Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live

Tanzania yapata tuzo mpya, 'Tuzo za Watu', zinawahusu mastaa wanaopendwa zaidi katika filamu, muziki na utangazaji.

$
0
0

Katika mwaka 2014, tasnia ya burudani Tanzania imepata kitu kipya kabisa ambacho kinaweza kuwa chachu katika kuendeleza tasnia hiyo hapa nchini na kuwafanya wadau wa tasnia hiyo kuongeza juhudi katika kile wanachokifanya kwa ajili ya watu.

Mtandao wa Bongo5 umeanzisha tuzo zinazojulikana kama Tuzo za Watu ama kwa kiingereza ‘Peoples Choice Awards’, ambazo zinalenga katika kuwatunuku wana michezo, wanamuziki na watangazaji wanaopendwa zaidi hapa nchini.
Mwenyekiti wa Bongo5 Media Group, Luca Neghesti amesema kuwa kampuni hiyo itawatunuku tuzo wale wanaopendwa zaidi, na kwamba mshindi ataondoka na tuzo pamoja na shilingi milioni moja za kitanzania.
 “Sasa hivi tumeshuhudia ukuaji katika tasnia mbalimbali na tumeona ni wakati muafaka wa kuwatunuku wale wanaopendwa na wananchi, kuwapatia tuzo pamoja na zawadi ya fedha taslimu milioni 1." Amesema Luca Neghesti.
Ameongeza kuwa alizisajili tuzo hizo mwaka 2009 lakini kutokana na mipango na malengo ya kampuni hiyo aliamua kuziweka hadi hivi sasa.
Ameeleza kuwa tuzo hizi zitahusu watu wa rika zote na kwamba hazilengi kuleta ushindani kwa tuzo zingine hapa nchini kwa kuwa zinalenga kuwatunuku watu kutokana na umaarufu wao na jinsi wanavyopendwa na wananchi, na sio ubora.
“Tuzo hizi hazileti ushindani na tuzo zingine kwasababu hazilengi tasnia moja tu. Tanzania imesifiwa kwa uhuru wa vyombo vya habari na tuzo hizi zinalenga kujumuika na tuzo zingine kuhakikisha watanzania wanaopendwa na kufanya vizuri wanatambuliwa.” Neghesti amefafanua.
Upigaji kura unaanza wiki hii katika vipengele 11 ambapo wananchi watachagua majina ya washiriki watakaoshindana kwenye vipengele hivyo.
Awamu ya kwanza ya upigaji kura itafungwa baada ya wiki mbili kutoka siku ya kwanza ya upigaji kura na majina ya watu watano waliotajwa zaidi kutoka kwenye kila kipengele watachaguliwa kama watajwa wa mwisho. Kuanzia hapo, upigaji kura wa wananchi utajikita tu katika orodha ya majina hayo matano kwenye kila kipengele kinachoshindaniwa.
Unaweza kupiga kura kupitia www.tuzozetu.com au kwa njia ya SMS kwa kutuma neno ‘Tuzo’ kwenda namba 15678 na kisha utaletewa Menu.
Tuzo za watu mwaka 2014 zitajumuisha vipengele 11:
- MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW1 na jina' kwenda
15678)
- KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW2 na jina' kwenda
15678)
-MTANGAZAJI WA TV ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW3 na jina' kwenda 15678)
-KIPINDI CHA TV KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW4 na jina' kwenda 15678)
- MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW5 na jina' kwenda 15678)
-MWANAMUZIKI WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW6 na jina' kwenda
15678)
-MWANAMUZIKI WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW7 na jina' kwenda
15678)
-WIMBO UNAOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye 'TZW8 na jina' kwenda 15678)
- MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW9 na jina'
kwenda 15678)
-MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW10 na
jina' kwenda 15678)
- FILAMU INAYOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye 'TZW11 na jina' kwenda 15678)

Huyu ndio Msanii aliyetangaza kuwa atafungwa jela wiki hii.

$
0
0

Katika hali ambayo haikutegemewa, rapper Deandre Cortez Way aka Soulja Boy amewaambia mashabiki wake kuwa ataenda jela.

Rapper huyo mzaliwa wa Chicago ametweet February 15 na kuonesha kuwa baada ya siku tano ataenda jela. Hii ina maana itakuwa wiki hii mwishoni.
“5 more days until I go to jail. Appreciate everyone who was there for me while I needed y'all.” Alitweet Souja Boy bila kutoa ufafanuzi zaidi.
Lakini mwishoni wa mwezi uliopita, TMZ iliripoti kuwa rapper huyo alishitakiwa kwa kosa la kuwa na bunduki na kuvuka bila kusimama katika eneo alilopaswa kusimama huko Los Angeles.

MB Dog aliwahi kulipwa shilingi Milioni kumi kwa show moja miaka ile.

$
0
0
“Lakini uzuri wakati mimi naanza kufanya, kazi zilifanyika na misingi za ile kazi zilikuwa zimekaa tofauti na watu wanavyosikia. Kwa hiyo uoga hata wa mapromota ulikuwepo wakati wanatusogelea. Kwa hiyo hatukuwa tunalipwa laki tatu viiile.” Mbwana Mohammed aka MB Dog ameiambia tovuti ya Times Fm.
Huenda inawezekana ulikuwa hujui kwa sababu wakongwe waliokuwa wanahit enzi hizo hawakuwa na tabia ya kuweka wazi kiasi wanacholipwa kama wanavyofanya wakali wa bongo flava wa kizazi hiki cha dijiti.
Mkali huyo wa ‘Latifa’ ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa alikuwa anakutana na milioni kadhaa kwenye show zake, na kwamba kiasi kikubwa zaidi alichowahi kulipwa kilikuwa shilingi milioni kumi nchini Burundi.
“Yaani mimi show ya kwanza nimeanza kuifanya nimelipwa milioni tatu, show ya mwisho mimi kuifanya nimelipwa milioni kumi...ambayo ndiyo ilikuwa show ya maajabu yaani...kwa ubongo wangu  nawaza naweza kufanya show tena ya watu wengi kama wale!! Nadhani ilikuwa mwaka 2006.” Amesema MB Dog na kusisitiza, “milioni kumi za kitanzania”.
Kumbe Bongo Flava ilianza kulipa zamani japo kwa wachache! Na huenda ni kwa sababu tu watu walikuwa hawaweki wazi wanachoingiza.
Hapa tumpigie picha Mr. Nice wa enzi hizo kwa kutumia mfano wa MB Dog.
Kama kweli mambo yalikuwa hivi, inaweza kuwa moja kati ya sababu zilizozaa wazo kati ya wakongwe Juma Nature na Lady Jay Dee kutaka Leo iwe ‘Kama Jana’.
Source:Times fm.

MAJANGA!!

Tuzo Za Kili 2014 Zimezinduliwa Leo, Fahamu Alichosema George Kavishe Na Mabadiliko Hapa.

$
0
0
Tuzo za kili zimeanza rasmi mwaka 1999 na mambo mengi yameboresha baada ya wadau wa muziki Tanzania kutoa sababu zao.

Kili Music awards 2014 mwaka 2014 zimezinduliwa tarehe 17/2/2014. Brand Manager wa Kilimanjaro Bei amesema haya kuhusu mwaka huu.
1] mwaka huu Watanzania watapigakura kwa njia ya simu {sms] kuchagua msanii gani aingie kwenye category gani. Itakuwa kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia February 18 2014 category zote zitaonyeshwa na kura zitapigwa kwenda 15440, Unachagua msanii, kikundi au producer gani aingie kwenye category gani.
2] Kura zitapigwa mara 2, ya kuingia kwenye kipengele na yakushinda tuzo.
3] Timu ya watu 100 ikiwa na Waandishi, Watangazaji na wadau wa muziki watafatilia tu kuhusu wimbo kuwa kwenye mwaka husika,pia kipengele sawa na kama unavigezo vya kuingia kwenye tuzo hizi.
Note, Mabadiliko ya Tuzo za mwaka Huu Ndio Haya.
1] 2014 KTMA itakua na vipengele 36 na category 34 ni za kupigiwa kura na mbili ni zile category maalum za kuteuliwa tu. Mwaka jana palikuwa na vipengele 37, Imetolewa ya - Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka Huu.
2] Vipengele vimebadilishwa majina Ndio Hivi
- Mtumbuizaji bora wa kike wa muziki badala ya msanii bora wa kike ilivyokua mwaka jana.
- Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki badala ya msanii bora wa kiume
-Mwimbaji bora wa kiume Taarab ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume Taarab.
-Mwimbaji bora wa kiume bongofleva badala ya Msanii bora wa kiume bongofleva.
-Mwimbaji bora kiume band Badala ya msanii bora wa kiume band.
-Mwimbaji bora wa kike bongofleva badala ya msanii bora wa kike bongofleva.
-Mwimbaji bora wa kike Taarab badala msanii bora wa kike Taarab.
-Mwimbaji bora wa kike band badala ya msanii bora wa kike band.
-Msanii bora chipukizi anaeibukia badala ya msanii bora anaechipukia.
-Video bora ya muziki ya mwaka badala ya video bora ya wimbo ya mwaka.
-Wimbo bora wa Afropop badala ya wimbo bora wa bongo pop.
-Wimbo bora wa vionjo vya asili ya kitanzania badala ya wimbo bora wenye vionjo vya asili tu.
Note Sababu Ya Mabadiliko Ya Mwimbaji na sio Msanii.
-Neno Msanii linapendekeza maana zaidi ya moja. Mfano Msanii wa sanaa ya Uchoraji Na Hata Uigizaji.
Mabadiliko Ya Vipengele Yapo Chini Ya Basata.

NIMEFANYA MAPENZI NA SHEMEJI YANGU KWA BAHATI MBAYA..PLEASE HELP.

$
0
0











Naombeni ushauri wa hali na mali katika hili , Siku kadhaa zilizopita hapa nyumbani kwetu tulifanya sherehe ya birthday ya mtoto wetu kutimiza miaka
mitano tuliwaalika ndugu wengi hapa home kwa ajili ya sherehe hiyo, Mgeni mmoja wapo ni mdogo wa mume wangu ambae alikuwa ametoka mkoani so alifikia kwetu, sasa siku ya birthday katika sherehe hiyo tulikunywa sana kila mtu akawa safi mume wangu pombe zilimzidi ilipofika saa sita usiku akaniaga anaenda kulala, mimi nikabaki na baadhi ya ndugu tunakunywa, ilipofika saa saba nami nikajikokota kwenda kulala, nikaingia chumbani nikajitupa kitandani bila kuwasha taa mme wangu alinipokea kwa mahaba tukabinjuka, baada ya kumaliza kiu kikanisha nikaamka niende kunywa maji ile kuwasha taa nikakuta kumbe nilikosea chumba na niliye fanya nae mapenzi ni mdogo wa mume wangu nae alizania nimemtunuku mambo basi hakufanya ajizi akanipa dozi ya uhakika...Hichi kitu kinanisumbua akilini sana mpaka naona sina raha je nimweleze mume wangu kilichotokea ili nipate amani ama nitaharibu zaidi?

HUDDAH MONROE ATUPIA PICHA ZENYE UTATA KWENYE MTANDAO...MMHH JIONEE

$
0
0
Jamani huyu Dada Noma Jionee Hapa ...



LINAH SANGA NA SKENDO YA UJA UZITO WA MUHINDI AKA MDOSI.

$
0
0

Habari ya Mjini leo kutoka katika Gazeti Moja Linasema Linah Sanga Amedungwa Ujauzito na
Mdosi mmoja Ajulikanae kwa Jina Nagar Aneye Ishi Mbezi , amekuwa karibu na Mhindi huyo anayedaiwa kuishi Mbezi jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu sasa na kwamba mimba hiyo imeonekana kumfurahisha sana msanii huyo.

“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda mrefu na inaonekana hii mimba ameipenda sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi wake,” kilisema chanzo hicho kilichodai kuwa wawili hao wamekuwa wakiambatana pamoja katika sehemu mbalimbali za starehe...

Linah Alitafutwa ili Kujibu Habari Njema Hiyo lakini Alikataa kutoa Ufafanuzi zaidi kuhusu Hilo...

BABY MADAHA AAMUA KUACHA MZIKI NA FILAMU..SKENDO NA PRESHA ZIMEMCHOSHA.

$
0
0

Baby Madaha Amehabrisha kuwa Ameamua kuacha fani ya mziki na ya Uigizaji kwa kila anachosema kuwa kuna maisha ya Presha , kila unalofanya
linaandikwa mitandaoni na magazetini , Amesema kuwa kibao chake cha mwishi kinachoitwa MR DJ ndio kitakuwa cha mwisho yeye kufanya katika music...Amesema anatarajia kurudi katika fani aliyosomea Darasani....
Mweee Utaweza?

Rubani aliyeteka ndege ya Ethiopia ajisalimisha.

$
0
0
Maafisa wanasema rubani huyo ambaye jina lake halikutajwa ana umri wa miaka (30). Alichukua udhibiti wa ndege hiyo ya 767 kwa kufunga mlango wa rubani baada ya rubani kutoka kuelekea kujisaidia.
Maafisa wa Uswisi wanasema mara ndege hiyo ilipotua Geneva rubani huyo msaidizi alitoka kwenye ndege hiyo kwa kutumia kamba na kujisalimisha kwa maafisa na kusema kwamba alikuwa ni ‘haramia’ anayetafuta hifadhi ya kisiasa kwa sababu alikuwa akiogopa kuteswa nyumbani .
Chanzo cha mateso hayo hakijafahamika mara moja.Ndege hiyo ilitokea mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa na ilikuwa imebeba abiria 202.

Amanda aandika ujumbe unaolishambulia gazeti lililoandika habari inayodai kuwa anajiuza 'Live'

$
0
0
Kupitia Instagram, msanii huyo amepost picha ya gazei hilo na kuandika ujumbe unaolishambulia vikali.
"Asanteni sana Gazeti la K** kwa Habari yenu nzuri kabisa yenye kuipotosha jamii ...lakini niliwauliza swali moja mkabaki mnajikanyaga.. NILIWAHI KUMUUZIA BOSS WENU AU MWANDISHI YYT? ...Mluwahi kunikuta barabarani au kati ya wasanii wanaojulikana mpk bei zao za kujiuza me mnaweza kunitajia ya kwangu? Au mlikosa habari mkaamua kukulupuka na kunichafua? Haya mwisho wake unakuja wala msijali ila katika maneno mliyoandika hilo neno #LIVE ndio limenimaliza kabisa....haya movie ndio inaanza hapo."

Rihanna adai hakupenda kuwa maarufu na alipenda muonekano wa 'jike dume' tangu utotoni.

$
0
0

Robyn Rihanna Fenty, Mwimbaji maarufu na mwenye mafanikio makubwa kimuziki na hata katika ulimwengu wa mitindo ameeleza kuwa hakupenda kabisa kuwa maarufu, ila umaarufu ulikuja tu.

RiRi amefunguka wakati akifanya mahojiano na jarida maarufu la Vogue la nchini Marekani, ambapo yeye ndiye atakayelipamba jarada la toleo jipya la jarida hilo litakalotoka rasmi March mwaka huu.
Katika interview aliyofanyiwa na Plum Sykes, mwimbaji huyo alieleza kuwa alikuwa anapenda sana kuimba wakati akiwa mdogo lakini pamoja na kuimba sana hakuwahi kabisa kutaka kuwa maarufu.
“Nilikuwa naimba sana kama mtoto, sana. Nilifanya mazoezi sana kuitengeneza sauti yangu. Napenda kuimba. Nilipenda na haikuwa ratiba ya kila siku. It’s an expression. Sikupenda kuwa maarufu. Nilitaka tu muziki wangu usikike duniani kote. Kisha ikatokea na ikaja na umaarufu.”  Rihanna aliliambia jarida la Vogue.
Alifunguka pia kuwa alipokuwa mdogo alipenda sana muonekano wa ki-tomboy aka jike dume, na kwamba alikuwa anapenda sana kuvaa nguo za kiume na kuonekana kama mwanaume.
“Nilipokuwa na umri wa miaka 13 au 14, sikuwa nataka kuvaa nguo ambazo mama yangu alikuwa anataka nivae. Nilikuwa napenda sana muonekano wa kivulana. Marafiki zangu wote walikuwa wavulana. Nilikuwa napenda vitu ambavyo wavulana wanafanya.” Alisema Rihanna.
Aliongeza kuwa kutokana na kupenda muonekano huo, mama yake hakupata shida ya kuchagua nguo kwa ajili yake kwa sababu nguo alizokuwa anamchagulia kaka yake, alichagua kama hizo pia kwa ajili ya Rihanna hivyo wakawa wanavaa saresare.
“Tulikuwa tunavaa jeans zinazofanana, fulana zinazofanana.” Alisema Rihanna na kufafanua kuwa alikuwa anafanya vitu ambavyo viko kinyume na mpangilio wa jamii yake kuanzia maamuzi na muelekeo na kwamba alikuwa anafahamu hicho.

MATOKEO KITADO CHA NNE YAKO HAPA.

Ditto azungumzia miradi aliyoianzisha kupitia muziki wake, kampuni ya kuandaa matangazo na mashamba.

$
0
0
Kwa kuzingatia hilo, msanii wa bongo flava, Lameck Ditto anaweza kuwa tajiri wa baadae kwa kile alichokifanya endapo Mungu atajaalia miradi yake iende sawa.
Mkali huyo wa ‘Tushukuru kwa Yote’ ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa ameutumia muziki kufungua miradi mbalimbali na mwisho kufungua makampuni mawili. Kampuni ya kwanza ni ile inaendana na msemo wa ‘Kilimo Kwanza’, na ya pili inatokana na uwezo wake wa kiubunifu kama msanii  ‘kutengeneza matangazo ya radio’.
 “Muziki ndio kila kitu katika maisha yangu yaani tangu naanza maisha mpaka sasa, kwa hiyo miradi tofauti niliyoianzisha inatokana na muziki wangu …kwa sasa nina kampuni (Green Lights Music) inayohusika na uandaaji ya matangazo ya radio, kuna baadhi ya matangazo tumeshaanza kutengeneza na yanachezwa katika vituo mbalimbali natumaini miaka mitatu ijayo nitaisajili na kuipa jina la (Creative Agents).” Amesema Ditto
“Pia nina kampuni nyingine inayojishughulisha na masuala ya kilimo ‘Tunda Jema’. Nina shamba kubwa lipo Bagamoyo tayari ninaanza kuvuna matunda kama Maembe na Mananasi.”
Ameongeza kuwa kwa sasa anafanya utafiti kuhusu ufugaji wa kuku na kwamba wakati wowote atakapojiridhisha ataanza kufuga kuku kwa kuwa ufugaji ni ndoto yake ya muda mrefu.

Diamond kuhudhuria tuzo za 'AFRIMMA' zitakazofanyika Texas Marekani, zitahusisha wasanii wakubwa Afrika.

$
0
0

July 26 mwaka huu, wasanii wengi wakubwa Afrika kutoka katika mataifa ya 17 watakutana Dallas, Texas, Marekani kuhudhuria utoaji wa tuzo za kiafrika zinazojulikana kama ‘AFRIMMA Awards’, na tayari Diamond Platinumz tayari ameshaonesha uthibitisho wa kuwa katika daftari la mahudhurio siku hiyo.

Diamond amepost kwenye Instagram video inayomuonesha akifanya promo maalum iliyoandaliwa na watayarishaji akiwaambia mashabiki kwa swag za kimarekani kuwa atakuwepo siku hiyo, na kisha akaisindikiza na maneno yanayosomeka, “Yess! i'll be ryt there....Afrimma Awards 26/07/2014 Texas, Dallas (USA).”
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Big A Entertainment na African Muzik Magazine, zimelenga katika kuwatunuku wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika waliopo duniani kote na itagusa nyanja mbalimbali za burudani ikiwa ni pamoja na wasanii wa muziki, wachezea santuri aka Dj’s, watayarishaji wa muziki, mameneja na watu wanaousapoti utamaduni wa Afrika.
Tuzo hizo zinatarajiwa kusindikizwa na vicheko vya mara kwa mara kwa kuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo ni mchekeshaji maarufu wa kimataifa, The Basket Mouth na atakuwa na muigizaji mrembo wa Nollywood, Juliet Ibrahim.

Ashanti aeleza siri ya kuwa na umbo lenye mvuto wa 'kibinti' ingawa umri umeenda.

$
0
0
Mwimbaji Ashanti Shequoiya Douglas mwenye umri wa miaka 35, yeye ni mmoja kati ya wanawake maarufu wanaopata huduma ya daraja la kwanza na wana pesa nyingi, lakini bado wanaumbo lenye muonekano wa binti mwenye miaka 25 hivi kibongobongo.
Mwimbaji huyo wa ‘Foolish’ alipoulizwa na Nicolebitchie kuhusu siri ya umbo lake alifunguka kuwa ni uchaguzi wa chakula (kuachana na vyakula vya mafuta mengi), na mpangilio wa kula lakini pia mazoezi yanayoitwa ‘squat’ maalum kwa kukata tumbo.
“You know what? I’m going to be honest with you. This may be TMI but a great colonic does wonders. Wonders… I promise you… Colonics and squats and cut out fried foods.” Alisema Ashanti.
Huenda hii ikawa siri ya umbo la Jennifer Lopez ambaye ana miaka zaidi ya 40 na mama watoto mapacha lakini bado ana umbo la kibinti.
Katika hatua nyingine, Ashanti mbaye albam yake ya ‘Braveheart’ inatarajiwa kuingia sokoni March 4 mwaka huu, amesema tayari watu wengi wameshaisikiliza albam yake na wameipenda sana na kwamba ndani ya wiki mbili zijazo ataenda Jamaica kukutana na Beenie Man na kushuti pamoja video ya wimbo wake ‘First Real Love’.

Abdu Kiba aeleza chanzo cha ukimya wa kaka yake 'Ali Kiba'

$
0
0
Abdu Kiba ameeleza kuwa ukimya wa ndugu yake unatokana na kubanwa na majukumu ya kifamilia.
“Unajua watu wengi wanahisi vibaya sana, mara mwingine anaibuka na kusema amefulia kwenye game,sio kweli naomba niweke sawa kuhusu suala hili ni kwamba Ally Kiba alikuwa na majukumu ya kifamilia pamoja na kazi zake,maana nakumbuka tangu anitambulishe kwenye muziki wa Bongo Flava ndio alianza kubanwa na mambo  yake binafsi.” Amesema Abdu Kiba.
Hata hivyo, mashabiki wa Ali Kiba wana kila sababu ya kukaa mkao wa kusikia hits za mkali huyo mwaka huu.
“Niliwahi kuzungumza nae hivi karibuni, akaniambia mwaka huu anatarajia kuja kivingine katika game. Kwa sasa anajaribu kumalizia baadhi ya nyimbo alizorekodi ili mwaka huu mashabiki wazisikie katika vituo mbalimbali vya radio.” Alisema Abdu Kiba.

Wyre, Chameleone na Radio & Weasel watajwa kuwania tuzo za muziki za dunia, kuchuana na wasanii wakubwa duniani.

$
0
0
Wyre na Chameleone watachuana na wanamuziki wenye majina makubwa kimataifa katika kipengele hicho kama vile Jay Z, Kendrick Lamar, Justine Bieber, Chris Brown, Kanye West, Trey Songs na wengine.
Radio na Weasel wao wanachuana na makundi makubwa zaidi ya 240 duniani, yakiwemo Backstreet Boys, Bon Jovi, Boyzone, Destiny’s Child, Mafikizolo na P-Square.
Mshindi wa tuzo hizo atategemea idadi ya mashabiki alionao kutoka kona zote za dunia ambao watashiriki kumpigia kura mara nyingi wawezavyo kwa njia ya mtandao.

Fid Q aitaja 'Machozi Jasho na Damu' ya Profesa Jay kama albam bora ya karne.

$
0
0
Tajiri huyo wa mashairi na flow ametweet ujumbe huo wakati akijibu tweet ya Oscar Maboko aliyoeleza kuwa albam hiyo iliuza nakala milioni kadhaa lakini iliathiriwa na wizi za kazi wasanii.
"#MachoziJashoNaDamu is an indisputable/classic/dope/great&prolly the best album of the 1st century! #PROFJ @OscarMaboko @africanhiphop." Ametweet Fid Q.
Katika hatua nyingine, mdau huyo wa muziki, Oscar Maboko alieleza kuwa anaamini hata albam ya kwanza ya Sugu enzi hizo anaitwa 2 Proud iliathiriwa kimauzo na kanda za kurekodi kwenye Fm Radio zilizokuwa zinauzwa mtaani na kwamba karibia kila kijana aliyekuwa na radio cassette alinunua nakala hizo.

Mwanamke mwenye ndevu kama mwanaume apokea vitisho vya kuuawa, adai anajiona mwenye mvuto zaidi.

$
0
0
Mwanamke huyo ambaye anakabiriwa na tatizo la kuwa na vinyweleo vingi kupita kiasi, tatizo linalojulikana kitaalamu kama ‘polycystic ovary syndrome’, ameeleza kuwa alianza kupata tatizo hilo akiwa na umri wa miaka 11 na kwamba alikuwa akizinyoa mara mbili kwa wiki.
Ameeleza kuwa alipokuwa shuleni alikuwa akionewa sana kwa kuitwa majina mengi ya kejeli kama ‘jike dume’, na kwamba alikuwa anashindwa hata kuwaangalia watu usoni na alipotoka shule alijifungia ndani siku zote asionekane mara kwa mara.
Ameongeza kuwa kutokana na kuishi katika hali hiyo alifikia hatua akafikiria kujiua.
Hata hivyo, Harnaam amesema kuwa amejiunga na dini ya Sikh na kubatizwa, na kwamba imani ya dini hiyo hairuhusu watu kunyoa vinyweleo vyao kwa kuwa Mungu ndiye aliyewaumba hivyo. Kwa hiyo ameziachia nywele zake na sasa anaonekana kama mwanaume akiwa na nywele nyingi kidevuni, mikononi na kifuani.
Imani hiyo imempa ujasiri zaidi juu ya muonekano wake, na anajiona mwanamke mwenye mvuto zaidi.
“Nahisi nimekuwa mwanamke zaidi, nina mvuto zaidi na nadhani naonekana hivyo pia. Nimejifunza kupenda jinsi nilivyo na hakuna kitakachonitikisa sasa hivi.” Amesema Harnaam.
“nawezza kwenda kwenye maduka ya wanawake bila kuhisi kuwa sitakiwi kuwa kule. Navaa skirts, gauni na vidani na napenda kutengeneza kucha zangu kama msichana mwingine yeyote.”
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live