↧
Mama Yake Rambo Mwenye Miaka 92 Baada Ya Upasuaji Wa Kubadili Sura.
↧
Hiki ndicho kitu kinachofuata kutoka kwa Diamond Platnumz.

Mwaka jana Diamond alikaa China zaidi ya wiki nzima kabla ya kufanya show ambapo moja ya mipango iliyomuweka ni kufanya maandalizi ya nguo hizo.
Muda wa kuzitoa unaonekana umekaribia kutokana na teaser aliyoitoa kupitia account zake za mitandao ya kijamii kuhusu hizo nguo.
↧
↧
Yajue hapa mambo yanahusiana na February 11 pamoja na mengine.

Siku kama ya leo miaka 32 iliyopita alizaliwa Kelly Rowland ambaye aliwahi kuja Tanzania na kufika hadi Uwanja wa fisi.
Kelly alikuja kwa ajili ya kampeni ya Staying Alive Foundation ambapo alikuwa balozi wa MTV AIDS Awareness.
![kelly-r5bc]()
Leo pia ni siku ambayo hayati Nelson Mandela aliachiwa huru kutoka kwenye gereza baada ya kuwa mfungwa hadi 11 February 1990.


Unaambiwa akiwa anatoka kwenye gerezani vyombo vya habari kutoka sehemu mbalimbali za dunia walizunguka kuihabarisha dunia kwa kilichokuwa kinaendelea.

Ndani ya eneo hilo utakutana na makao makuu ya Google,Facebook,eBay,Adobe,Apple,Yahoo,HP,Intel,Mozilla Foundation,Linkedln,Twitter na mengine mengi.
↧
STEVE NYERERE"WASANII WENGI WA BONGO MOVIES HAWAJITAMBUI"

Mwenyekiti wa kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mangere ‘Steve Nyerere’ amesema wasanii wengi wa filamu hawajitambui, mbumbumbu na wabinafsi katika kila kitu, jambo linaloleta ugumu katika harakati zao za kujikwamua.
Steve Nyerere ambaye pia ni mwigizaji na mchekeshaji, amesema wasanii wengi wanakosa umoja wa kudai haki zao kutokana na uelewa mdogo walionao huku wengine wakitazama maendeleo yao binafsi.
“Wasanii tumekuwa mbumbumbu wa kila kitu, tumeyumba kwa kuuza na kuibiwa kazi zetu na maharamia. Dada zetu nao wanafanya Bongo Movie ni sehemu ya kufanyia ukahaba.
Pia amesema yeye kama kiongozi anapigania haki za wasanii zisisahaulike katika mchakato wa katiba mpya ili waweze kupata nafuu ya kazi zao.
Source, Mwanaspoti
↧
Young Dee kumfungulia mashitaka mtu anayetumia jina lake Facebook kufanya utapeli.

Rapper anaewakilisha kundi la Mtu Chee, Young Dee, amedai kuwa ingawa hayuko kabisa facebook, kuna mtu ambaye amekuwa akitumia jina lake kufanya utapeli licha ya kuzungumzia mara kwa mara kuhusu mtu huyo kwenye vyombo vya habari.
Rapper huyo wa ‘Kijukuu’, ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa japokuwa alitangaza zawadi kwa mtu atakayefanikisha zoezi la kumpata mtu huyo bado hajafanikisha na kwamba mtu huyo anaendelea hadi leo.
Amesema aliwahi kwenda polisi kufungua mashitata dhidi ya mtu huyo akiwa na utambulisho wa BASATA kuwa yeye ndiye ‘Young Dee’, lakini polisi walidai ampeleke mtu ambaye ametapeliwa ndipo aweze kufungua kesi hiyo.
Tayari Young Dee ameshajipanga kwa ajili ya kuupeleka ushahidi utakaofanikisha zoezi la kumpandisha kizimbani tapeli anayetumia jina lake kwenye Facebook.
“Bado naendelea na zoezi langu, lakini sasa hivi nachokitafuta…kuna mtu wa sheria amenishauri kuna jinsi ambavyo hiyo kesi tunaweza kuifungua ikamake sense. Kwa hiyo ndio niko nae naconfirm naye, lakini bado tunakusanya ushahidi, kuna mtu mmoja nimempata ambaye ameshatapeliwa, natafuta mwiningine. Kwa hiyo tukishapata ushahidi wa kutosha tunaweza kum-sue. Young Dee ameiambia tovuti ya Times Fm.
Kama uko facebook na unachat na Young Dee, sanuka, jamaa hayuko facebook kabisa!
↧
↧
Linex akanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi na Agnes Masogange, 'Sina haraka ya kuwa na mpenzi'

Kupitia akaunti yake ya Facebook, mkali huyo wa ‘Kimugina’ ameonesha kusikitishwa na habari iliyoandikwa na tovuti moja kuwa yeye na Agnes wako kwenye mapenzi mazito.
“ni kweli watu wa blog mnapush sana kazi zetu but nimesikitishwa na habari hii iliyoandikwa na blog kadhaa mtasababisha tutashindwa ata kukaa na Dada zetu au marafiki zetu Uliza b4 Hujaandika ujinga am single na sina haraka ya kua na mpenzi.” Ameandika kwenye Facebook.
Wikendi hii, Linex alipost picha mbili Instagram akiwa na mrembo huyo, moja wakiwa wamepoz ufukweni, na nyingine akiwa naye katika mechi ya mpira wa kikapu kati ya timu za madirector wa video za muziki Tanzania, Adam Juma na Karaban.
↧
Vigogo sita CCM waitwa Kamati ya Maadili.

Habari ambazo zililifikia gazeti hili jana zinawataja vigogo hao kuwa ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Wengine ni Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
“Wote wamepelekewa barua za wito wa kufika mbele ya Kamati ya Maadili inayoongozwa na Mzee Mangula (Philip, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara), ambayo itakutana mjini Dodoma, Februari 14 (kesho kutwa) ,” kilisema chanzo chetu cha habari kutoka Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam na kuongeza:
“Barua hizo zimesainiwa na Mzee Kinana (Abdulrahman, Katibu Mkuu wa CCM) mwenyewe na tayari zimeanza kusambazwa leo (jana) mchana.”
Kamati hiyo ndogo ya maadili, inaundwa na Mangula, Kinana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Shamsi Vuai Nahodha, Dk Maua Daftari na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye jana alithibitisha kuwapo kwa Kikao cha Kamati ya Maadili Februari 14 pamoja na kuitwa kwa baadhi ya wanachama kwa ajili ya kuhojiwa.
Hata hivyo, hakuwa tayari kutaja majina yao wala idadi ya walioitwa... “Wewe fahamu tu kwamba kikao hicho kitafanyika tarehe hiyo uliyoitaja, lakini masuala ya majina na idadi ya walioitwa yatajulikana kwenye kikao, mimi sina kwa sasa,” alisema Nnauye.
Katika siku za karibuni kumekuwa na vita ya maneno baina ya makada wa chama hicho, wakituhumiana kutangaza mapema kugombea urais kabla ya ruhusa rasmi ya chama.
Kauli za walioitwa
Jana, gazeti hili lilizungumza na baadhi ya walioitwa na wengi wao walisema hawakuwa wamepokea barua za wito huo.
Sumaye kwa upande wake alisema: “Kwa sasa niko Mwanza na sijapata barua yoyote ya kuitwa katika kikao chochote cha chama.”
Chanzo:Mwananchi.
↧
Vivian-namuheshimu Jaguar, mtuache.
Mwanamuziki Vivian Wambui, amewaomba wapenzi wa muziki kumheshimu na kuacha kumuhusisha na tuhuma za uhusiano wa kimapenzi na Jaguar.
Amesema anaweza kuwa na uhusiano na mtu yeyote anayempenda lakini siyo kwa watu anaowaheshimu kama Jaguar.
“Naomba mniheshimu, Jaguar ni kama kaka yangu jinsi tunavyoheshimiana na anavyonishauri kwa nia njema, sioni sababu ya kila kukicha kusema ni mpenzi wangu mnanidhalilisha,” alisema Vivian, alipohojiwa kwa njia ya simu na mtandao wa Bigeye.
Vivian alifafanua kuwa jambo la maana kwao ni kutathmini muziki wanaokufanya badala ya kuanzisha maneno ya ajabu ambayo yanaishushia hadhi tasnia ya muziki, kwa kuonekana ni kama kituo au kazi ya kuendeshea uhuni.
↧
Irene Uwoya:Wasanii bado hatujaweza kuthamini muda wetu.

Akizungumza katika mafunzo maalumu ya wasanii na wafanyakazi wa Kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa filamu 5 Effect, Uwoya alisema kinachokwamisha tasnia ya filamu kufika katika nafasi za juu kimafanikio ni kutokujali muda.
“Tatizo kubwa ni kutokuthamini muda, unakuta mmekubaliana kwamba mkutane saa nane mchana katika eneo la kutengenezea filamu (Location), unafika pale mtu unayetakiwa kushirikiana naye katika (Scene) kile kipande hajafika, anafika saa kumi jioni, kazi inachelewa kuanza na muda unapotea,” alisema Uwoya.
Alisisitiza kwamba ikiwa tasnia hiyo itajali muda ipasavyo, inaweza kupiga hatua kubwa kwa mwaka huu, hasa ukizingatia sanaa imerasimishwa na Serikali hivyo ni kazi inayotambulika kwa sasa.
“Serikali yetu imerasimisha sanaa, kwa sasa ni kazi kama ya ofisini, inatakiwa sisi wasanii tulitambue hili na kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anatekeleza majukumu yake ipasavyo.Pia mtu wa kamera naye lazima ajue script (muswada) inasema nini.
Vivyo hivyo kwa upande wa masoko na wasambazaji tunahitaji watu wenye uelewa na elimu kuhusu kazi hizi ili tusonge mbele,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa viongozi ni kama dira, hivyo wanapaswa kutoa mwongozo mzuri kwa wasanii na kusimamia kampuni vema ili kujikwamua na wizi wa kazi za sanaa nchini.
“Lazima tuondoe dhana kuwa bila watu wa jamii ya Asia hakuna usambazaji,” anasema.
↧
↧
Wanasayansi wa kampuni ya Google:Wabuni magari yasiyotumia dereva.

Wanasayansi wa Google wanaosimamia teknolojia hiyo mpya, wanaamini kwamba madereva wanafanya makosa mengi wawapo barabarani, yakiwepo ya kizembe ama bahati mbaya na ndiyo yanakuwa chanzo cha ajali mbaya barabarani.
Wakati teknolojia ya kompyuta ilipogundulika, wanasayansi walisema wamegundua mbinu ya kufuta makosa ya kibinadamu katika shughuli za hesabu.
Waliamini kuwa kila hesabu 500 afanyazo mtu ambaye ni mtaalamu wa fani hiyo, lazima kuwepo na makosa yasiyopungua mawili. Lakini baada ya kugundua kompyuta, maelfu kwa maelfu ya hesabu yanaweza kufanyika bila makosa.
Makosa hayo ya kibinadamu yanayoweza kufanywa na mtu bila kukusudia, ndiyo yanayoaminika kuweza kufanywa na dereva yeyote akiwa barabarani.
Magari hayo yako je?
Mtaalamu wa kompyuta katika Chuo Kikuu cha Stanford, Profesa Sebastian Thrun, anayesimamia, teknolojia hiyo akisaidiana na mhandisi wa kampuni ya Google, Chris Urmson, wanasema teknolojia hiyo itasaidia kuepusha ajali, foleni na pia kupunguza kiwango cha mafuta yanayopotea kutokana na uendeshaji usiofaa.
Mhandisi Urmson anasema magari hayo hayatakuwa na tofauti kwa kiasi kikubwa na mwonekano au miundo ya magari yaliyopo sasa. Kama haitoshi yana chaguo la ama liendeshwe kwa kompyuta ama na dereva.
Mwonekano wake
Kimwonekano, magari hayo anayaelezea yatatofautiana na mengine, kwa kuwa na kifaa maalumu juu ambacho kinasaidia mawasiliano na kutambua maeneo.
Anasema kwenye mfumo wa kompyuta zitatumika programu mbalimbali kama vile ya 3D, ambayo itasaidia kuliongoza gari kulingana na ramani ya eneo.
“Hii ina maana kwamba magari yote yatakuwa yanatumia ramani ambayo lazima iingizwe kwenye mfumo wake ili itambue barabara itakazopita ili kufika aneo ambalo mhusika ama wahusika wanataka” anasema.
↧
RAY AVUNJA UKIMYA"NIMEMISS .............STEJINI"
mrefu sababu hata yeye ameimiss mic na jukwaa, “Naimiss steji vibaya mno!!!!” ameandika Ray C katika Instagram yake.
“Likizo ya mwaka mzima alhamdullilah!!!!Mungu ni mwema sana!!!!!!!Asante kwa afya baba yangu!!!!!muda si mrefu ntarudi Kazini na uhakika mashabiki wangu wapenzi mmenimiss sana!Kila kitu tayari kimeshapikwa bado tu kuwaambia lini tu but niombeeni heri wapenzi wangu najua sana mmeimiss sauti ya Ray C All over the world!!!!jinsi ninavyowapenda na jinsi mlivyoniombea zawadi Kama kumi hivi nimewaandalia!!!mtashauaje sasa!!kama nawaona vile!!!!!!Bila nyie hakuna Ray C!!!!!!!Thank you so very much guys!!!!!!My fans!My everything!!Nawapenda mno!!!!”.
Mwishoni mwa mwaka jana Ray C alisema ameanza kuingia studio na tayari amemaliza kurecord album yake mpya, hivyo naamini comeback yake itakata kiu ya mashabiki wake.
↧
UKWELI KUHUSU P-SQUARE.
Nyota toka nchini Nigeria, Peter Okoye wa kundi la P Square hivi kkaribuni kwenye mahojiano yake amefunguka kwa kusema kwamba kamwe kundi lao halitokuja kugawanyika kwa mmoja wao kufanya kazi peke yake (solo) huku pia akieleza vile wanavyogawana kile wakipatacho.
Peter alisema: Haiwezekani! Tuko na furaha na tunagawana 50-50 kwa kila kitu. Hata kama tunafanya album sasa nami nikawa nahusika kwa kazi zote, Paul bado ataendelea kupata asilimia 50 yake. Wakati mwengine naweza andika wimbo na nikaimba vesi ya kwanza, sauti ya Paul inaweza kuwa haiko sawa kwenye vesi ya pili ila hutoweza kuona tofauti. Mtu pekee labda mwenye uwezo wa kutufanya tuwe solo ni mama yetu na ni kitu ambacho hakito wezekani.
Peter alisema: Haiwezekani! Tuko na furaha na tunagawana 50-50 kwa kila kitu. Hata kama tunafanya album sasa nami nikawa nahusika kwa kazi zote, Paul bado ataendelea kupata asilimia 50 yake. Wakati mwengine naweza andika wimbo na nikaimba vesi ya kwanza, sauti ya Paul inaweza kuwa haiko sawa kwenye vesi ya pili ila hutoweza kuona tofauti. Mtu pekee labda mwenye uwezo wa kutufanya tuwe solo ni mama yetu na ni kitu ambacho hakito wezekani.
↧
Shilole Afunguka, Ataja Mapesa Aliyomwaga Kufanya Video Ya Chuna Buzi.

Shishi Baby, maarufu zaidi kama Shilole, ameweka wazi kuwa amewekeza kiasi cha shilingi milioni 8 katika kutengeneza video ya ngoma yake mpya
inayokwenda kwa jina Chuna Buzi kwaajili ya kutoa kitu kizuri ambacho mashabiki wake watavutiwa nacho.Shilole amesema kuwa, katika video hii kutokana na malalamiko, maoni na maombi mengi ya mashabiki, kutaonekana ‘viuno’ vya hatari kama vile ambavyo mashabiki wake wanapenda.
Msanii huyu ameweka wazi kuwa, nusu ya kitita hiki cha pesa amemkabidhi muongoza video Nisher, na nusu nyingine ameipeleka katika maswala ya kupendeza na location za video.
Msanii huyu ameahidi mashabiki wake kuwa mwisho wa mwezi huu kazi hii itakuwa tayari kwaajili ya mashabiki wake kuburudika.
↧
↧
Kanisa Lingine La Ajabu Laibuka, Sheria na Misingi Yake Yashtua Wengi.Watu Wanasali wakiwa Uchi wa Mnyama.

Kanisa lenye taratibu za ajabu za kuabudu limeibuka huko Virginia Marekani, ambapo waamini wake wameruhusiwa kuhudhuria ibada wakiwa uchi
kutokana na madai kuwa Waamini wa makanisa mengi sikuhizi wamekuwa wakishindana na kupeana hadhi kulingana na aina ya mavazi wanayoingia nayo katika ibada.Kiongozi wa kanisa hili (White Tail Chapel), Pastor Allen Parker amesema kuwa ameamua kuwaruhusu waumini wa kanisa lake kuingia kanisani bila nguo ili kuweka usawa kati yao mbali na mavazi na vitu vya kidunia.
Pastor Allen pia amekuwa akisimamia mafundisho yake haya kwa kuzingatia hadithi za Maandiko Zikiwepo za Adam na Hawa kukaa uchi katika bustani ya Eden bila aibu, Kuzaliwa bila kuwa na nguo pamoja na mambo mengine yanayofanana na hayo.![article-0-1B61B0F700000578-550_634x352]()
![article-0-1B61B1AD00000578-28_634x358]()
![article-0-1B61B1C200000578-837_634x356]()
![article-0-1B61B1CB00000578-444_634x356]()
![article-0-1B61B1F500000578-922_634x352]()





Hata hivyo, Swala la kuingia katika Kanisa hili bila nguo limefanywa kuwa la hiyari hivyo kwa wale wanaojisikia kuingia wakiwa wamevaa nguo huendelea kufanya hivyo kama kawaida.
↧
AGNES MASOGANGE AFUNGUKA KUHUSU KUTONGOZWA NA WANAUME WAKWARE.

Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Masogange alisema tangu atoke Sauz aliponaswa kwa msala wa kusafirisha malighafi haramu, wanaume wakware wamekuwa wakimsaka kama fisi aliyeona mfupa kitu ambacho hakubaliani nacho.“Sitaki kutongozwa kabisa, waniache. Kinachonikera zaidi wanaonitongoza wengi wanatambua kabisa nina mchumba wangu (Evance), watu wengine sijui wapoje!” alisema Masogange.
↧
DIVA LOVENESS NDANI YA PENZI ZITO LA CRAZY GK WA EAST COAST.

Diva akipenda, ulimwengu wote utajua. Hajui kuficha siri na haoni shida kuweka wazi hisia zake wote wajue. Na kwakuwa Valentine’s Day ndio hii,
mtangazaji huyo wa redio ambaye kwa sasa ana uhusiano na rapper wa East Coast Team, King Crazy GK, amewaonesha followers wake wa Instagram kuwa kwa sasa si Diva the Bawse tu, bali ni ‘Diva the Queen’.
Diva amepost picha inayomuonesha akipigwa busu shavuni na Mfalme wake na kuandika: Me and My GK….. closer .. kisses from US.”
↧
WEMA: PIGA, UA LAZIMA DIAMOND ANIOE.

Licha ya mama yake mzazi kupinga kwa nguvu zote, staa wa filamu nchini na mtangazaji wa Kipindi cha Runinga cha In My Shoes, Wema Sepetu ameapa
kwamba hata iweje, lazima msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond’ awe mume wake, Amani lina stori kamili.
NI CHAGUO LAKE
Akizungumza na Amani katika spesho intavyu hivi karibuni, Wema ambaye kwa sasa anapika na kupakua na Diamond alifunguka kuwa, amepita kwa wanaume wengi ila anaamini mwanaume huyo ndiye chaguo lake.
Alisema katika uchunguzi wake aligundua kwamba Diamond anampenda kupita maelezo na kwa mapenzi anayomuonesha hana sababu ya kugoma kumpa nafasi ya kuwa mkewe.
“Yaani watu watasema sana lakini piga, ua, garagaza, lazima Diamond anioe. Amekuwa akilizungumzia hilo na kuonesha kuwa yuko ‘siriasi’ hivyo ipo siku historia itaandikwa bila kujali nani atasema nini.
“Unajua mimi ni mtu ninayejitambua na ninayejali maisha yangu hivyo ninapobaini mwanaume f’lani anaonesha kunijali na kunipa mapenzi ninayoyahitaji, kwa nini nisikubali kuingia naye kwenye maisha ya ndoa…?
“Kwa kifupi nampenda Diamond na yeye ananipenda, that’s it,” alisema Wema.
MKWARA WA MAMA YAKE
Kuhusu mama yake kuchimba ‘biti’ kuwa hamtaki Diamond na kamwe hawezi kukubali mwanaye aolewe na mwanaume huyo, Wema alisema:
“Unajua yule ni mzazi, wakati mwingine si mbaya kuonesha hisia zake lakini nitamseti na naamini kwa kuwa ananipenda atakubaliana na mawazo yangu.”
NDOA LINI?
Alipobanwa kuhusu lini watafunga ndoa kwani wamekaa kwenye uhusiano kwa muda mrefu huku wakiachana na kurudiana, Wema alionekana kutokuwa na jibu la moja kwa moja ila akaishia kusema kuwa, siku ikifika kila kitu kitakuwa wazi.
NUKUU YA MAMA WEMA!
Katika sakata hilo, kwa upande wake mama Wema alikuwa na haya ya kusema: “Ndoa yao watafungia chumbani, si hadharani, tena wakiwa na ndugu wa upande mmoja tu wa Diamond.
“Sisi hatuwezi kushiriki ng’oo, ndugu zangu wakijitokeza tu nitakuwa na panga mkononi, watakiona cha moto.”
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2011 ndani ya Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki, Dar, Diamond aliwahi kumvisha pete ya uchumba Wema na ikadaiwa kuwa siku nyingi wangeingia katika maisha ya ndoa lakini haukupita muda mrefu wakaachana.
Baada ya kumwagana, Diamond alikwenda kwa mtangazaji wa DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema alihamishia penzi kwa yule kigogo aliyefahamika kwa jina moja la Clement ‘CK’ kabla ya kumwagana hivi karibuni.
Credits:Global Publishers
↧
↧
KIMWANA ALIYE VUNJA NDOA YA BOB JUNIOR AFUNGUKA LA MOYONI.

Mama wa mtoto wa kike mmoja na muigizaji kutoka kenya ambaye vile vile ni Promota ambaye alikumbwa na skendo kuwa ndiye chanzo cha ndoa ya msanii kutoka Tanzania Bob Junior na mkewe kuvunjika.
Mwanadada huyu anayejulikana kwa jina la Ashlay Toto alikumbwa na skendo hiyo walipokuwa nchini Denmack na Bob Junior kikazi. baada ya skendo hiyo kumfikia mwanadada huyu alifunguka na kukanusha taarifa hizo vile vile Bob Junior naye pia alifunguka na kukanusha taarifa hizo.
Siku kadhaa zilizopita Bob Junior alifunga tena ndoa na aliyekuwa mke wake ambaye waliachana kwa kwa miezi kadhaa. Hapa mwanadada huyu kaamua kufunguka na kueleza hisia zake kuhusu ndoa hiyo.
↧
Kutana na Mwanamke Mwenye Kiuno Kidogo Kuliko Wote Duniani.
Mwanzoni nilikuwa natia shaka juu ya hili mpaka nilipokuja kuona kuwa naye yumo miongoni mwa watu kwenye kitabu maarufu cha kumbukumbu za Guinness world.
Cathie Jung ana miaka 77 na ndiye mwanamke mwenye kiuno chembamba zaidi Duniani. Hakika hii inashangaza kimtindo.
Cheki picha zaidi hapo chini...
lla unadhani hii ni hali ya kawaidia au ni ugonjwa...?
Cathie Jung ana miaka 77 na ndiye mwanamke mwenye kiuno chembamba zaidi Duniani. Hakika hii inashangaza kimtindo.
Cheki picha zaidi hapo chini...
lla unadhani hii ni hali ya kawaidia au ni ugonjwa...?
↧
MB Dog aeleza vitu anavyomiss Tip Top Connection.

Akiongea na tovuti ya Times Fm, MB Dog amesema kuwa kikubwa alichokimiss kutoka kwenye kundi hilo ni ‘sikio’ la boss wake Abdu Bonge katika kusikiliza na kuzitabiri hits kwa kumsikia tu mwimbaji akifanya mitindo huru ‘freestyle’.
“Kule kitu kimoja nilichokuwa nakimiss…ujue nikikaa na boss wangu Bonge, na Madee kichaa wangu alikuwa sana, ninapofanya hata freestyle ya uongo tu…Bonge unajua anasikio sana la kutaka kujua kitu gani ambacho unakifanya, unaweza ukaimba ngoma ambayo unaipenda akakwambia ‘daah hiyo sio hebu ile nyingine ile’.” Amesema MB Dog.
“Kwa hiyo yeye anamasikio sana ya kusikia kitu kizuri kabla watu hakijawafikia. Kwa hiyo hicho kitu kimoja ambacho huwa nakaaga nakifikiria kwamba daah, yule mchizi alikuwa ananipiga tafu…lakini kwa sasa sina mtu wa kuniambia hivyo, so hivyo ni vitu waga nakaa navimiss.”
Katika hatua nyingine, MB Dog ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa tayari ameshakaa na uongozi wa Tip Top connection na wamemaliza tofauti zao, na kwamba Abdu Bonge amemuahidi kumsaidia tena kuzisimamia kazi zake japokuwa hayuko Tip Top Connection.
“Kwa sasa niko chini ya kampuni ya QS niko na jamaa mwingine anaitwa Ngonyani. Jamaa walikaa wakawaza ‘daah huyu jamaa mwanetu tulikuwepo naye’, kama kuna sehemu walikuwa wanakwamisha wanaijua wamefikiria unajua, na kinachowaumiza kwa nini mimi niko kimya halafu kimya changu kimezidi.
“Sasa kuna vitu wanavyovipata kwenye mioyo yao, wakanisogelea ‘bana eeh inakuwa vipi’, na kwa sababu hii ni kazi na haya ni maisha wakaona sio vyema. Ndio maana sasa hivi naweza kusema nina back up kubwa kutoka kule kwa sababu Bonge mwenyewe alisema bana tufanye kazi mwanangu nisimamie, kama kuna hivi na hivi pia tutajua tunafanya nini.” MB Dog ameeleza.
Msanii huyo amesema hivi sasa anamiliki studio yake na ameiboresha zaidi hivi sasa.
↧