‘B’ Division, Ijamo, Ilesa in Osun State and he confessed to the police that he committed the offence, saying that on his return from school on the fateful day, his father, Mr Ayodele Adetoyinbo (56), had accused him of stealing 10 empty kegs.

Olalekan said his explanation to his father that he knew nothing about the missing kegs fell on deaf ears, a situation which led to a heated argument between father and son.

He admitted hitting his father on the head with cement bricks, which led to the injury sustained by the older man.

In an interview with Crime Reports, the Economics/Political Science student from Ilesa town said: “We live at Irojo, Ilesa. I am the first of seven children of my parents. I went to school on Sunday, November 10, to read in preparation for my exams. On Wednesday, November 13, my father called me to come and help him measure the chemical he would use in soap making.

“As I got home, he told me he could not find 10 of the kegs we were using to buy palm kernel oil for soap making. I told him I didn’t know anything about it. After I finished, I was leaving for school when I remembered that I didn’t take the receipt I would use as a pass for my exams in the school. I went back home for it but my father asked of the key to the house from me and I told him it was in school. He did not believe me and wanted to search my pocket. At that time, my mother was not around; only my siblings were around.

“He said he would not allow me to go if I didn’t give him the key. We started struggling and he used hoe stick to hit me. We dragged ourselves outside and we fell down. I took a concrete block to hit him and he fainted. I tried to take him to hospital but people did not allow me. He gave up the ghost and residents of the community started beating me before I was rescued.”

Crime Reports gathered that the deceased used a stick to hit his son when he refused to give him the key of the house he had with him. The man was said to have insisted on collecting the key so that his son would not have access to the house whenever he was not around, since he denied knowing anything about the missing kegs.

Olalekan reportedly took the stick from his father and hit the man. As the man fell, he allegedly dragged a concrete block from where it was placed and hit his father with it.

The man was said to have been covered with blood immediately as he started bleeding from the nose and head. He reportedly died shortly after. A police source told Crime Reports that detectives took the injured man to the hospital where he was confirmed dead by a medical doctor.

When contacted, the state police spokesperson, Folasade Odoro, a Superintendent of Police, confirmed the story, disclosing that the corpse had been deposited at Wesley Guild Hospital, Ilesa for autopsy.

She added that the Commissioner of Police, CP Dorothy Gimba, had ordered the State Criminal Investigation Department, Osogbo, to take over the case for further investigation, adding that the suspect would be charged to court at the completion of investigations.

MSHINDI WA BIG BROTHER '' DILLISH MATHEWS'' AFUNGA NDOA LEO HUKO NAMIBIA.PICHA ZAIDI ZIKO HAPA.

$
0
0

Big Brother Africa Winner, Beautiful Dillish Mathews got married to her beau, today in Namibia......but

it looks like Melvin Oduah was the only big brother contestant in attendance.


















HII NI AIBU KWA KWELI ONA JOH MAKINI ALICHOMFANYA G-NAKO.

$
0
0

Hichi ndicho alichomfaya Gnako Joh Makini baada ya kutaka kujua nani Raia wanamkubali zaidi.

JOH MAKINI
  69 (81%)
 
GNAKO
  16 (18%)
 

Votes so far: 85
Poll closed 
Hapo juu inaonyesha wazi kabisa Joh Makini yuko juu sana,G-NAKO aendelee kusubiri tu.

Dakika 6 za kauli ya Zitto Kabwe ya msimamo baada ya kuvuliwa vyeo Chadema.

$
0
0
Zitto K Ayo TVZitto Kabwe alizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa habari kuhusu ishu yake ya kuvuliwa
vyeo Chadema baada ya kamati kukaa, bonyeza play hapo chini utazame alichosema ndani ya dakika 6.
Credit:Millardayo.


HUYU DADA AMEKIRI KUWA AKIPIGA PICHA ZA UTUPU ZINAMPA COMENTS NYINGI FACE BOOK.

$
0
0
http://www.theclicktz.com/
Akidai kwamba inauma kama natupia picha facebook halafu sipati hata like wala comment ila nikitupia picha nimeweka hata ziwa langu tu moja
nje ndani ya dakika moja tu nitakuwa na comments hata hamsini ndio watu wanataka hivyo sasa nitafanye...??

Credit:the clickTZ

ZINGATIA SANA MAMBO HAYA BAADA YA KUCHUMBIWA.

$
0
0
Kuna mambo kadhaa ambayo msichana anatakiwa kuwa makini nayo katika kuhakikisha uchumba wake unadumu na kufikia hatua ya kuolewa na kwenda kuanza maisha mapya.
 
Yapo mengi lakini nitagusia matano ambayo kwa utafiti wangu ndiyo


yamekuwa yakiwafanya wengi wakimbiwe na wachumba wao na kuachwa wakilia.

  Mazoea na wanaume

Wapo ambao wamejikuta wakiachwa solemba kufuatia tabia zao za kuwa na mazoea ya kijinga na wanaume.
Yawezekana kabla ya kuchumbiwa marafiki zako wakubwa walikuwa wanaume (Wapo wanawake wa aina hiyo). Unachotakiwa kufahamu ni kwamba hakuna mwanaume anayefurahia ukaribu wa mchumba wake kwa wanaume wengine.
Hata kama hakuna uhusiano wa kimapenzi lakini epuka sana kujichekelesha kwao, kuongozana nao, kukaa nao au hata kuwasiliana nao. Ukifanya hivyo utakuwa unamkwaza mchumba wako na inaweza kuwa moja ya sababu za kukuchenga.

Marafiki micharuko

Ukishachumbiwa, kuna marafiki zako ambao ‘automatikale’ unatakiwa kuachana nao. Nazungumzia wale micharuko ambao hawawezi kukushauri vizuri juu ya maisha yako.
Hata wale ambao wamekuwa wakikushawishi kila wikiendi muende mkajirushe, baada ya kuchumbiwa unatakiwa kujiweka mbali nao ili kumpa amani mchumba wako.

Tabia za kisichana 

Ukishachumbiwa wewe si msichana tena, utakuwa ni mama mtarajiwa wa familia yako. Tabia za kisichana kama vile kuvaa mavazi yasiyo ya heshima, kukaa vijiweni kuongea mambo ya umbeya na nyinginezo kama hizo hutakiwi kuendelea kuwa nazo.

Kujifanyisha

Alichokupendea huyo mchumba wako anakijua mwenyewe, kwa maana hiyo unatakiwa kuendelea kubaki wewe kama wewe. Usijifanyishe kwa namna yoyote kama ambavyo baadhi ya wasichana wamekuwa wakifanya.

Eti umeshaolewa

Kuolewa ni mpaka pale mtakapoingia kanisani, msikitini nk na kufungishwa ndoa. Kama bado hamjafika huko, wewe bado ni mchumba tu na hata kwenye ndoa unaweza usifike.
Kwa maana hiyo hutakiwi kuhamia kwa mwanaume kama ambavyo baadhi wamekuwa wakifanya. Unachotakiwa kufahamu ni kwamba kitendo cha wewe kuchumbiwa kisha kuamua kubeba virago vyako na kwenda kuishi na mwanaume ni kuwakosea wazazi. 


Msomaji wangu, yapo mengi ya kuepuka mara tu unapochumbiwa lakini haya machache yanatosha kwa leo. Jiangalie tabia zako, zile ambazo unajua wanaume wengi haziwafurahishi, jiepushe nazo ili kumjengea mchumba wako mazingira ya kukamilisha taratibu za ndoa yenu.
 
credits: bongonews 

MAVAZI YA KATA K SIO KWA WANAUME TU,SASA MPAKA WANAWAKE.HII NI NOUMAH SANA!!

LILI KIM APANDA JUKWAANI NA VAZI LINALOONYESHA MAUNGO YAKE YOTE NA KUONEKANA KAMA YUKO UCHI.

$
0
0

Lil Kim mwanamuziki wa kike mwenye umri wa miaka 39 Aliwapagawisha wakaazi wa London Siku Ya Ijumaa Tarehe O2/11/2013  aliwaacha midomo wazi mashabiki kwa vazi alilolitinga yani mambo yote hadharani haina tofauti na kupanda Jukwani Uchi..!




HUYU NDIO MTANZANIA ALIYEVAMIWA NA MAJAMBAZI HUKO KENYA NA KUUMIZWA VIBAYA SANA.

$
0
0

HABARI tulizopata kupitia mtandao wa Jamii Forum zinasema kuwa pichani ni mtanzania alyievamiwa na kuumizwa vibaya huko Nairobi nchini Kenya.


Police Nairobi ndo walimuokota na akajitambulisha kwao kama Dr. Juma Maliki. Wito unatolewa kwa yeyote anemfahamu awasiliane na ndugu zake maana inasemekana hali yake ni mabaya na kwa sasa hawezi kuongea. Mpaka sasa hakuna mtu wa karibu aliyejitokeza na amelazwa Kenyatta National Hospital na hakuna taarifa zaidi ya hizi.

UPDATE:
Inasemekana Dr Juma Maliki ni mkurugenzi Wizara ya Afya Zanzibar na ni daktari bingwa katika hopital ya Mnazi Mmoja alikuwa Nairobi kikazi na wamepoteza mawasiliano nae tangu Ijumaa.

LADYA JAY DEE AMPA WAKATI MGUMU MH. JANUARY MAKAMBA.

$
0
0
Lady Jaydee
Lady Jaydee kweli ni Anaconda na sio mtu wa kuchezea kwani ukiingia kichwa kichwa kwenye kumi na nane zake anakumeza na kukupaka live
kama huna hoja ya msingi. Hayo yamempata Mbunge wa Bumbuli January Makamba. Angalia alichoandika Makamba hapo chini na jibu la Lady Jaydee ambaye ni mwanamuziki mwenye jina kubwa Afrika mashariki.




UMEWAI KUONA HII VIDEO YA DIAMOND PLATNUMZ AKIWA NA KING MAJUTO,KINGWENDU NA BAMBO.WIMBO UNAITWA UKIMWONA.HATARI TUPU.

Zaidi ya watoto 60 wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni - Dar es Salaam.

$
0
0

Zaidi ya watoto 60 wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni ,Dar es Salaam, ambalo ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba.


Utekaji huo unadaiwa kufanywa na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa.

Mtoto Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo, ndio waliofichua ukatili huo mwishoni mwa wiki.

Watoto hao walitekwa na Wazungu w awiliasubuhiyaSeptemba2mwaka huu, wak ati wakiendas huleni n akufan ikiwa kutoroka katikaj engohiloSeptemba 23 mwaka huu.

Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna watoto wengi wa kike na kiume.

Walisem a w atoto hao wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia wazazi wao ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa.

"Jumba hili limejengwa ndani ya handaki, tulikuwa tukifanyishwa kazi ngumu na nzito, usiku tunajaza maji katika mapipa mengi na kubebeshwa ndoo kupanda na kushuka kilima.

"Tunapigwa fimbo, wasichana wanafungiwa kwenye vyumba, wanabakwa na kulawitiwa kwa zamu na Wazungu, tunachomwa moto (alionesha mguu wake uliochomwa) na kupigwa shoti ya umeme tunapowaulizia wazazi wetu," alisema Emmanuel kwa uchungu akitokwa na machozi.

Aliongeza kuwa, asubuhi ya Novemba 23 mwaka huu, katika jengo hilo kulitokea kutokuelewana kati ya Wazungu na Waswahili ambapo mswahili mmoja aliwatisha wazungu kwa kuwaambia polisi wanakuja hivyo walikimbia na kuacha mlango wazi.

"Hali hiyo iliniwezesha mimi, mdogo wangu na watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu kufanikiwa kutoroka, nilimshika mkono mdogo wangu ambaye alionekana kuchoka nikamvuta.

"Watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu nao wakatoka, wengi hawakuweza kutoka kutokana na kukosa nguvu, wanaumwa, wana vidonda vikubwa mwilini kutokana na kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme, wasichana hawakuweza kabisa kutoka kwa kuwa wamefungiwa ndani ya vyumba," alisema Emmanuel

Aliongeza kuwa , alijikokota taratibu na mdogo wake mbali ya maumivu makali waliyonayo akatokea Mswahili mmoja ambaye alikuwa na gari lenye vioo vyeusi akawaambia wapande ili awatoroshe.

"Tulipanda gari hilo akatushusha darajani mpakani mwa Manispaa ya Kinondoni na Wilaya ya Kibaha, jirani na mzani eneo ambalo sisi hatukuwa tukilifahamu...dereva huyo alituambia gari limeishiwa mafuta hivyo alitutaka tumsubiri aende kuyanunua.

"Tulitembea kidogo tukiwa hatujui tunakokwenda... tulikaa kando ya barabara kutokana na uchovu pamoja na njaa kali kwani katika jengo hilo mbali na kazi nzito tulizokuwa tukizifanya na mateso mengi, mlo ulikuwa mmoja tu kwa siku.

"Tulikula saa 10 jioni, wali na maharage...tukiwa kando ya barabara, nilisikia sauti ya baba yangu wa kufikia, dereva wa magari makubwa yanayobeba kokoto ikiniita.

"Nilidhani naota kumbe ilikuwa kweli, alikuja akatukumbatia akalia kwa uchungu kwa namna tulivyokuwa tumechoka na afya kuzorota, akatupeleka polisi ambapo tulipatiwa maji tukaoga na kupewa chakula kizuri na kitamu, tukala na kupata nguvu za kuzungumza vizuri," alisema Emmanuel.

Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa ndani ya jumba hilo la mateso.

Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.

Mama mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za mama lishe, njia panda y a Ba r a k u d a , Ta b a t a Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio.

"Nimepoteza fedha nyingi kwa kuwatafuta na kutapeliwa mara kadhaa katika kuhangaika," alisema Godianus huku akitokwa na machozi ya furaha katika Kituo kidogo cha Polisi Maili Moja.

Alisema zaidi ya watoto saba walipotea katika mtaa wao, wawili wakapatikana baada ya wiki mbili, wengine wakiwemo wanaye wakawa hawajapatikana na kuomba Serikali ilichukulie kwa uzito suala hilo ili kubaini kundi linalowateka watoto na kuwatesa.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuanza kulifanyia kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.

Alisema makachero wa polisi wamewahoji watoto hao ili kupata maelekezo ya kufika katika andaki hilo na kuwataka watu wote wenye taarifa za eneo hilo watoe ushirikiano.

Credit-Gazeti la Majira.

KAULI 10 ZA ADEN RAGE BAADA YA KUTIMULIWA SIMBA ZIKO HAPA.SINA MBAVU KWA KWELI.HATARI TUPU.

$
0
0
Zifuatazo ni kauli za Ismail Aden Rage ambazo nimemnukuu akiongea na Waandishi kutokana na
stori zilizochukua headlines kwa siku kadhaa kuhusu Kamati kumsimamisha kama Mwenyekiti wa Simba.
1. ‘Kwanza napenda kuipongeza kamati ya utendaji ya TFF kwa kuafiki mimi Ismail Aden Rage ndio Mwenyekiti halali wa Club hii ya Simba na nimepata barua yao jana ileile, katika katiba ya Simba kuna kitu wengi hawajui maana ya Kamati ya utendaji wanadhani ni wale watu saba… hapana!!! kamati ya Utendaji ni Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti… hamna kaimu hapo, kuna Wajumbe 7 waliochaguliwa katika mkutano halali… , Wajumbe saba wa kuchaguliwa mmoja wapo akiwa ni Mwanamke na wengine wawili wa kuteuliwa na Mwenyekiti, leo nitateua mwingine mmoja.. nimetoa mmoja’
2. ‘Kwa bahati mbaya Club ya Simba haina Makamu Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti alishajiuzulu ila ina Kaimu Mwenyekiti tu ila huku kwenye katiba hatajwi, kwenye katiba ya Simba Makamu Mwenyekiti ana kazi mbili, moja kwa kuelekezwa na Mwenyekiti na pili Makamu Mwenyekiti anafanya kazi wakati Mwenyekiti hayupo’ – Aden Rage
3. ‘Joseph Itangire ni Kaimu Mwenyekiti tu niliemteua lakini hajapata uhalali wa kikatiba kwa hiyo katiba hii inaendelea kusema, mwenye mamlaka ya kuitisha kamati ya Utendaji mara nne kwa mwaka ni Mwenyekiti, nimekua muungwana tumefanya mara 12 mwaka huu.. kama Mwenyekiti hayupo, katiba inasema anakaimu hana mamlaka ya kuitisha kikao chochote kwa mujibu wa katiba kwa hiyo kikao kile kilichofanyika hakina tofauti na kikao cha harusi’
4. ‘Maamuzi yangu kama Mwenyekiti wa Simba sasa, kwa kuwa mkutano ule ulikua ni batili… jana niliandika barua kwa TFF kwamba viongozi hawa wamevunja katiba za TFF, Simba, CAF na FIFA… ukitaka kulalamika ni lazima uwe na ushahidi wa aina mbili unaokubalika ambao ni document na video casette iliyo na sura za watu na maneno yao waliyosema, wana document ambayo kwenye barua ya Malinzi amekiri anayo na imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba Joseph Itangire’
5. ‘Nimesikitika sana na maagizo ya TFF ya kunitaka niitishe mkutano na Wanachama wa Simba ndani ya siku 14, sijui wameitoa wapi kwenye katiba ya TFF na Simba, wamekwenda mbali na kuninyang’anya madaraka… wamenipa alafu wameninyang’anya alafu wamenipa na Ajenda ya mkutano, sasa wamenirudishia madaraka ya nini? mimi kama Mwenyekiti wa Simba… siitishi mkutano, nalindwa na katiba kwa hilo’
6. ‘Unaponipa amri unaninyang’anya madaraka yangu, katiba inasema kama naona itafaa nitaitisha… tuheshimu katiba, nilitegemea taarifa ya kwanza ya TFF mpya ingelaani mapinduzi ya kipuuzi yanayotokea’
7. Heshima yangu mimi ni Mbunge taifa linaelewa hivyo, nimekuta ofisi hii hakuna umeme miaka 18 pamoja na pazia za magunia, nimekuta uhuni mtupu.. wachezaji wameuzwa, Henry Joseph, Matole na wengine uliza wanachama wa Simba ilipata shilingi ngapi? leo imani inawatoka kusikia nimeuza Wachezaji wawili tu Congo DRC milioni 320 na nikaweka wazi hadharani sio kuwaambia Mke wangu na watoto wangu..
8. Leo nimetumiwa msg kutishia kuuwawa na tayari nimesharipoti Polisi, leo hii msg nimepata mtu kaniambia ‘Nisipotoka Simba ataniua’ alivyokua mpumbavu hajui hizi simu zinasajiliwa, nimecheki jina lake mpaka mtaa anaokaa pengine sasa yuko Lupango… why??? mpira ni burudani!! kuna mtu alikua Simba sasa yuko TFF anataka kuleta vurumai ndani ya TFF na Simba, kwa nini? kwa nini ununue watu? waandishi wa habari hebu tuache kuchochea, wewe Mwandishi ni nani ununuliwe? kuna Mwanamke Mwaandishi mmoja kalipwa milioni 2 ili anichafue, sijali.. ‘
9 Nimefanya Demokrasia sana na ndio inanitokea puani, nimeteua kamati… ziko kamati nyingi sana lakini sijaona Mwandishi hata mmoja anakwenda kuuliza kamati ya ufundi, Usajili ila kila mmoja ananishambulia mimi, leo sitaki maswali ya Waandishi wa habari, sasa mna hiari… kuandika au kuacha wala hamnipi tabu nyie, kuchafuliwa nimezoea’
10. Ukitaka kuwa kiongozi teka Ikulu kwanza, hapa ndio ikulu. 

RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI AMEMFOLLOW VENESSA MDEE KWENYE TWITTER.

$
0
0
Hii itakuwa ni kwa mara kwanza kwa mwimbaji wa Tanzania na pengine Afrika kuwa followed na Rais
Barack Obama wa Marekani kwenye twitter ambae ana zaidi ya followers milioni 40 lakini yeye anafollow watu laki sita.
Vanessa Mdee ameingia kwenye list ya watu laki sita ambao Rais Barrack Obama ana wa-follow sasa hivi ambapo baada ya Rais huyu kufollow, kwa furaha Vanessa alishare kwenye instagram screenshot ya ukurasa wake wa twitter ukionyesha Barack Obama ameanza kum-follow.
Kama ilivyo twitter, hii inamaanisha ana Vanessa ana uwezo wa kumuandikia msg binafsi kwenye inbox Rais Obama.

VIDEO MPYA YA SNURA NIMEVURUGWA IKO HAPA!!


DR WA MAREHEMU MICHAEL JACKSON AELEZA SIRI NZITO KUHUSU MAREHEMU.

$
0
0
Kwenye mahojiano yake ya kwanza mara baada ya kuachiwa toka gerezani kwa kuhusishwa na kifo cha nguli wa muziki wa pop duniani Michael Jackson,
Dokta Conrad Murray alielezea kwenye mahojiano aliyofanya na The Mail kwamba, Michael hakuwa baba wa hata mtoto wake mmoja, aliathiriwa na madawa kiasi cha kufikia hatua ya kuhitajika kuwa anavaa condom sababu mkojo ulikuwa unatoka wenyewe kwenye uume wake.

“Unataka kufahamu ni kwa kiasi gani mimi na Michael kwa vile tulikuwa karibu? Nilikuwa nikishukilia uume wake kila usiku. Nilikuwa namvalisha condom sababu mkojo wake ulikuwa ukitoka wenyewe. Michael alikuwa hajua namna ya kuvaa condom, hivyo ilinibidi niwe namvallisha. Kilikuwa ni kitu cha kipekee sana ila aliniamini mimi. Sikumuuwa Michael Jackson, aliathiriwa na madawa, Michael Jackson kwa bahati mbaya alimuuwa Michael Jackson, naamini aliamka na kuamua kufanya aliyozoea kufanya, akajidunga sindano haraka ambayo ilisababisha kumpeleka kwenye hali iliyomfika.’’ 

Alikuwa kwenye majanga mwishoni mwa maisha yake, akiwa na msongo wa kimawazo na kupaniki … Mwishoni, Michael alikuwa mtu aliyekata tamaa. Nilijaribu kumlinda ila mwisho wa siku niliangushwa naye.

Jackson alikuwa ameingia kwenye matatizo ya kuathirika kiakili na kimwili kutokana na ziara yake ya London.’’ Alisema Dokta Conrad Murray. 

ZITTO AJIWEKA NJIA PANDA.

$
0
0
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amejiweka katika mazingira magumu zaidi
kisiasa ndani ya chama hicho, kutokana na shaka kubwa iliyougubika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam juzi.

Zitto pamoja na viongozi wengine wawili wa Chadema; Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu ya Chadema baada ya kubainika kupanga mbinu za uasi, kupitia waraka ambao ulikuwa ukieleza mkakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani.

Leo, uongozi wa Chadema umeitisha mkutano wa waandishi wa habari ambao pamoja na mambo mengine, utajibu baadhi ya hoja za utetezi ambazo zilitolewa na Zitto pamoja na Dk Kitila. Katika mkutano wa juzi, Zitto na Dk Kitila ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, walizungumzia kuvuliwa kwao madaraka, lakini maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo yanazua shaka kutokana kuwahusisha watu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

Miongoni mwao, wamo waliowahi kuwa wanachama wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Habib Mchange na Mtela Mwampamba ambao walitimuliwa kwa makosa yanayofanana na yale yalizosababisha Zitto na wenzake kuvuliwa nyadhifa zao.

Mchange na Mwampamba pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza, walivuliwa uanachama wa Baraza hilo Januari 5, mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia mitandao ya kijamii kukihujumu Chadema na kuwatukana viongozi wake wakuu. Baadaye walihamia CCM wanakoendeleza harakati zao za kisiasa.

Jana, Machange alipotafutwa, alisema: “Mimi sikuwahi kuondoka Chadema, nilifukuzwa kihuni kama walivyowafanyia Zitto na Kitila. Nimepeleka malalamiko yangu tangu Januari hadi leo sijajibiwa, hivyo siwezi kusema nimeondoka.

Nataka nimuunge mkono mwathirika mwenzangu kama ilivyokuwa mimi lakini nitabakia kuwa mwanachama mwaminifu.

“Mimi ni mwanaChadema na sikuwahi kujiunga na CCM au chama chochote, walioondoka ni Mwampamba na Shonza.” Mwampamba alisema: “Nilijitokeza pale kuonyesha mshikamano kwa sababu mimi pia ni mwathirika. Kwa hiyo nilitaka ulimwengu ufahamu kuwa mimi ni kati ya wanaopinga siasa za aina hii... Chadema ni chama kinachojiandaa kuchukua dola, sasa kama kila mwenye mawazo tofauti anaonekana mhaini itakuwaje siku wakichukua dola? Ubaguzi huu haujalishi uko chama gani, hata kama niko CCM, hilo halinizuii kuungana na mtu aliyepatwa na tatizo kama langu.”

Kuwepo kwao katika mkutano wa Zitto kunaweza kutumiwa na uongozi wa Chadema kuwa uthibitisho wa kiongozi huyo kushiriki katika uasi na kunaweza kupuunguzia nguvu utetezi unaotolewa na Dk Kitila kwamba hakuwa sehemu mpango wa kuuondoa uongozi wa sasa madarakani. Zitto, Dk Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba wanasubiri kukabidhiwa barua za kuvuliwa kwao madaraka na katika siku 14 wanapaswa wawe wamewasilisha utetezi wao wakieleza kwa nini wasifukuzwe uanachama kutokana na tuhuma zinazowakabili.

Dk Slaa

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema jana kuwa ilikuwa lazima viongozi hao wavuliwe madaraka hasa baada ya Dk Kitila kukiri kuhusika na waraka ambao anasema ulilenga kushinda kupitia uchaguzi halali ndani ya chama hicho.

“Hata katika ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe.Hakuna Katiba itakayokuruhusu kufanya mipango ya siri. Kwanza uchaguzi wa Chadema nani katangaza mpaka mipango ianzwe kutengenezwa sasa hivi?” alihoji Dk Slaa.
Alikiri kwamba watuhumiwa hao hawajapewa barua za uamuzi wa Kamati Kuu na alipoulizwa sababu, alisema Katiba ya chama hicho haitoi mwisho wa mtu kupewa barua, huku akihoji: “Wao nani kawaambia waende kwa waandishi wa habari?”

“Mimi ndiye Katibu Mkuu. Katiba inasema ni lini barua iandikwe? Utatokaje kwenye kikao alfajiri na wakati huohuo uandae barua za kuwapa?” alihoji Dk Slaa.

Mkutano leo

Mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa leo unatarajiwa kujibu  baadhi ya hoja za utetezi za viongozi hao zilizotolewa juzi. Zitto alifichua kile alichokiita tuhuma zilizotolewa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu akimaanisha kwamba tuhuma zilizotamkwa kwenye vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazikuwa kamilifu.

Habari zinasema uongozi wa Chadema utaweka wazi kile kinachodaiwa kuwa ni “Zitto kujitungia tuhuma, kisha kuzipatia majibu”, badala ya kujibu hoja ambazo zilitolewa na Kamati Kuu.

Jana, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema Kamati Kuu haiwezi kuchaguliwa tuhuma za kusema na za kuacha... “Hiyo hoja walete kwenye vikao, nani anayeipangia Kamati Kuu ichukue hatua gani pale inapotaka kufanya hivyo?”

Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene akizungumza jana alisema: “Kamati Kuu ilijadili mambo mengi na hayo ndiyo tunataka umma ufahamu msimamo wetu kama chama.”

Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema katika mkutano huo, huenda uongozi wa Chadema ukaweka wazi “makosa mengine” ambayo Zitto anadaiwa kuwa amewahi kuyafanya na kuonywa katika vikao vya ndani ikiwa ni pamoja na kiongozi huyo kutofika makao makuu ya chama hicho kwa zaidi ya miezi sita. “Kuna makosa mengi (Zitto) ameyafanya yenye sura ya kukiumiza chama chetu na alionywa mara nyingi tu, tena na vikao vya juu vya chama kuhusu mwenendo wake, lakini aliendelea na uasi.Sasa Kamati Kuu imechoka,” alisema mmoja wa maofisa wa Chadema Makao Makuu.

Habari zaidi zinasema katika mkutano wake wa leo, chama hicho kitatoa ufafanuzi kuhusu mikutano yote ya kichama ambayo imekuwa ikifanywa na Zitto, huku kukiwa na hoja kwamba alikuwa akifanya hivyo bila kuwashirikisha maofisa wa makao makuu wala sekretarieti ambayo kimsingi ndiyo inapaswa kuiandaa.

Wasomi wanena

Akizungumzia mgogoro huo, mtaalamu wa mambo ya siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema hali inayoendelea ndani ya Chadema ni matokeo ya vyama vya siasa kutofanya kazi kama taasisi.

“Misingi ya vyama haiweki wazi misingi ya watu kuwa viongozi. Kwa mfano, kesho nikitaka kujiunga na Chadema nitaweza kuwa Mwenyekiti? Misingi ya wazi hakuna,” alisema Mbunda.


Alisema hali ilivyo ndani ya Chadema kwa sasa ni furaha ndani ya CCM, kwani watu wanaona kuwa chama kilichoonekana kuwa mbadala hakiwezi hata kushughulikia mambo yake ya ndani.

Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema vyama vya siasa ni watu au kikundi cha watu wenye malengo na mitazamo tofauti.

“Ukisoma huo waraka utaona kuwa unazungumzia uongozi, upungufu uliopo kwenye uongozi na namna ya kubadili uongozi, mimi binafsi niseme ieleweke kwamba hata kwenye jumuiya yoyote mambo haya yapo hasa kwa kuwa walikuwa wanaelekea kwenye uchaguzi,” alisema. Alisema haoni kwa nini Zitto na Dk Kitila waonekane wahaini kwa kupanga mikakati yao ambayo walitaka kuitekeleza kupitia uchaguzi.


“Mabadiliko ni jambo la kawaida, hali hii ya kuwaondoa kwenye nyadhifa zao inawezekana ikawagharimu Chadema na inaweza kuwagharimu zaidi wakiwafukuza uanachama,” alisema Makulilo. 

Hii Post Ya Director Adam Juma Yazua Mapya Kuhusu Yeye Na Nisher. Fuatilia Hapa Majibu Makali Ya Adam

$
0
0
Kwenye instagram account inayoaminika kuwa ni ya Adam Juma, director bora wa video na kazi za wasanii Tanzania kumekuwa na post yenye
muonekano wa saini ya director Nisher ikiwa na maneno haya. "I m Not Next Level, I M A New Game' huku tukijua kuwa brand name ya Adam Juma inayompa heshima kila siku kwa kazi bora ni Next Level. Fuatilia Hapa



Fahamu hii post haijaonekana kwenye account ya Nisher kwa sasa ila watu wanaofatilia account yake Ya facebook, instagram na whatsup wanasema ilikuwepo kote na ameitoe hivi karibuni. 

Tunafahamu kuwa Nisher ameonekana kama Replacement ya Adam Juma au kimbilio la wasanii wanapotaka video bora kwa sasa hapa Tanzania baada ya Adam kusitisha kazi hii. Ila pia wasanii wamekuwa wakienda sana Kenya kufanya kazi na Ogopa kitu kinachopelekea mashabiki kuona bado nafasi ya Adam haijazibwa.

Baada ya hii post shabiki wa Nisher alitia neno hapo kuhusu ubora wa Nisher.


Majibu Ya Adam Juma Yalikuwa Hivi. 

SOURCE:Sammisago.

NAY WA MITEGO YUKO KENYA ANAKULA UJANA NA JAGUAR.ONA ALICHOPOST.

MTANZANIA HUYU ANAISHI KWA MATESO NA RISASI KICHWANI.MADAKTARI WASHINDWA KUITOA.

$
0
0
Na Makongoro Oging’
UJAMBAZI ni unyama, anayejishughulisha na kazi huyo ni mtu mbaya kupita kiasi. Hana stahili hata chembe ya kujumuika na jamii yenye raia wema.



Jambazi anaweza kubadili jina la mtu na kuitwa marehemu ndani ya kipindi cha kufumba na kufumbua. Leo hii, msomi wa sheria aliyebobea katika masuala ya katiba, Dk. Sengondo Mvungi, hayupo tena nasi hapa duniani. Majambazi wamekatisha uhai wake.

Dk. Mvungi alikuwa mjumbe wa Tume ya Katiba na alipania kutumia elimu yake kuisaidia nchi kupata katiba bora sana. Ndoto yake imekatizwa, Mungu amlaze mahali pema peponi ila kwa hakika tuwaalani majambazi na tumuombe Mungu awafanye washindwe.

Ubaya wa majambazi anaujua vizuri sana Fredrick Mdima, ukimsikiliza, simulizi yake inatia huzuni mno. Maisha yake yamebadilika kabisa. 
Ana siku 134 akiwa anaishi na risasi kichwani. Madaktari wamejitahidi kuitoa imeshindikana, sasa amebaki mgonjwa, kila siku maumivu ya kichwa hayamuishi, kikohozi mara kwa mara. Anatia huruma sana.

Mpaka Julai 15, mwaka huu, Mdima alikuwa mzima kabisa. Akiwa katika harakati za maisha, alipanda Basi la RS, akitokea Kagera alikokwenda kwa shughuli zake za mihangaiko ya kusaka riziki, akawa anarudi Dar es Salaam ambako ndipo yalipo makazi yake.

TUJUE MKASA WAKE KAMILI
Mwandishi wetu alimtembelea Mdima, nyumbani kwake, Yombo Dovya, Temeke, Dar es Salaam, kwa hakika hivi sasa anaishi kwa shida, mwenyewe anasimulia:

“Nilipanda basi Muleba, Kagera, nikiwa na matumaini tele ya kufika Dar es Salaam salama. Ilikuwa saa 12:00 asubuhi, sikujua kama saa mbili zijazo maisha yangu yatabadilika na kuwa ya mateso.
“Saa 2:00 asubuhi, basi likiwa kwenye Kijiji cha Kasindangwa, tulikuta lori limepaki katikati ya barabarani, dereva wetu na kila abiria aliyeshuhudia, alidhani lile lori ni bovu. Tulikuwa watulivu bila wasiwasi wowote.

“Dereva wa basi akaamua kupita pembeni kwa kujibana, kumbe lile lori lilikuwa mtego. Ghafla majambazi zaidi ya 10 wenye silaha za moto, walilizunguka basi tulilokuwa tumepanda.
“Binafsi nilikuwa nimefuatana na mwanangu, Method mwenye umri wa miaka 16, kwa maana hiyo masahibu haya yalinikuta mwanangu akinishuhudia.

“Wale majambazi baada ya kuzingira letu, walimuamuru dereva alizime kabisa. Mmoja wao akasema kwamba kati yetu sisi abiria kuna mwenye bunduki, hivyo walimtaka awakabidhi. Kumbe walimlenga askari polisi aliyevaa kiraia ambaye alisindikiza basi letu na kukabiliana na wahalifu.

“Askari huyo hakujitokeza, wale majambazi wakaanza kumimina risasi ovyo kwenye gari. Wote tukawa tumelala chini, huku kila mmoja akipiga kelele kwa namna alivyoweza kuomba msaada na kumtaja Mungu.
“Nilikuwa nimekaa siti za nyuma, bahati mbaya ikawa zaidi kwangu, maana katika zile risasi zilizopigwa, mbili ziliniingia kichwani.

“Damu zilitoka nyingi, wale mjambazi wakaamrisha abiria watoke nje. Yule askari baada ya kuona mimi navuja damu, aliisogeza bunduki jirani yangu kisha yeye akashuka kama raia wa kawaida.
“Wale abiria walipokuwa wanatoka nje walikaguliwa na kunyang’anywa fedha, simu na mali nyingine. Baada ya kumaliza uporaji, wale majambazi waliingia ndani ya gari na kunikuta nimezungukwa na dimbwi la damu, wakajua nimeshakufa, kwa hiyo walichukua ile bunduki na kuondoka zao.

“Kuanzia hapo sikujua kilichokuwa kinaendelea, nilipata fahamu ikiwa saa 8.00 mchana nikiwa Hospitali ya Biharamulo kabla ya kuhamishiwa Bugando siku iliyofuata, yaani Julai 16.
“Pale Biharamulo madaktari waliweza kunitoa risasi moja tu, nilipopelekwa Bugando kulikuwa na matumaini ya kutolewa iliyosalia lakini nako ilishindikana. Nilihamishiwa Muhimbili ambako pia madaktari walisema haiwezekani kuitoa. Wakasema inabidi nikubali matokeo na niishi nayo kwa miasha yangu yote.

MATESO YAKE
Mdima sasa hana uwezo wa kuzungumza vizuri, maana risasi kukwama kwake kichwani, imesababisha uharibifu wa mfumo wa fahamu.
Anasema akiwa amezingirwa na sikitiko: “Risasi hii kichwani imenisababishia matatizo makubwa kiafya, ikiwa ni pamoja na kukohoa mara kwa mara, kuumwa kichwa na kutoongea vizuri.”

Anabainisha kuwa risasi hiyo ndani ya kichwa chake ni ulemavu mkubwa, maana kwa sasa muda mwingi anajiuguza kutokana na kusumbuliwa na maumivu makali mara kwa mara, hivyo kumfanya ashindwe kujishughulisha na harakati za kusaka riziki.
Anaeleza: “Kwa kawaida shughuli zangu ni ufundi na uuzaji wa spea za magari ila kwa sasa mtaji umekata. Sina fedha, tangu siku nilipopata janga la kupigwa risasi, sijaweza kujishughulisha ufundi wala uuzaji was pea, nipo tu najiuguza. Mimi na kuumwa, kuumwa na mimi.”

KILIO CHAKE
“Natamani sana apatikane daktari wa kuweza kuitoa hii risasi, natamani sana kurudi katika yake ya kawaida, niendelee na shughuli zangu niweze kuilea familia yangu, niwasomeshe watoto wangu,” anasema Mdima na kuongeza.

UNAWEZA KUMSAIDIA MDIMA
Mbali na ombi hilo la kutolewa risasi, Mdima anatoa wito kwa kila mwenye uwezo kumuwezesha kadiri anavyoweza aweze kuihudumia familia yake, maana yeye kama baba ambaye ndiye nguzo ametetereka na nyumba nzima imeyumba.
Kwa mtu yeyote aliyeguswa na kilio cha Mtanzania huyu, anaweza kuwasiliana naye kupitia simu nambari 0719 754770 au 0689 715277.
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live