Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live

FORMULA MPYA YA KUSAHIHISHA MITIHANI YAWABEBA WENGI MATOKEO KIDATO CHA NNE.

$
0
0

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne wa 2013, huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 15.17.

Matokeo hayo ni ya kwanza tangu kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa upangaji ambao ulipanua wigo wa alama na madaraja, hivyo kutoa nafasi kubwa zaidi kwa watahiniwa kufaulu.

Licha ya kuanza kutumika kwa mfumo huo, idadi ya waliofeli imeendelea kuwa kubwa kwani watahiniwa 151,187 sawa na asilimia 42.91 wamepata sifuri. Kati ya hao, wavulana ni 78,950 sawa na asilimia 41.54 na wasichana ni 72,237 sawa na asilimia 44.51.


Kadhalika matokeo hayo yameendelea kushuhudia baadhi ya watahiniwa wakiandika matusi kwenye karatasi zao za majibu, huku wengine wakichora vitu vya ajabu kwenye mitihani hiyo, huku wengine wakishindwa kuandika chochote kwenye karatasi hizo.
Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema waliofaulu mtihani huo ni 235,227 sawa na asilimia 58.25 ya 404,083 ya waliofanya mtihani huo, ikilinganishwa na 185,940 sawa na asilimia 43.08, waliofaulu 2012.


Dk Msonde alisema wasichana waliofaulu ni 90,064 sawa na asilimia 55.49 na wavulana ni 111,088 sawa na asilimia 58.45.
Alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa ni 427,679 wasichana wakiwa ni 199,123 sawa na asilimia 46.56 na wavulana walikuwa ni 228,556 sawa na asilimia 53.44. Kati yao watahiniwa wa shule ni 367,163 na watahiniwa wa kujitegemea ni 60,516.
Dk Msonde alisema watahiniwa 23,596 ambao ni sawa na asilimia 5.52 ya waliojiandikisha, hawakufanya mtihani huo.
Dk Msonde alisema matokeo hayo yalipangwa kwa kutumia alama zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome mwaka jana.
Alama hizo ni A: 75-100, B+:60-74, B:50-59, C:40-49, D:30-39, E:20-29 na F:0-19. Kabla ya mabadiliko hayo, alama zilizokuwa zikitumiwa kupanga matokeo ya kidato cha nne ni A:80-100, B:65-79, C:50-64, D:35-49 na F: 0-34.
Alisema pia alama za maendeleo ya wanafunzi zilizotumika ni 30 huku mtihani wa mwisho ukichangia alama 70.
Kuhusu waliochora na kuandika matusi, Dk Msonde alisema: “Wengine wamechora nyumba, wengine picha za freemason na michoro mingine ambayo haiendani na somo husika.”

Hata hivyo, alisema tabia ya kuchora michoro hiyo imepungua ikilinganishwa na 2012.
Ubora wa Ufaulu
Dk Msonde alisema watahiniwa waliofaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu ni 74,324 sawa na asilimia 21.09 wakiwamo wasichana 27,223 sawa na asilimia 16.77 na wavulana 47,101.
Alisema waliopata daraja la kwanza ni 7,579 sawa na asilimia 2.15 wavulana 5,030 sawa na asilimia 2.65 na wasichana wakiwa 2,549 sawa na asilimia 1.57, wakati waliopata daraja la pili ni 21,728 sawa na asilimia 6.17, wakiwamo wavulana 14,167, asilimia 7.45 na wasichana 7,561 ambao ni asilimia 4.66.
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa waliopata daraja la tatu ni 45,017 sawa na asilimia 12.78; wavulana 27,904 sawa na asilimia 14.68 na wasichana 17,113 sawa na asilimia 10.54.
Watahiniwa waliopata daraja la nne ni 126,828 sawa na asilimia 36 na wavulana wakiwa ni 63,987 na wasichana 62,841 sawa na asilimia 38.72.
Ubora wa ufaulu kwa mwaka 2013 umepanda kulinganisha na mwaka 2012 ambapo waliofaulu kwa daraja la kwanza mpaka la nne walikuwa ni 159,747 sawa na asilimia 43.08 huku waliopata sifuri wakiwa 210,846 sawa na asilimia 56.92.
Watahiniwa wa shule
Dk Msonde alisema watahiniwa wa shule waliofaulu mtihani huo ni 201, 152 sawa na asilimia 57.09 kati yao wasichana wakiwa 90,064 sawa na asilimia 55.49 na wavulana ni 111,088 sawa na asilimia 58.45.
Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo ni 34,075 sawa na asilimia 66.23 ya waliosajiliwa, wakati 2012, watahiniwa wa kujitegemea 26,193 walifanya mtihani huo.
Kuhusu mtihani wa maarifa (QT), Dk Msonde alisema waliofaulu mtihani huo ni 6,529 sawa na asilimia 43.38.

MAPENZI YA RAY, CHUCHU HANS NI PIGO!

$
0
0

Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
Ni pigo kubwa! Ile ndoa inayodaiwa kukaribia
kufungwa kati ya nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Miss Tanga 2006 aliye pia msanii wa filamu Bongo, Chuchu Hans imepingwa isifungwe mpaka mambo f’lani yakae  sawa.
Kwa mujibu wa mtonyaji wetu, Ray na Chuchu wako mbioni kufunga ndoa wakati wowote kuanzi Mei, mwaka huu, lakini mjadala mzito uliopo mbele yao kwa sasa ni uhalali wake.
“Unajua wanachofahamu wao (Ray na Chuchu) wanaweza kufunga ndoa kwa ulaini kabisa, lakini ukweli ni kwamba kuna ugumu mkubwa.

UGUMU ULIPO
“Kanisa analosali Ray, viongozi wanasema wao si wa dunia hii mpaka wakubali kufunga ndoa ambayo mmoja wa wahusika ana ndoa yake,” kilisema chanzo hicho.
Kikaendelea: “Kwa hiyo kama wako tayari kufunga ndoa hiyo lazima Chuchu akubali kubadili dini yeye ndipo ataruhusiwa kungia kanisani kufungishwa ndoa.”

KANISA LA RAY
Juzi Alhamisi, Risasi Jumamosi lilifunga safari hadi kwenye Kanisa la Living Water-Makuti Kawe, Dar ambako mpaka mwaka uliopita magazeti pendwa yaliandika Ray anaabudu huko.
Lengo la Risasi Jumamosi lilikuwa kuonana na Mtume na Nabii Onesmo Ndegi lakini hakuwepo ofisini, ila msaidizi wake mmoja alipopatikana alikiri kumfahamu Ray.
Msaidizi:  Ray alishasali hapa, lakini sijamwona siku nyingi, sijui ana matatizo gani?
Risasi Jumamosi: “Oke, tukiacha hilo la kutofika kwa siku nyingi. Lililopo sasa hivi ni kwamba anataka kufunga ndoa na dada mmoja anaitwa Chuchu Hans ambaye ana ndoa tayari, hajaachika na mumewe yu hai. Unasemaje kuhusu hilo?
Msaidizi: “Sisi hatuamini katika kuachana. Kama alishafunga ndoa na mume yupo hai, hao wametengana tu, lakini ndoa yao ipo.
“Huyo mwanamke alishajifunga, kifungo chake kitatenguliwa pale tu mumewe atakapoondoka duniani (kifo).

KANISA LA MTAKATIFU MAXIMILIAN KOLBE
Baada ya kuondoka kanisani hapo, mapaparazi wetu walikwenda Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe, Mwenge, Dar es Salaam.
Risasi Jumamosi liliambiwa Baba Paroko hakuwepo kwa wakati huo, lakini muumini mmoja aliyesema yeye ni mwalimu alipoulizwa kuhusu nafasi ya Ray kufunga ndoa na Chuchu Hans alisema:
“Maandiko yako wazi. Sasa kama huyo mwanamke ana mume wake tena mmesema yupo nje ya nchi, siku akija si atamshika ugoni kwa mke wake?
“Huwezi kufunga ndoa kama bado una ndoa. Mungu hajaagiza hivyo. Ndiyo maana sisi (Wakristo) huwa tunatoa siku ishirini na moja za kutangaza ndoa ili kama kuna mwenye pingamizi ajitokeze na kulianika.
“Watu waongo siku hizi. Wapo wachumba wanakuja kuandikisha ndoa kumbe mmoja bado yupo kwenye ndoa halali.”

IMANI YA KIISLAM INASEMAJE?
Mapaparazi wetu hawakuchoka, walimtafuta Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum ambaye kuhusu Ray na Chuchu kufunga ndoa alifunguka hivi:
“Kama Chuchu ni Muislam, itabidi Ray abadili dini awe Muislam, si vinginevyo.”
Risasi Jumamosi: Chuchu alifunga ndoa Bomani na mume Mkristo, ila yeye Muislam. Inakuwaje hapo?
Sheke Mkuu: “Itakubalika kama Ray atabadili dini tu, maana hiyo ndiyo ya Bomani, Kiislam siyo.”

JOHARI, MAINDA WAPATANA
‘Johari’ ambaye ni Blandina Chagula na ‘Mainda’ mwenye uhalisia wa jina la Ruth Suka (zamani Mwanaid), wawili hao sasa ni mashosti wakubwa baada ya kuwa na bifu la miaka 8 kisa kikitajwa  kuwa ni ‘kaka mkubwa’ huyo (Ray) kuwachanganya kimapenzi.
Kwa mujibu wa chanzo, mastaa hao wanaotamba kwenye filamu za Bongo kwa miaka mingi wameamua kumaliza tofauti zao huku wengi wakitafsiri kuwa, wanashikamana kwa sababu ya  kuumaliza uhusiano wa Chuchu na Ray. Haikufafanuliwa.

MADAI MENGINE
Pia ilidaiwa kuwa, Mainda aliamua kumaliza bifu na Johari kwa sababu mchungaji wake alimtaka  kufanya hivyo.
“Niliwakuta kambini wakishuti filamu, Mainda akaniambia aliitwa kushiriki filamu hiyo kama mpambaji, Johari yeye amecheza baadhi ya  vipande ndipo Mainda akamtaka mwenzake wamalize tofauti zao,” kisema chanzo chetu.
Hivi karibuni, Risasi Jumamosi liliinasa picha iliyotundikwa mtandaoni na Mainda akimwonesha yeye, Johari na Mtangazaji wa StarTV, Sauda Mwilima.
Mainda aliisindikiza picha hiyo na maneno  yaliyosema: “Nimejifunza kitu katika maisha, kusamehe.”
KAKA MKUBWA RAY
Juzi, Risasi Jumamosi lilimpigia simu ya mkononi Ray lakini hakupokea. Akatumiwa meseji, hakujibu!
CHUCHU HANS
Baada ya kusomewa mashitaka yote, alijibu kwa ufupi: “Sina cha kuongea.”
JOHARI
Johari naye hakupokea simu yake ya mkononi licha ya kuita kwa muda mrefu na kukatika kisha kupigwa tena. Akatumiwa meseji, hakujibu!
MAINDA
Na yeye simu yake iliita sana bila kupokelewa, akatumiwa meseji, hakujibu!
Credits:Global Publishers

Rooney awa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi EPL baada ya kusaini mkataba mpya Manchester United.

$
0
0
Rooney ambaye ameichezea timu hiyo tangu  mwaka 2004, atakuwa anapata kitita cha pound 300,000 kwa wiki, sawa na dola 500,000 ni hivyo kuwa mchezaji wa ligi kuu ya Uingereza (EPL), anayelipwa fedha nyingi zaidi.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Uingereza, mkataba huo utakapoisha inaweza kuwa ndio wakati ambapo mchezaji huyo atakakuwa anastaafu soka na kwamba atabaki kuwa katika benchi la ufundi la timu hiyo.

Said Fella: Mimi sio mwanamuziki, ila kuna muda nauzingua tu muziki.

$
0
0
Fella ambaye ana mradi mpya wa Mkubwa na Wanawe, amesikika kupitia kipindi cha ‘Trending Africa’ cha 100.5 Times Fm alipoulizwa kuhusu uhusika wake kwenye game kama mwanamuziki kwa kuwa ameshawahi kuachia track hewani.
“Mimi ujue sio kwamba naamua kufanya muziki, ila kuna muda tu nakaa nasema bwana ngoja nipeleke ladha kwa mashabiki wetu, ndo maana natoaga ile ladha tu. Mimi sio kwamba mimi ni mwanamuziiiki, hapana. Mimi nasimamia muziki bana, lakini sio mwanamuziki, ila kuna muda huwa nauzinguazingua tu muziki.” Amesema Said Fella.
Ameeongeza kuwa yeye huwa anafanya ngoma muda mwingine kwa lengo la kufurahisha watu tu na kuwaonesha wanamuziki wake kuwa anapokuwa anawaelekeza vitu kwenye muziki wajue anajua kweli na sio kwamba hafahamu.
Sifanyi kubahatisha kufanya muziki, yaani niliamua kuingia kufanya muziki kama nilikuwa mimi ndiye meneja wa kwanza Tanzania niliangalia muziki unafanya hivi, kwanza nilianza kuusoma mimi mwenyewe mpaka nikaanza kuusimamia. Ndio maana hadi leo ni mwaka wa 14 niko kwenye usimamizi wa muziki.”
Mwaka 2012, Fella alianza kufanya muziki wa aina ya Taarabu na kutangaza kuwa ataachia albam nzima ya nyimbo za aina hiyo.

HATIMAYE HUDDAH MONROE AMTAJA MPENZI WAKE MPYA..HUYU HAPA.

$
0
0
Aliyekuwa mwakilishi wa Kenya katika jumba la Big Brother msimu uliopita, Huddah Monroe ambaye
pia alikuwa mpenzi wa rapper Prezzo, ametangaza kuwa kwenye penzi jipya na msanii mwingine wa Kenya aitwae Colonel Mustafa.

MAJINA YA WASICHANA NA WAVULANA 10 BORA KWENYE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE.

$
0
0




Kwenye matokeo ya kidato cha nne Watahiniwa wa kike wamefanya vizuri kwa kuchukua nafasi saba kati ya 10 za juu, huku Shule ya Marian Girls ya Pwani ikiongoza kwa kuwa na wanafunzi wanne. 

Mwanafunzi aliyeongoza ni Robina Nicholaus wa Shule ya Marian Girls, akifuatiwa na Magrath Kakoko wa St Francis (Mbeya) wakati wa tatu ni Joyceline Marealle kutoka Shule ya Canossa (Dar es Salaam).
Wengine ni Safarina Mariki na Abby Sembuche wa Marian Girls, wakati wavulana pekee kwenye wanafunzi 10 bora ni Sunday Mrutu kutoka Anne Marie (Dar es Salaam) na Nelson Rugola Anthony na Emmanuel Mihuba Gregory wa Kaizirege (Kagera).

Wanaofuata ni Janeth Urassa kutoka Marian Girls (Pwani) na Angle Ngulumbi wa St Francis (Mbeya).

Wasichana 10 bora
Wasichana waliofanya vizur kwenye mtihani huo wameongozwa na Robina Nicholaus (Marian Girls), Magrath Kakoko (St Francis), Joyceline Leonard Marealle (Canossa), Safarina W Mariki, Abby T Sembuche na Janeth Urassa (Marian Girls).


Wengine ni Angle Ngulumbi (St Francis), Getrude James Mande wa Precious Blood (Arusha), Violet Mwasenga wa St Francis na Catherine Swai kutoka Marian Girls.


Wavulana 10 Bora
Wavulana waliofanya Vizuri ni Sunday Mrutu wa Anne Marie, Nelson Rugola Anthony na Emanuel Mihuba Gregory wote kutoka Kaizirege, Razack Hassan wa St Matthew’s (Pwani) na Hamis Msangi kutoka Eangles (Pwani).
Matokeo ya Kidato cha Nne
Matokeo ya Kidato cha Nne 2013/2014



Wengine ni Joshua Zumba wa Uwata (Mbeya), Brian Laurent na Mohamed Ally wa Marian Boys (Pwani), Shahzill Msuya wa St Amedeus (Kilimanjaro) na Shabani Hamisi Maatu wa Mivumon Islamic Seminary (Dar es Salaam).


Shule za serikali hoi

Matokeo ya kidato cha nne yanaonyesha kuwa shule kumi za kwanza ni za binafsi tu na shule za Serikali zimeanguka vibaya.


Shule bora ni St. Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Pwani, Feza Girls ya Dar es Salaam, Precious Blood ya Arusha, Canossa ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Anwarite Girls ya Kilimanjaro, Abbey ya Mtwara, Rosmin ya Tanga na Don Bosco Seminary ya Iringa.


Katika shule zenye watahiniwa chini ya 40 shule iliyoongoza Matokeo ya Kidato cha Nne ni Kaizirege ya Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, Thomas More Machrina ya Dar es Salaam, Mwanza Alliance ya Mwanza na Queen of Apostles Ushirombo Seminary ya Geita. 

Nyingine ni St Joseph Kilocha Seminary ya Njombe, Bethelsabs Girls ya Iringa, St Mary Junior Seminary ya Pwani, Maua Seminary ya Kilimanjaro na Hellen’s ya Dar es Salaam(Matokeo ya Kidato cha Nne). 

Diego Maradona Kamvalisha Pete Huyu Mpenzi Wake.

$
0
0

Diego Maradona amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake mwenye miaka 23 Rocio Oliva baada ya kugundua wanategemea mtoto wao wa kwanza.

Rocio ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa mpira wa miguu ameanza mahusiano na Maradona mwaka jana na hivi karibuni alivalishwa pete kwenye sherehe ndogo ndani ya hoteli ya Rome  kwenye Valentines Day. Hii ilikuwa siku mbili tu baada ya binti mwingine aliyewahi kuwa na Maradona kusema kuwa anaujauzito wa star huyo, Binti huyu anaitwa Ojeda.
Maradona amekanusha uvumi huo na kusema sio baba wa mtoto huyo. Fahamu Maradona anatambua watoto  wake wawili na aliyekuwa mke wake Claudia Villafane na mtoto wake wa kiume Diego na mwingine wa kike anaitwa Jana aliyezaliwa mwaka 1996.

Diego Maradona Kurudi Uwanjani Tena Na Timu Atakayochezea iko Hapa.

$
0
0
Nyota wa kimataifa kwenye soka ambaye ni mchezaji mwenye umri wa miaka 53 kutoka  Argentina Diego Maradona amekuwa katika mazungumzo na klabu
ya Deportivo Riestra, ambayo inashiriki ligi ya chini kabisa  kwa lengo la kujiunga nao kama mchezaji mpaka kumalizika kwa msimu.
Nchini kwake ni maarufu kwa jina ‘God’  Maradona amekuwa akipambana na uzito katika siku za hivi karibuni kwa lengo kujiweka sawa na fiti  kabla ya kuanza mchezo wake wa kwanza March 23.
Mmoja wa wachezaji wa Deportivo Kiungo Victor More, amesema yuko tayari kuvua jezi yake nambari 10 anayovaa sasa na kumkabidhi Maradona atakapo saini kuichezea klabu hiyo na pengine mkongwe huyo anayetumia mguu wa kushoto akarejea kuitendea haki jezi hiyo aliyokuwa akiivaa enzi zake.

BAADA YA KULALAMIKA, SASA POSHO YA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUWA SH. 500,000/=

$
0
0

Posho Bunge Maalumu la Katiba kuwa 500,000 kwa siku. Habari zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la Leo kwamba Kamati ya kufuatilia posho za wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000 kwa siku imethibitishwa ni kweli. Natoa wito kwa Wananchi wote kushinikiza kwa Rais pendekezo hili asilikubali. Naunga mkono wazo la mjumbe wa Bunge Maalum ndg Julius S. Mtatiro la kuorodhesha majina ya wote wanaopinga nyongeza ya posho. Nitaweka sahihi kwenye petition yake hiyo mapema kesho asubuhi. Wagombea uenyekiti nao wanaahidi kupandisha posho. Nawaonya wasithubutu kutoa ahadi hiyo kwani sio mamlaka yao. Mgombea mwenye sera ya posho hatapata kura yangu na nitashawishi wajumbe wengine wasimpe kura. #..

MNYIKA ATOA MAONI KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013.

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mh. John Mnyika.

Maoni yangu kuhusu matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne wa mwaka 2013 yaliyotangazwa na kuelezwa kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 15.17 yamedhihirisha tahadhari niliyotoa kuhusu mabadiliko ya viwango vya ufaulu yaliyotangazwa na Serikali tarehe 30 Oktoba 2013.

Serikali kwa barakoa (veil) ya kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) imeamua kulificha taifa juu ya Matokeo Mabaya ya Sasa (Bad Results of Now). Hivyo, wachambuzi wa masuala ya elimu wanapaswa kutoa takwimu za matokeo yangekuwa namna gani iwapo viwango vya awali vya ufaulu vingetumika ili  nchi ijue hali halisi kwa manufaa ya wananchi.

Aidha, natoa mwito kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuweka wazi kwa umma ripoti za uchunguzi zilizoundwa kuwezesha wananchi kuihoji Serikali iwapo kupanda huko kwa ufaulu ni matokeo ya kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza au ni kiini macho cha mabadiliko ya wigo wa alama na madaraja?

Ukweli ni kuwa hali ya mazingira ya kujifunza na kujifunzia katika shule nyingi za msingi na sekondari hasa za umma sio nzuri kutokana na kutokuwa na vitabu vya kutosha, maabara za kutosha, waalimu wenye sifa wapo wa kutosha na kuboresha maslahi ya waalimu ambayo yamekuwa yakilalamikiwa kwa siku nyingi.

Ikumbukwe kwamba miaka mitatu mfululizo, mfumo wa elimu wa Tanzania, na hususani kwa upande elimu ya msingi na sekondari umekuwa ukiporomoka kwa kasi ya ajabu. Kufuatia kuporomoka huko, na hasa kushuka kwa viwango vya ufaulu, Serikali kwa vipindi totauti (mwaka 2010 na 2012) imeund Tume kuchunguza sababu za kushuka kwa viwango vya ufaulu.

Ingawa ripoti za tume zilizoundwa kuchunguza sababu za kushuka kwa ufaulu hazijulikani kwa wananchi ambao ni wadau wakuu wa elimu, Serikali imeendelea kutoa maagizo na matamko mbalimbali kuhusu viwango vya ufaulu.

Ikumbukwe kuwa mwezi Mei, 2013 Serikali ilitangaza kufutwa kwa matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2012 kutokana na kushuka mno kwa viwango vya ufaulu ambapo zaidi ya asilimia 65 ya wanafunzi walipata daraja sifuri na kuamuru matokeo hayo kupangwa upya.

Takribani miezi sita baadaye, yaani 30 Oktoba 2013 Serikali ilitangaza kubadili viwango vya ufaulu bila kutoa ufafanuzi kuhusu msingi wa mabadiliko hayo na kuwasilisha bungeni ripoti za kamati/timu zilizochunguza kuporomoka kwa ufaulu.

Hivyo hata baada ya kauli ya Serikali kuwa “kundi la watahimiwa walioshindwa Mtihani na ambalo awali lilikuwa likiandikwa kama ‘failures’ litaendelea kujulikana kama Daraja Sifuri (Zero) bado Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapaswa kutoa ufafanuzi juu ya athari za mabadiliko hayo kuwezesha Bunge kusimamia Serikali ipasavyo.

Pamoja na mpango wa Serikali wa kuficha matokeo mabaya ya kidato cha nne ya mwaka 2013 bado idadi ya waliofeli imeendelea kuwa kubwa kwa kuwa watahiniwa 151,187 sawa na asilimia 42.91 wamepata sifuri. Kati ya hao, wavulana ni 78,950 sawa na asilimia 41.54 na wasichana ni 72,237 sawa na asilimia 44.51. Aidha, katika matokeo hayo hali ya watahiniwa kutokuweza kufanya mtihani kabisa kwa kiwango cha kuacha karatasi tupu, kuchora vitu vya ajabu au kuandika matusi inadhihirisha udhaifu mkubwa uliopo katika mfumo wetu wa elimu kwa kuwa wahusika wameweza kupanda kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne wakiwa hawana uwezo wa kufanya mitihani.

Hivyo, Serikali ihojiwe ieleze dhamira ya kweli ya mabadiliko ya viwango vya ufaulu na kutakiwa kushughulikia vyanzo vya matatizo katika elimu badala ya kuficha matokeo mabaya na hali halisi za wahitimu.

Serikali inafanikiwa kuficha udhaifu kwa sababu ripoti kamili za uchunguzi juu ya ufaulu duni wa wanafunzi hazijawahi kuwekwa hadharani ili kujua kiini cha tatizo. Mara zote Serikali imekuwa ikifanya maamuzi bila kuzingatia ripoti za uchunguzi na ndio maana Serikali haikusita kuunda tume ya kuchunguza sababu za kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2012 wakati kulikuwa na tume iliyofanya kazi hiyohiyo mwaka 2010.

Endapo tutaendelea kufikiri kwamba kulegeza njia za ufaulu ndio kuboresha elimu, tutajikuta tuna taifa la watu wenye vyeti vizuri vya elimu lakini wasioweza kufanya kazi inayoshabihiana na alama za ufaulu katika vyeti vyao.

Wataalamu wa elimu waitake Serikali kuacha kufanya mambo yanayohitaji utaalamu kwa ajili ya kujitafutia sifa kisiasa kwa mipango mibovu. Suala la elimu lisichukuliwe kama ajenda ya siasa chafu kwani kwa kufanya hivyo tunaiua elimu yetu.

Ni vema kabla Serikali haijafanya maamuzi ya jambo linaloathiri maisha ya watanzania wengi kama hili la mitihani ikaleta kusudio la kufanya hivyo bungeni ili wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi wajadili na kuishauri Serikali Ipasavyo.

Mwisho kabisa, napenda wananchi wafahamu kwamba kwa mujibu wa kitabu kinachoonyesha viwango vya ufaulu duniani kila mwaka cha “International Qualification”, baada ya Tanzania kutangaza alama mpya za ufaulu, sasa inakuwa nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na alama za chini za ufaulu. Maana yake ni kwamba, tumeshusha ubora na thamani ya elimu yetu.

Hivyo naitaka Serikali kutoa ufafanuzi ni kwanini isifute uamuzi wake wa kubadili viwango vya ufaulu ambayo tayari umeanza kuficha hali hali ya matokeo mabaya katika mitihani. Na badala yake itoe kwa umma na iwasilishe bungeni ripoti za uchunguzi zilizoundwa na kuliwezesha Bunge kufanya maamuzi ya kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,

John Mnyika (Mb) 22/02/2014

MGANGA WA DIAMOND YAMEMKUTA.

$
0
0

Yule mganga anayejitapa kumtengenezea nyota ya mvuto staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ustadh Yahya yamemkuta mazito.



Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa jamaa huyo anahenyeshwa na polisi akiwa mahabusu kufuatia madai ya wizi wa gari aina Toyota Rav 4 ‘milango mitatu’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, gari hilo liliibwa wiki kadhaa maeneo ya Msimbazi-Kariakoo jijini Dar.

HABARI ZA AWALI
Habari za awali zilidai kuwa gari hilo lilifika mikononi mwa Ustadh kutoka kwa mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Mwanahamis ambaye ilisemekana kwamba alikuwa akichukua dawa kwa mganga huyo.

Ilidaiwa kuwa mwanamke huyo naye alihongwa gari hilo na mume wa mtu huku akiwa hajui kuendesha hivyo aliliweka poni kwa Ustadh ambaye alimpa dawa ambayo aliipeleka Kigoma kuwauzia watu wake.

Hata hivyo, ilizidi kudaiwa kwamba mwanamke huyo alichukua dawa za shilingi milioni 3 lakini akashindwa kurudisha fedha hizo na riba waliyokubaliana na mganga huyo.
Ikazidi kudaiwa kuwa, Ustadh alimuongezea dawa nyingine mwanamke huyo hadi kufikia deni la shilingi milioni 6 ndipo akaamua kulichukua gari hilo.

NI UZEMBE?
Ukiacha stori hizo za awali ambazo zilikosa ‘balansi’, kuna habari nyingine kuwa gari hilo mali ya Edric Magayane liliibwa baada ya kuachwa eneo la tukio likiwa ‘sailensi’ bila mtu ndani.
Ilielezwa kwamba aliyekuwa na gari hilo aliingia dukani kununua vitu na alipotoka alichanganyikiwa akidhani gari hilo lilikuwa limevutwa na watu wa ‘breki dauni’ waliokuwa wakivuta magari yaliyoegeshwa hovyo katikati ya jiji.
Habari zinasema kuwa mhusika alikwenda kulitafuta katika ‘yadi’ zinakopelekwa magari yaliyovutwa lakini hakuliona.

POLISI
“Alichokifanya ni kwenda kuripoti polisi ambao walianza kulisaka Dar bila mafanikio.
“Wakati polisi wakiendelea kulisaka kuna mtu akasema amemuona Ustadh akitanua nalo.
“Yule mwenye gari (Magayane) alimtafuta Ustadh hakumpata. Akaelekezwa nyumbani kwake, Kigogo Luhanga, Dar au Urambo, Tabora.
“Jamaa alipatafuta nyumbani kwa Ustadh, Kigogo hadi akafika akiwa na polisi waliovalia kiraia lakini hawakumkuta.

ALITAKA KULIRUDISHA?
“Waliambiwa amesafiri Tabora. Pia walihakikishiwa kwamba kweli Ustadh alikuwa na gari hilo. Jamaa akaambulia namba za simu.
“Alipompigia simu Ustadh alimwambia kama gari limeibwa ana uwezo wa kutumia uganga wake kulirejesha kwa kuwa ni mtaalam wa mambo hayo.
“Ustadh aliomba apewe fedha ili afanye mambo yake gari lirudi. Kweli alitumiwa fedha, lakini akawa anazungusha huku akijiita majina lukuki kama Maimuna na mengine,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

MKOKO WATAFUTIWA MTEJA
Baadaye polisi walifanya uchunguzi na kubaini kuwa, gari hilo lilikuwa likitafutiwa mteja mkoani Tabora lakini ilishindikana kutokana na kukosa ‘dokyumenti’ muhimu.

GARI LAKAMATWA
Habari zilizidi kutiririka kwamba, wakati Ustadh akikatiza na gari hilo Tabora mjini ndipo alipokamatwa na polisi kisha kuwekwa nyuma ya nondo za mahabusu kabla ya kusafirishwa jijini Dar kwa hatua zaidi za kisheria.

MASHITAKA MAWILI
Habari za uhakika zilieleza kuwa, Ustadh alipofikishwa Kituo cha Polisi cha Kati (Central), Dar alifunguliwa mashitaka mawili; wizi wa gari na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.
Baada ya kujikusanyia habari hizo, juzi gazeti hili lilishuhudia polisi wakipekuwa nyumbani kwa Ustadh kisha kumrejesha kituoni kwa ‘difenda’ huku amepigwa pingu mikononi.

MMILIKI ANENA
Akizungumza na gazeti hili juzi, mmiliki wa gari hilo, Magayane alikiri maelezo yote juu ya habari hiyo.
Alipoombwa namba ya jalada la kesi aliitaja kuwa ni MS/RB/827/ 2014-WIZI WA GARI NA KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA ISIYO HALALI.
Jitihada za gazeti hili kuzungumza na Ustadh juu ya msala huo mzito ziligonga mwamba kwa kuwa simu yake ilikuwa haipatikani na bado alikuwa mahabusu huku ikelezwa kwamba soo limemkalia vibaya.

DIAMOND KAINGIA MITINI?
Kwa mujibu wa chanzo kingine, Diamond amekuwa akiombwa kumsaidia jamaa lakini akaingia mitini kwa madai kuwa hapendi kuhusishwa na Ustadh ambaye aliahidi msanii huyo kupata majanga makubwa baada ya kumkimbia na kwenda kwa waganga wengine.
Diamond alipotafutwa juzi kwa njia ya simu hakupatikana huku mmoja wa watu wa timu yake akisema yupo Afrika Kusini ‘Sauzi’ kwa ajili ya kufanya kolabo na D’Banj wa Nigeria.
Credits:Global Publishers 

KINACHOWAPONZA WANAWAKE WENGI NI MAAMUZI DUNI KWENYE MAMBO YA MSINGI..ONA HII

$
0
0
Kinachowaponza Wanawake ni POOR DECISION MAKING IN CRITICAL ISSUES.

Unakuta mtu anajua kabisa ana Boyfriend Levi la Kutupwa,analala mtaroni kila siku,anafikishwa nyumbani hajitambui kafikaje,yeye yupo tu amekazana na Fanta yake..Unachumbiwa na kuolewa na hilihili levi,unasota nalo miaka 2 ya ndoa inakuwa kero...Ulimvumilia kwenye Uchumba coz hamkuwa mnalala pamoja,analewa na kutapika akiwa kwake na wewe uko kwenu..Sasa Mzigo ni wako,mko SAME BED..Anatapika hapo..Harudi home siku 4..Na hata akirudi yuko Njwii,hata 'kazi hawezi kupiga'
Unaenda kulalamika kwa Mchungaji kuhusu Tabia mbaya ya mmeo...YOU KNEW IT..Ukapuuzia na ukakubali kuolewa na JANGA...Mtabaki kusumbua Wachungaji na Wakwe kuwapatanisha wakati mlikuwa na Muda wa kujuana kabla hamjaamua kuishi pamoja
Kipindi cha Uchumba kitumie KUMFAHAMU VIZURI..Sio ukitumie KUMCHUNA,KULA BATA,OFA ZA KITIMOTO,TRIP ZA BAGAMOYO,KUMPIGA MIZINGA YA PERUVIAN HAIR..Ukasahau KEY ISSUES...Mmekaa miaka 6 ana watoto 2 na Wanawake wengine..Analewa na kulala mtaroni..Halafu analeta Posa unasema kuolewa ni Bahati.
Yakikushinda Usitusumbue...Sio kila POSA ni bahati,Posa nyingine ni kichaka tu cha kutua majanga yao...Your Decision TODAY will affect your TOMORROW...Think twice before you say YES to a Problem.

Dully Sykes kuachia wimbo mpya aliomshirikisha Diamond, unaitwa 'Chipolopolo'

$
0
0
Mkali huyo ambaye wiki iliyopita video ya wimbo wake ‘Kabinti Special’ ulifungiwa kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa amekiuka maadili ya kitanzania, amesema kuwa ataachia wimbo huo hivi karibuni.
“Hivi sasa najiandaa kuachia wimbo wangu mpya niliomshirikisha mshikaji wangu Diamond Platinumz.”Alisema  Dully.
“Ni wimbo mzuri ambao naamini mashabiki wataupenda na umetayarishwa hapa hapa studio 4.12 na mimi ndiye producer. Hivi sasa tunajipanga tu kufanya video nzuri na Adam Juma ili wimbo ukitoka uwe na video pia…na itakua hivi karibuni ila ndani ya mwezi wa tatu.”
Chipopolo inafahamika zaidi kuwa ni jina la timu ya taifa ya Zambia, jina linalomaanisha risasi za madini ya copper (copper bullets). Lakini kwa mujibu wa maelezo ya Dully Sykes, wimbo huo hauiuhusu kabisa timu hiyo.
Dully Sykes na Diamond walikutana kwenye wimbo unaoitwa ‘Utamu’ wakiwa na Ommy Dimpoz na ukateka usikivu wa watu wengi. Vipi kuhusu Chipolopolo? 

Lady Jay Dee aeleza sababu za kujifunza Karate, anataka kumkabili nani?

$
0
0

Moja kati ya surprises zilizokuwepo wiki iliyopita ni pamoja na habari ya Lady Jay Dee aka Anaconda kujifua kikomando kuumudu mchezo wa Karate, habari iliyoambatana na picha zikimuonesha akifundishwa mchezo huo tena akiwa ndani ya mavazi rasmi.

Itakuwaje Jide akishakuwa fiti kwenye mitindo hatari ya karate kama Shotokan, Wado-ryu, Shito-ry na Goju-ryu? Na je, anataka kumkabili nani hasa? Haya ni kati ya maswali ambayo wengi tulijiuliza.
“Kwa sababu ninao muda wa ziada, halafu kukaa tu idol bila kufanya kitu saa zingine inaweza kupelekea mawazo yako kufikiria vitu vibaya. Kwa hiyo nikaona sio vibaya nikifanya mazoezi.” Alisema Lady Jay Dee aka Anaconda.
Alipoulizwa kama kuna mtu anataka kupigana naye alisema hakuna mtu ila anajiweka fiti tayari kwa lolote.
“Hapana ni kutaka kujiweka fiti unajua kufanya mazoezi sio kwa ajili ya kutaka kupigana na mtu, ni wewe mwenyewe tu uwe vizuri ili jambo likitokea ujue jinsi ya kuji-protect.” Ameeleza.
Mkali huyo wa Joto Hasira amedai kuwa ana mwalimu mzuri na kwamba yeye pia ni mwanafunzi mwenye bidii.

ASKOFU BILIONEA ATIKISA BONGO.

$
0
0
ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni
alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi  kwa kuwa na magari ya kifahari na ndege aina ya helikopta ‘chopa’ iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga kulinda usalama wake, Uwazi lina ushuhuda wa kutosha.

Katika mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara, mwandishi wetu alishuhudia msafara wa Geordavie ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.

Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.

Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.

Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.

“Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii ni mara yangu ya kwanza kuona,” alisema muumini mmoja ambaye hakupenda kutajwa gazetini.

Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha.

“Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?” alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.

Pia, waumini wengine walilalamikia ugumu wanaoupata wanapotaka  kumuona mtumishi huyo wa Mungu kutokana na ulinzi mkali anaopewa.

“Kila mtu alitamani kumuona mtumishi wa Mungu lakini haikuwezekana kutokana na ulinzi wake kuwa mkali, utajiri wake hakuna mfano, hata kule nyumbani kwake Arusha, anaishi kama Mfalme Daud,” alisema Fred Mushi.

Gazeti hili lilimsaka Askofu na Nabii Geordavie kwa lengo la kutaka kujua sababu ya kuwa na ulinzi mkali na kutumia magari ya kifahari ikiwemo chopa katika mikutano anayoifanya lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Credits:Global Publishers 

MREMBO AFIA GESTI ARUSHA.

$
0
0
Stori: Joseph Ngilisho, Arusha
MREMBO mmoja ambaye alihu-dumu kwenye nyumba ya kulala wageni na baa (jina tunalo) iliyopo Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha,

Blandina Michael (33) amekutwa amekufa kwenye moja ya vyumba vya nyumba hiyo huku chanzo cha tukio hilo kikihusishwa na vitendo vya ushirikiana.

Taarifa za awali zilimtuhumu mmiliki wa nyumba ya wageni moja ambaye pia anajihusisha na biashara za madini (jina tunalo) kwamba alimtoa kafara mhudumu huyo. Ilidaiwa kuwa, kila mwaka mtu mmoja katika biashara zake hupoteza maisha ghafla.

Hata hivyo, mfanyabiashara huyo alipoongea na Uwazi juzikati alikanusha vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa yeye ni muumini mzuri wa imani yake.

‘’Hao watu wanapotosha sana, unajua kuna mwaka mwanaume mmoja alikufa ghafla kwenye nyumba yangu ya kulala wageni, alikuja na mpenzi wake ila alimeza Viagra ambazo hata polisi walizikuta mezani.
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema.

Kifo cha Blandina kilitokea ndani ya chumba huku mtu mmoja anayedaiwa kuwa mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Timo, mkazi wa eneo hilo akihojiwa na polisi.

Marehemu Blandina ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga, anaelezwa na bosi wake huyo kwamba alikuwa kama mtoto wa familia yake kwa vile alimwamini sana. Alifanya kazi hapo kwa miaka 8 na hakuwa na tatilo la kiafya.

Bosi huyo alisema mwili wa marehemu uligundulika baada ya mfanyakazi mwenzake wa kiume kumpigia simu saa 2 asubuhi ambapo simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa ndipo alipoamua kwenda kumgongea katika chumba hicho.

Alisema baada ya kufika alishangaa kukuta mlango wa chumba chake uko wazi na alipochungulia alibaini kwamba Blandina alikuwa amefariki dunia.

Hata hivyo, polisi baada ya kufika na kuufanyia uchunguzi wa awali mwili huo hawakugundua kuwepo kwa jeraha lolote linaloashiria kuuawa, ingawa mwili huo ulipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

KAJALI ALISHWA SUMU, AKIMBIZWA HOSPITALINI.

$
0
0
Mwanadada mwigizaji Kajala juzi alikumbwa na dhahama ya kusikitisha baada ya kulishwa kitu
kinachosadikiwa kuwa ni sumu alipokuwa kwenye show ya msanii wa muziki kizazi kipya Izzo Business.

Akielezea Zaidi kajala alisema…

‘’Jana (juzi) nilivyokuwa kwenye shoo ya izzo ghafla nikaanza kuumwa nikapelekwa home halafu nikaenda hospitali. Nilivyo pimwa nikakutwa nimekunywa kitu chenye sumu lakini namshukuru mungu naendelea vizuri asante mungu kwa kila jambo...

Hali ya kajala ni nzuri na ameruhusiwa kutoka hospitalini sasa. Pole sana Kajala. 

HAYA NDIYO MADHARA YATOKANAYO NA NGUO ZA KUBANA (SKIN TIGHT)

$
0
0
KADIRI siku zinavyokwenda kumekuwapo na ugunduzi wa vitu mbalimbali vinavyochangia kuleta mabadiliko katika jamii.


Mabadiliko hayo yanaweza kuwa hasi au chanya kutegemea na aina ya  bidhaa iliyogunduliwa na matumizi yake.

Zipo bidhaa zinazoonekana kuwa na matokeo ya haraka na mazuri baada ya kutumika, lakini wakati huo huo kuwa na madhara kiafya kwa mtumiaji.
Nchi nyingi zinazoendelea hasa zilizopo barani Afrika ikiwamo Tanzania zimekuwa ndizo waathirika wakubwa wa bidhaa zinaotajwa kuwa na madhara huku vijana wakiwa ndiyo kundi kubwa linaloathirika. Sababu za kundi hilo kuathirika zaidi ni kutaka kwenda na wakati kwa kujaribu kutumia kila bidhaa zinazotoka nje ya nchi bila kujua madhara yake.
Miongoni mwa bidhaa hizo ni nguo za ndani zilizoundwa maalumu kwa ajili ya kupunguza unene, pia kutengeneza umbile la mvaaji katika mwonekano wenye mvuto aupendao. Nguo hizo zimetengenezwa kwa mtindo wa mbano, (Skin tight)ambapo ikivaliwa hubana eneo la tumboni hadi kwenye mapaja na hufanya kazi ya kupunguza unene, zikiufanya mwili kuwa mwembamba kulingana na nguo husika ilivyo.
Licha ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na kusaidia kwa kiasi kikubwa watu wengi kupunguza miili yao, utafiti wa kisayansi unaonyesha kuwa nguo hizo za ndani huchangia kwa kiwango kikubwa uwezekano wa mvaaji kupata matatizo ya kiafya.
Utafiti uliofanywa na wataalamu mbalimbali wa nchini Uingereza, unaonyesha kuwa uvaaji wa nguo hizo unaweza kumfanya mvaaji kupata maradhi ya mgongo, saratani na kiwango kikubwa cha asidi mwilini.
Mmoja wa wataalamu wa afya katika Hospitali ya The London Clinic, Dk Johnson Wilson, anasema kubana kwa nguo hizo katika eneo la tumbo huzuia mzunguko wa asidi inayozalishwa ndani ya mwili na kuisababisha kupanda juu, badala ya kushuka chini.
Anasema kuwa hali hiyo inatokana na msukomo unaotokea kwenye tumbo, hivyo kusababisha mlundikano wa asidi ndani ya mwili ambayo hupaswa kutoka baada ya kuzalishwa.
“Nguo hii inapovaliwa inatenganisha  eneo la kifuani na tumbo, hivyo asidi inayozalishwa inashindwa kushuka chini na matokeo yake inashia kwenya usawa wa  matiti na kurudi kwenye mrija unaopitisha chakula,”anasema DkWilson.
Kuhusu hatari ya saratani, Dk Wilson anasema kuwa kulundikana kwa asidi katika mrija wa chakula, kunamweka mhusika katika hatari ya kupata saratani ya koo na kinywa.
Anasema kwamba licha ya kuwa siyo watu wengi walioathirika na uvaaji wa nguo hizo, lakini matokea yake huonekana baada ya muda mrefu kutokana muda ambao mhusika atavaa nguo hizo.
“Hatari ipo zaidi kwa wanaovaa nguo hizi mara kwa mara, madhara yake hayawezi kuonekana kwa haraka zaidi, lakini kiafya kuna hatari ya kutengeneza saratani ya koo kutokana na kuzuia asidi na kusababishia irudi na kulundikana kwenye mrija unaosafirisha chakula,”anaonya.
Pamoja na hatari hiyo uvaaji wa nguo hizoi pia unachangia kusababisha ugonjwa wa ngozi unaotokana na mwili kubanwa kupita kiasi, hivyo hewa kushindwa kupita.
Dk Wilson anafafanua kuwa ikifikia hatua hiyo, kuna uwezekano wa kutengeneza mazingira ya bakteria na fangasi kujificha kwenye mwili hivyo kusababisha mvaaji kupata maradhi ya ngozi yaliyo magumu kutibika.
Mtaalamu wa ngozi Dk Sam Bunting anasema, kubanwa kwa ngozi pamoja na joto linalosababishwa na msuguano, vinachangia kuleta madhara makubwa katika mwili wa binadamu.
“Hali hii inasababisha ugonjwa unaofahamika kwa jina la kitaalamu kama Intertirgo, ambao huwatokea watu wanaovaa nguo maalumu za kubana kwa ajili ya kutengeneza maumbile,”anasema.
Nguo hizo pia huchangia kuifanya misuli ya tumbo kuwa dhaifu, kutokana na kubanwa muda mwingi, hata inapoachwa huru inashindwa kuwa na nguvu yake ya kawaida.
“Kwa asili misuli ya tumbo haina nguvu na unapoibana kwa muda mrefu unaisababishia kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi, hivyo hulegea na kuwa  dhaifu zaidi hata inapofunguliwa au kutolewa nguo inayobana,”anasema.
Kwa upande mwingine, mtaalamu wa misuli Dk Robert Shanks anasema kuwa nguo hizo zinachangia pia kusababisha maumivu ya mgongo kwa mvaaji. Anasema nguo hiyo inapovaliwa, kunakuwapo na ugumu kwa viungo vya mgongo kujongea kwa urahisi, hivyo kusababisha maumivu ya mgongo mara kwa mara.
“Viungo na mifupa iliyopo kwenye mgongo inapaswa kujongea, lakini kuibana kupita kiasi kutasababisha kushindikana kwa hali hiyo hivyo mvaaji lazima atakumbana na maumivu ya mgongo mara kwa mara”
Pamoja na madhara hayo, nguo hizi pia huweza kusababisha kizuizi katika mzunguko wa damu kwani mishipa inayotakiwa kufanyakazi hiyo inashindwa, kutokana na maeneo ya tumbo hadi kwenye nyonga yanakuwa yamebanwa.
“Ni vigumu mzunguko wa damu kufanyika vizuri katika maeneo yaliyobanwa kupita kiasi; ni wazi kuwa nguo hizi siyo rafiki, huifanya damu isizunguke inavyopaswa,”anasema Dk Shanks na kuongeza:
“Ikifikia hatua hiyo, kuna dalili mvaaji kuweza kupata maimivu ya miguu kwa kuwa mishipa ya damu iliyopo katika maeneo hayo inashindwa kufanya kazi yake vizuri.”
Kwa upande wake mtaalamu wa masuala ya ngozi nchini Tanzania, Dk Isack Maro, anasema kuwa madhara yanayotokana na uvaaji huo siyo makubwa ikilinganishwa na ripoti ya utafiti unavyoeleza.
“Inawezekana kukawapo uwezekeno wa kupata maradhi ya ngozi kutokana na mwili kubanwa kwa muda mrefu, hivyo jasho kushindwa kutoka na kutengeneza mazingira ya fangasi,”anasema Dk Maro na kuongeza:
“Madhara yapo, lakini siyo kwa ukubwa huo. Inawezekana kuwakumba watu wachache mno kati ya wengi, lakini sidhani kama yanaweza kuwa kwa ukubwa huo.” 

Louis akanusha taarifa za kujiunga na klabu ya Tottenham.

$
0
0
Louis van Gaal amezikana taarifa hizo baada ya kuhusishwa nazo kwa muda wa juma moja lililopita ambapo baadhi ya vyombo vya habari vya nchini Uingereza vilidai kwamba huenda kocha huyo mwenye umri wa miaka 62,angejiunga na Spurs mara baada ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambazo zitafanyika nchini Brazil.
Van Gaal amesema ana hakika uzushi huo wa vyombo vya habari huenda umeibuka kutokana na mkataba wake wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kutarajia kufikia kikomo mara baada ya fainali za kombe la dunia,lakini hakusita kukiri wazi kwamba suala hilo lina ukweli.
Amesema pamoja na kutoitarajia kuendelea kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi bado haijalishi kama atajiunga na klabu ya Spurs,kutokana na mipango yake aliyojiwekea ya kutaka kuishi nchini Ureno ambapo ndipo alipowekeza maisha yake kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo Louis van Gaal amesema angependa mara baada ya kuachana na timu ya taifa ya Uholanzi akarejea tena kufanya kazi ya kufundisha moja ya klabu kubwa nchini Uingereza,lakini hakuwa tayari kuitaja licha ya kutania mbele ya waandishi wa habari kwa kusema huenda ikawa Tottenham Hotspurs ama la.
Louis van Gaal kabla hajakabidhiwa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi  mwaka 2012 aliwahi kuwa meneja wa klabu kubwa kama FC Barcelona pamoja na FC Bayern Munich huku klabu za nyumbani kwao Uholanzi alizobahatika kuzifundisha ni AZ Alkamar pamoja na Ajax Amsterdam.
Kama itakumbukwa vyema uongozi wa Tottenham Hotspurs umekua ukihangaika kumsaka mbadala wa mkuu wa benchi la Ufundi tangu walipomtimua meneja kutoka nchini Ureno Andre-Villas Boas japo kwa sasa kitengo hicho kimekuwa kikiongozwa na Tim Sherwood aliyesainishwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

MCHUNGAJI FEKI ALIYETABIRI KUA MWISHO WA DUNIA NI MWAKA 2000 AFARIKI DUNIA.

$
0
0
kiongozi wa Kanisa la World Message Last Warning ambaye alitabiri kwamba mwaka 2000 utakuwa mwisho wa dunia, Wilson Bushara (53) amefariki dunia.

Bushara ambaye alivuta vyombo vingi vya habari alipotabiri na kusisitiza kwamba mwisho wa dunia utakuwa Juni 30 mwaka 1999 na kusashawishi waumini wake kuuza mali zao na kununua nafasi zao mbinguni alifariki asubuhi ya jana.
Alitabiri na kusisitiza kwamba dunia itafikia mwisho wake kabla ya kuingia kwa milenia mpya, ambayo ilikuwa ni mwaka 2000.


Hata baada ya tarehe hiyo aliyoitaja kupita bila tukio hilo kutokea, Bushara alikimbilia mafichoni baada ya polisi kuvamia kambi yake ya maombi ya Bukoto iliyokuwa huko kwenye Wilaya ya Luweero Jimbo la Nakaseke Septemba 18, 1999.


Bushara anatambulika kuwa ana ushirikiano na kiongoni mwingine wa kundi la kidini, Joseph Kibwetere ambaye aliwashawishi waumini wake zaidi ya 1000 kujichoma moto kanisani Machi 17, 1999.


Hata hivyo aliamua kukataa kuwa na ushirikiano na Kibwetere pamoja na kuwa na ushahidi wa picha walizopiga kwenye matukio kadhaa wakiwa pamoja.


Bushera pamoja na baadhi ya waumini wake ambao wengi walikuwa wakifanya kazi za kuuza maziwa na uhudumu kwenye hoteli wote walikimbilia wilayani Busia ambapo walijificha baada ya kusikia taarifa kwamba polisi walikuwa wakitaka kuwakamata.


Alioa wake tisa aliokuwa akiishi nao kwa pamoja, mmoja kati yao akiwa binti wa miaka 15. Miaka 10 baadaye, yaani mwaka 2011 Bushara aliibuka na kutabiri kwamba dunia inaelekea kufikia mwisho wake siku za karibuni na kuanza kugawa kadi za mwaliko kwa waumini wake, kwa ajili ya tafrija maalumu ya "karamu ya mwisho" ambazo kila moja iliuzwa kwa Sh23,000 za Uganda.


Aliwaeleza wafuasi wake kwamba ishara za mwisho huo wa dunia ziko wazi ikiwemo miale mikali ya radi na milipuko ya volcano wanayoishuhudia kwa mwaka huo ndiyo uthibitisho kwamba dunia imefikia mwisho. 


Kwa kusisitiza, aliwahakikishia kwamba wale watakaokuwa wamenunua kadi hizo ndio watakaopata fursa ya 'kunyakuliwa' moja kwa moja kwenda mbinguni na wale ambao hawatakuwa wamezipata, wataishia kwenye moto wa jehanamu.

Kwa wakati huu, Bushara alikuwa makini akikataa kutaja tarehe rasmi ya mwisho huo wa dunia aliokuwa akiutabiri.


Bushara amefariki huku akikabiliwa na mashtaka kadhaa mahakamani, ikiwemo kufunguwa kanisa lake ambalo lilipigwa marufuku.

Mei mwaka jana alishtakiwa kwa ulaghai na kuitisha mkusanyiko usiokuwa halali kisheria, kisha kushikiliwa kwenye gereza la Luzira na hatimaye kuachiwa.



CHANZ:MWANANCHI
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live