
Hii inatokana na jinsi ilivyo na wafuasi wengi ‘active member takribani bilioni 1.9’, na hivyo mengi yanazungumziwa huko na bahati mbaya mengine huwekwa bila kuthibishwa.
Kwa kuzingatia hayo, mwimbaji mkongwe wa Tanzania, Stara Thomas ameamua kukaa chini na kuandika wimbo kuhusu mtandao huo wa kijamii ‘Facebook’.
Mwimbaji huyo wa ‘Wasiwasi wa Mapenzi’ ameweka wazi mpango huo wakati akizungumza katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100. 5 Times Fm, baada ya msikilizaji mmoja kutaka kufahamu kama kweli amehama VOA band ya Linex.
“Nadhani mara nyingi mtu anapokuwa anaongea jambo…tumekuwa na tatizo la Facebook ndani ya ubongo. Facebook inadaka halafu inajibu hapo hapo.” Amesema Stara Thomas.
“Na kuna wimbo naandika kuhusu Facebook, really I’m telling you. Na Times Fm itakuwa ya kwanza kuucheza.” Ameongeza Stara, kisha akalijibu swali la msikilizaji.
“Kwenye VOA band, sio kana kwamba ni bendi ambayo tunapiga kila siku. Yeye ana project zake, na mimi naproject zangu lakini pale tunapotaka kufanya kwa pamoja tunafanya kwa pamoja, lakini sio kwamba ni bendi tunayopiga kila siku.”
Stara Thomas alisisitiza kuwa bado hajatoka VOA band.