Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live

Tendo la ndoa Ni Tiba mbadala ya maradhi ya moyo,ubongo na maumivu ya kichwa.

$
0
0
Ingawa tendo la ndoa lisipofanywa kwa kuzingatia kanuni na taratibu, sambamba na umakini, linaweza kusababisha maradhi, lakini kwa wanandoa, tendo  hilo linatajwa kuwa na manufaa mengi  kiafya tofauti na faraja ya kawaida iliyozoeleka kwa wengi.
Imefahamika kuwa tendo hili likifanyika ipasavyo husaidia kuondoa msongo wa mawazo, maradhi ya moyo, maumivu ya kichwa yasiyokoma na kupunguza kasi ya saratani ya tezi dume.
 Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), Dk Yahya Kishashu anasema inategemea tendo linafanywa na nani na mhusika yupo kwenye mazingira gani.
“Kwa mfano, tendo la ndoa linaondoa msongo wa mawazo iwapo unayetenda naye unampenda na  amekupa maandalizi mazuri. Sidhani kama alimradi utende hilo tendo na yeyote litakusaidia,” anasema mtaalamu huyo.
Anaongeza kuwa  ndiyo maana baadhi ya watu wanatoka nje ya ndoa zao kwa sababu si mara zote tendo la ndoa linawafurahisha wanandoa.
“Wakati mwingine tendo hilo laweza kuwa karaha kwao,” anasema
Mazoezi
Si hivyo tu, utafiti uliofanyika Canada  hivi karibuni umebainisha kuwa kufanya tendo la ndoa kwa kipindi cha dakika 25 kwa wanamume kunachoma kalori 100 na kwa wanawake kalori 69.
Tendo hilo likifanyika kwa nusu saa, linaweza kupunguza kalori za mwili kuliko kutembea kwenye mashine ya mazoezi ya ‘treadmill’.
“Ni sawa na kucheza mpira wa tenisi au kutembea ukipanda mlima kwa dakika 20 au kucheza gofu kwa kasi kwa dakika 33 au zoezi la yoga kwa dakika 40,” sehemu ya utafiti hiyo inasema.
 Utafiti huo wa Canada ulishabihiana na kampeni  iliyofanywa na Taasisi ya Moyo ya Uingereza ambayo ilisema kuwa  dakika 30 za tendo la ndoa kwa siku ni muhimu kama mazoezi ya kutembea kwa mashine.
Kwa undani zaidi utafiti huo ulichambua na kusema kuwa, tendo la ndoa, lina manufaa  kwa moyo na mapafu.
Inaelezwa kuwa vichocheo  vinavyotoka  baada ya tendo la ndoa vinasaidia kupunguza kiwango cha msongo wa mawazo na kuongeza  uzalishaji wa seli mpya za ubongo.
 Kuhusu mazoezi, Dk Kishashu anasema anakubaliana na utafiti huo na kusema kuwa ni kweli tendo hilo linasaidia kupunguza kalori, lakini linapofanyika mara nyingi zaidi linazeesha.
Hata hivyo, wanasayansi wanalipa uzito mdogo tendo hilo katika muktadha wa ujenzi wa hisia na mwili na kuwa halisisitizwi vya kutosha kama aina mojawapo ya mazoezi.
Tiba kwa moyo, mapafu na ubongo
Inaelezwa kuwa tendo la ndoa, linasaidia kuondoa msongo wa mawazo hivyo kupunguza hatari ya maradhi ya moyo.
Si hivyo tu, bali tendo hilo husaidia mapafu kufanya kazi yake vyema, kuingiza na kutoa hewa chafu.
Kitaalamu, upo mchakato uitwao ‘Neurogenesis’ ambao husaidia kulinda seli za ubongo zinazokufa kutokana na uzee. Kuna eneo kwenye ubongo linaloitwa ‘hippocampus’ ambalo ni eneo linalotengeneza kumbukumbu.
“Kazi kubwa inafanyika kwenye ubongo, wakati wa tendo la ndoa, kiasi kikubwa cha viamsha raha huanzia kwenye ubongo na kuleta taarifa kwenye maeneo mengine ya mwili.
Ndiyo maana watu wengi hupotea kiufahamu wakati wa kilele” anasema Dk Gosh, ambaye ni mtafiti.
Hata hivyo, wanaume ambao wanaendelea na tendo la ndoa mara kwa mara hadi wanapofikisha miaka 50 na zaidi, kwa maana ya kutoa mbegu za kiume mara kumi kwa mwezi, wapo katika hatari ndogo ya kupata saratani ya tezi dume.  Inaelezwa kuwa mbegu za kiume hazitakiwi kukaa mwilini kwa muda mrefu.Zinatakiwa zitolewe mara kwa mara ili kuzifanya seli mpya zizalishwe. Ni kama kusafisha mpira, inasaidia kusitisha ujenzi wa seli za zamani ambazo zaweza kuwa chanzo cha saratani.
Kwa wanawake, tendo la ndoa husaidia kuundwa kwa misuli ya nyonga ambapo misuli hiyo ikiwa imara huondoa hatari ya kushindwa kuzuia mkojo,(urine incotinence) jambo linaloathiri mwanamke mmoja kati ya wanne wenye umri wa miaka zaidi ya 50.
“ Wakati wa tendo la ndoa, kwa kawaida sakafu ya nyonga za mwanamke hubana na kuachia. Hii husababisha misuli hiyo kuwa imara’ anasema mtafiti huyo.

DK Cheni adai filamu yake 'Nimekubali Kuolewa' haichochei ushoga kama bodi ya filamu ilivyoichukulia na kuamua kuizuia.

$
0
0

Uamuzi wa bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuizuia filamu ya muigizaji wa kiume na mkongwe, Dk Cheni ‘Nimekubali Kuolewa’, kwa madai ya kukiuka maadili na kuchochea tabia za ushoga, umepingwa na msanii huyo ambaye anaamini kabisa kuwa maudhui ya filamu hiyo yangeelisha jamii zaidi ya picha katika cover yake.

Dk Cheni ameiambia Global Publishers kuwa picha iliyoko kwenye bango la filamu hiyo inayomuonesha akiwa amevaa shera, ndiyo iliyotumiwa na TFB kama kigezo zaidi huku mahudhui yakiwekwa kando.
“Eti ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, wamenionea, lengo letu ni kukemea na kupinga vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja, huwezi kuelimisha bila kuonesha madhara yake kwa vitendo kama ilivyo kwenye filamu hiyo. Amesema Dk Cheni.
Msanii huyo alivitaja vipande ambavyo anaamini ilibidi vifikiriwe na TFB kufunika sababu zao zilizopelekea kuzuiwa kwa filamu hiyo.
“Lakini ndani ya filamu hiyo, kuna kipande ambacho kinaonesha kiongozi wa serikali akikemea kitendo hicho, sasa hapo ushoga wangu uko wapi? Kuvaa shera kwenye cover? Alihoji Dr. Cheni na kusisitiza kuwa uamuzi huo haukuwa sahihi.
Mwaka jana Dr. Cheni aliiambia tovuti ya Times Fm kupitia kipengele cha Times Q & A ambapo alisema kuwa anatarajia kufanya filamu hiyo ambayo itakuwa ya tofauti ama ya pekee (unique) zaidi.
“Nahisi filamu inayokuja inaitwa ‘Nimekubali Kuolewa’, itakuwa ya kipekee sana, kwa sababu hata pale kwenye cover lake tu itakuwa ‘unique’ kwa sababu ntakuwa nimekaa nimevalishwa shela, kuonesha kwamba ni kweli nimekubali kuolewa, hii itakuwa tofauti na movie nyingi nilizowahi kucheza, itakuwa ‘Unique’.” Dk Cheni aliiambia tovuti ya Times Fm.

AY kuachia wimbo mpya 'Asante' February 10, amemshirikisha Dela.

$
0
0

Mwaka 2014 umeingia mwezi wa pili huku mashabiki wa muziki wakipata nyimbo mpya kadhaa kutoka kwa wasanii wanaowakubali.

Lakini mwezi February ndio kama umewasha green light tena kwa mwimbaji wa Tanzania ambaye ameyazoea mashavu ya kimataifa, Ambwene Yesaya aka AY, ambapo anatarajia kuachia wimbo mpya aliupa jina la Asante, February 10 mwaka huu.
“Where there is love there is life.. #ThanksForTheLove STAY TUNNED... 10TH FEBRUARY 2014.” AY ameandika kwenye Instagram.
Ay amemshirkisha Dela katika wimbo huo uliopikwa ndani ya MJ Records na Marco Chali, na tayari umeanza kuzungumziwa vizuri na watu ambao bila shaka wameusikiliza na wameanza kuutaja kama wimbo mkali unaokuja ‘hit’.
“Ya'll get ready fi dis one...Major Hit....Major Artist.... Asante @aytanzania @timesfmtz @mwanafa.” Hermy B, producer na CEO wa B’Hitz Music Group ameandika kwenye Instagram na kupost artwork ya wimbo huo.

Jose Chameleone amuonesha mkewe 'Danniella' anavyompenda kwa kuchora tattoo ya jina lake shingoni.

$
0
0
Chameleone ambaye yuko nchini Afrika Kusini kwa shughuli za kimuziki, alipost picha hizo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, picha zinazoonesha tattoo hiyo hata mtu akimuona kwa mbali kidogo.
Mwimbaji huyo wa Valuvalu ambaye ana watoto watano aliozaa na mkewe Daniella hakuwasahau wanae pia, alijichora katika mkono wa kushoto tattoo yenye majina manne ya wanae wanne na anatarajia kuongeza moja yenye jina la mwanae wa kwanza, Ayla.
“2014 we stand tall for the ones we care for and those that love us back with their whole. For me, this is my expression..” Amesema Chameleone.

Shilole ayazungumzia makavu aliyorushiwa na Baby Madaha, 'najua kuna vitu vingi nimekuzidi..' ampa ushauri.

$
0
0

Baada ya msanii wa Candy n Candy, Baby Madaha kufunguka akimchana wazi msanii mwenzake wa kike, Shilole aka Shishi Bybee kwa kudai kuwa nyimbo zake haziwezi kulinganishwa na nyimbo anazofanya Shilole, Shilole nae kakikalia kiti kile kile na kuyajibu makavu hayo.

Shilole amedai kuwa hawezi kupoteza muda kumzungumzia Baby Madaha, na kwamba yeye anaamini hana tatizo naye lakini anashangaa kuona anamzungumzia.
“Ni kama Baby Madaha anavyonizungumzia mimi, mmekua mkiona na wengine mliumia mkasema sana kwa nini ananizungumzia mimi. Baby Madaha sina tatizo naye lakini nashangaa amekuwa mtu wa kunizungumzia everyday, I don’t know why.” Amesema Baby Madaha.
Mkali huyo aliamua kumpa ushauri Baby Madaha kwa kile alichokiita kumsema yeye vibaya ni kupoteza muda wake.
“Wewe mwanamke, mimi mwanamke mwenzio nafanya kazi, umeshaniona hata siku moja naenda kukuzungumzia somewhere? Muogope Mungu kukaa unamzungumzia mtu ambaye hana time, hana shida na wewe. Hebu tubadilike wanawake tupendane tuache kuzumziana vibaya.” Shilole ameeleza.
“Kwani ukinizungumzia mimi vizuri utapata nini, najua kuna vitu vingi nimekuzidi lakini usikae unamzungumzia vibaya. Wanawake tupendane tupeane sapoti. Ndio maana hatufiki mahali tunabaki tu kulalamika ‘ooh nimerogwa’, hujarogwa umejiroga mwenyewe.” Shilole anakaririwa.
Chanzo: Channel 10

MH.LOWASSA AKANA UMILIKI WA KURASA ZA MITANDAO YA KIJAMII.

$
0
0
Kumekuwa na kurasa (accounts) mbalimbali zenye jina la Mh. Edward Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mitandao
ya kijamii Kama vile Facebook,Twitter,Instagram nk.
Zinazoonye kuwa mmiliki wake ni Mh. Edward Lowassa.
Ukweli ni kwamba hizo kurasa zote hazimilikiwi na Mh. Lowassa.
Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye kurasa hizo,hazihusiani kwa namna yoyote na Mh. Lowassa.
Hata hivyo Mh. Lowassa anawashukuru wote wenye kumiliki account hizo bila ya ruhusa yake, kwani anaamini wamesukumwa na mapenzi yao kwake.


Credit:Udakuspecially.

Simu 600 zanaswa kwenye Gereza la Kamiti.

$
0
0

Zaidi ya simu 600 za mkononi pamoja na takriban laini 5,000 za simu zimenaswa katika gereza la Kamiti Maximum baada ya msako wa kushtukiza uliofanywa chini ya usimamizi mkuu wa gereza hilo.
Naibu ofisa mkuu katika gereza hilo, Patrick Isaboke alisema msako huo uliodumu kwa siku nne ulifanywa baada ya uchunguzi kubaini kuwepo na ujumbe mwingi wa kutishia raia hutoka magerezani.  Isaboke alisema kuwa hawakuweza kuwajua wafungwa wanaomiliki simu hizo kwani walitolewa wote ndani ya sehemu wanazoishi ndani ya gereza hilo, kabla ya msako kufanywa.
Msako huo umethibitisha hofu kwamba Gereza la Kamiti linahusika kwa kiasi kikubwa katika visa vya utekaji nyara jijini Nairobi na viungani mwake, kutokana na mawasiliano ambayo yamekuwa yakiendelea baina ya wafungwa waliopo gerezani humo na jamaa au makundii yao yaliyopo uraiani.
Juzi, wafungwa walizua vurugu baada ya msako. Katika vurugu hizo, wale walioitwa  kuripoti katika viwanda vya gereza hilo waligoma na badala yake kuandamana. Walinzi walilazimika kufyatua risasi hewani ili kutuliza vurugu hizo.
Angalau wafungwa wanne walijeruhiwa lakini wasimamizi wa gereza hilo walikataa kutoa taarifa yoyote kuhusu kisa hicho, kwa kuwa taarifa za mambo mengi yanayoendelea ndani ya magereza hufanywa siri.
Taarifa zilieleza kwamba baadhi ya walinzi walizidiwa wakati wa vurugu hizo na ikamlazimu mkuu wa gereza hilo kuwaita walinzi kutoka magereza mengine na wale walio katika Chuo cha Magereza cha Ruiru.
Vyanzo muhimu katika tukio hilo vilikaririwa vikieleza kwamba ofisa mkuu wa Serikali alimwamuru Waziri wa Usalama, Joseph ole Lenku kufanya msako wa kunasa vitu visivyoruhusiwa magerezani baada ya uchunguzi kuhusu kisa cha utekaji nyara kuonyesha kuwa kilikuwa kinapangwa gerezani humo.
Kuadhibiwa
Ingawa maofisa hao wanapaswa kuwafanyia msako wafungwa wote, ripoti zinaeleza kuwa baadhi ya walinzi wa gereza wanashirikiana na wafungwa ili kupeleka vitu hivyo haramu gerezani. Duru zinasema kuwa maofisa hao huwauzia wafungwa simu hizo.
“Baadhi ya wafungwa hawaadhibiwi wanapokutwa wakiwa wanamiliki vitu haramu kama hivyo, ambavyo kimsingi huwa havitakiwi kabisa kuwepo gerezani. Kuna viranja ambao ni macho ya walinzi katika kila seli,” alisema mlinzi mmoja wa cheo cha chini ambaye aliomba asitajwe jina.
Ilielezwa kwamba mara nyingi simu hubebwa na maofisa wakuu ambao huwa hawafanyiwi msako wanapoingia katika taasisi hiyo. Maofisa hao hukabidhi simu hizo kwa walinzi wanaosimamia vitengo tofauti.

NAY WA MITEGO AMEMNUNULIA GARI MPYA MPZ WAKE.PIA AMESEMA MWAKANI ATAMNUNULIA PRADO.

$
0
0

Rapper Ney Wa Mitego aka True Boy kaweka hii picha na maneno haya kuhusu gari mpya aliyomnunulia Mpenzi wake huku akiahidi kumnunulia Prado mwakani.

” Zic iz 4u bby..#zawadi #yako my #super #women…#chama #kubwa#966 Mwezi wa #7 ntakununulia #prado sawa?! Hahaha kaa Umooooo@truegal966 ”
ney

Diamond Karudisha Muonekano Wake Wa Zamani.

$
0
0

Kwa Shabiki wa msanii wa bongo fleva mwenye nyimbo nyingi na zinazopendwa kwa sasa, Msanii Diamond, Jamaa karudisha muonekano wake wa kawaida na kaweka hii picha kwa ajili yako.

Hii ndio ilikuwa comment yake kwenye hii picha
dd 2
“I decided to change my look and jus get back to my old one dat is entire black…Haya sasa wewe niambie, wat’s your opinion, should i keep this look or jus go back to da blonde…. ??”

Kutana na Binadamu Wa Kwanza Kupewa Mkono Wa Kieletroniki Wenye Hisia.

$
0
0

Repoti ya Bbc Kuhusu Mlemavu mmoja kutoka Denmark Dennis Aabo ambaye amekuwa binadamu wa kwanza kupewa mkono wa kieletroniki wenye hisia kama ule wa binadamu Iko Hapa.

BBY 3
Mfumo wa mkono wa Kielektroniki
Katika tukio linalopigiwa upatu kuimarisha hali ya walemavu katika siku za usoni, madaktari huko Italia wameuunganisha mkono huo wa kielektroniki na neva za mabaki ya mkono wa Dennis uliokatwa baada ya ajali mbaya ya fataki na hivyo kumwezesha kuhisi kupitia kwa vidole vya mkono huo wa kielektroniki .
Hisia
Mkono bandia
Silvestro Micera aliyeongoza upasuaji huo alifurahishwa mno na uwezo wa mgonjwa wake kuutumia mkono huo bandia .
” tumeshangazwa sana na urahisi wa mgonjwa wetu kuwasiliana mara moja na mkono huu bandia wa kielektroniki kuekelea majukumu ya kushika na kuhisi vitu tofauti .
Hata ikiwa upasuaji huu utakuwa wa muda tu, ninahakika Denis ameotambua mwenyewe kuwa utakuwa wenye manufaa makubwa kwake katika siku za usoni”
Dennis hakuficha furaha yake alisema mkono huo umebadilisha kabisa hali yake.
”hisia zangu za mkono zimeimarika maradufu maanake ninawezajua ugumu na mfumo wa kitu chochote ni kama mkono wa kawaida”
nas
Mkono bandia wa kielectroniki

Hawa Ndio Wachezaji Wanaopinga Matumizi Ya Makahaba katika Kombe La Dunia Brazil.

$
0
0

Hii Ni kutoka kwa wachezaji wa ligi zinazofwatiliwa zaidi duniani,

Ligi ya soka ya Uingereza na ligi ya Brazil. Wachezaji hawa wameunga mkono kampeni ya kupinga kutumiwa kwa makahaba watoto wakati wa kombe la dunia.
Watatu kutoka klabu ya Chelsea ambao ni  Frank Lampard,Oscar na Ramirez wamekubali kuunga mkono kampeni hiyo kinachofanya kazi na  kitengo cha kukabiliana na uhalifu  wa binadamu nchini Uingereza .
mimi 2
Kampeni hii inazuia mashabiki kutoka Uingereza kulala na msichana mwenye umri chini ya miaka 18 na kumlipa.
Fahamu kuwa  Brazil linakadiriwa kuwa na nusu ya milioni ya idadi makahaba watoto wanaosimamiwa na magenge ya uhalifu na kuna hofu kwamba idadi hiyo itaongezeka wakati wa michuano hiyo.

Facebook Inawatumiaji Wangapi, Imefikisha Miaka Mingapi Na Watu Gani Wanaikimbia Sasa.

$
0
0

Facebook inasherehekea miaka kumi wiki hii tangu kuzinduliwa. Ina watumiaji bilioni 1.2. Lakini nani anatumia Facebook and wanaitumia kwa njia gani?

Mishumaa kwenye keki ya Facebook inaposherehekea miaka 10 haitazima kabla ya mtu kuwa na tashwishi ikiwa kampuni hiyo itadumu na kufikisha mwaka wake wa 11.
Katika utafiti uliofanywa hivi karibuni, ikiwa utaaminika , siku za mwisho za Facebook zinakaribia.
Taarifa mbali mbali zinapendekeza kuwa idadi kubwa ya watumiaji wa Facebook , vijana wakiwemo wengi, wanachoshwa na mtandao huo wa kijamii baadhi ya watafiti wakisema kuwa watumiaji wengi wanalinganisha Facebook na maradhi mabaya.
Utafiti kama huu ambao huambatanishwa na picha ya Mark Zuckerberg mwasisi wa mtandao huo akionekana mwenye huzuni huonyeshwa sana na vyombo vya habari na hata kusambazwa zaidi kwenye Facebook.
bby
Kwa hivyo wakati watafiti waliposema kuwa kampuni hiyo itapoteza asilimia themanini ya watumiaji wake katika kipindi cha miaka mitatu, wakuu wake walijibu kwa ukali.
Facebook ina watumiaji wengi zaidi vijana kuliko mtandao mwingine wowote.
Imekuwa ikibadili sura yake tangu mwaka 2004.
Hata hivyo baadhi ya watafiti wanasema kuwa karibu vijana milioni tatu waliondoka kwenye Facebook katika miaka mitatu iliyopita nchini Marekani.
Vijana wengi wanasema waliacha kutumia Facebook kwa sababu ya wazazi wao, ambao pia wamejiunga na mtandao huo wa kijamii.
Wazazi hutuma picha za watoto wao kwenye mtandao ambazo wao wenyewe wanahisi ni za kuchekesha.Jambo hili limewatia aibu vijana ambao wameamua kutumia mitandao kama WhatsApp au Snapchat badala ya kuwa kwenye mtandao mmoja na wazazi wao.
Licha ya vijana wanaotumia Facebook kupungua watu wenye umri zaidi ya 55 wameonekana kuongezeka.
Sasa je ni hali ya vijana kuondoka Facebook na kuwachia watu wazima nafasi kutumia mtandao huo? Je utafikisha miaka 11? Wataalamu wana shaka na hilo. Wewe je? Bado utahitaji Facebook mwaka ujao?

JOKATE AFICHUA SIRI YA KUPATANA NA WEMA.

$
0
0

THE big boss wa Kidoti, Jokate Mwegelo ambaye pia ni staa wa sinema na Bongo Fleva, amefichua siri ya kupatana na Wema Isaac Sepetu akisema kuwa
sababu ya yeye kuonekana kwenye jukwaa moja na aliyekuwa hasimu wake huyo ni kutafuta amani ya moyo aliyokuwa ameikosa si kweli kwamba alisukumwa na nguvu ya pombe.…
Wawili hao walipatana hivi karibuni wakiwa jijini Arusha.
Akizungumza na gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Jokate alisema ilipokaribia siku ya kwenda Arusha, Wema alimkaribisha kwenye shoo yake iliyofanyika jijini humo lakini alimwambia kuwa amebanwa ila akamuahidi kwamba akimaliza mambo yake atakwenda kumsapoti.
“Wema aliondoka bila kujua kama nitakwenda lakini nilipopanga ratiba yangu ikakaa sawa, niliamua kwenda na kumfanyia ‘sapraizi’ na si kweli kwamba nilisukumwa na nguvu ya pombe,” alisema Jokate.
Jokate alisema kwamba hakushauriwa wala kujadiliana na mtu yeyote isipokuwa aliamua mwenyewe kufanya jambo hilo ambalo lilikuwa likimkosesha faraja kwa muda mrefu.
“Nimeamua kumaliza mabifu kwa sababu nilikosa amani ninayoitaka kwa muda mrefu. Ukweli Wema alinikaribisha, nikaona ndiyo sehemu ya kutimiza lengo langu la kupatana naye,” alisema Jokate ambaye aliingia kwenye gogoro na Wema baada ya kutembea na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Chanzo:Global Publishers

BABY MADAHA AKIRI UCHAWI UPO BAADA YA KUPIGWA JUJU NA KUSINGIZIWA KUJIUZA.

$
0
0

Mwanamuziki na muigizaji baby Joseph madaha amefunguka na kusema kuwa kweli ameamini uchawi na kupigana juju vipo kwenye gemu kwani mambo yaliyomtokea hivi karibuni haelewi hata imekauje.


Chanzo nini?

Hapo siku za nyuma baby Madaha alipatikana na dhahama ya kukumbwa na kashfa nzito sana ya kujiuza kwa dau la milioni kumi kwa jamaa mmoja hivi mitaa ya Dar es Salaam Jambo lilolopelekea yeye kupigwa chini na Record label yake ya Candy and Candy ya huko Kenya na kupokonywa gari aina ya AUDI TT aliyokuwa akitembelea huku akiharibu pia uhusiano wake na bosi wa record label hiyo - Joe kairuki ambaye pia anadaiwa kuwa mpenzi wake.

Je ni Kweli alijiuza?

Baby Madaha ambaye amerudi nchini hivi karibuni tokea Nairobi alipoenda “ku-solve” ishu yake hiyo na label hiyo anasema yani hata haelewi kitu gani kilitokea siku hiyo ingawa mpaka akaandikwa kama alienda kujiuza, anachokumbuka ni kupigiwa simu na mtu asiyemfahamu an kumwambia anataka wafanye naye kazi ya kusambaza filamu yake mpya ya Gal Bladder ambaye inatikisa soko kwa sasa.

Baada ya kufika hapo waliongea vizuri na kuondoka ghafla kabla ya kuja kusoma kesho yake kuwa alikuwa anajiuza kitu ambacho ansema hajui kimetoka wapi.

“Yani hata sielewi ilikuaje nikaenda kukutana na yule jamaa, ilikuwa ni kama muujiza hivi, mwanzo nilisita sana ila nikashangaa nimefika tu pale bila kujielewa, ni vitu vya ajabu sana” alieleza baby Madaha.

Uhusiano wake na Label hiyo ukoje sasa?

Akizungumza na bongomovies, baby amesema kwa sasa kila kitu kipo sawa kwani alipoenda Kenya waliongea vizuri na bosi wake huyo na kumaliza tofauti zao na sasa amerudi nchini kusambaza filamu yake hiyo mpya ya Gal bladder huku akijiindaa kupiga show kwenye tour yake aliyoiandaa  jina la Top Up and Refill itakayofanyika mwezi ujao wa tatu.

Mwenyewe anasemaje zaidi?

Hata wafanyaje, waniroge, wanichafue, i'm a bad gal, na sibabaishi na vijimaneno vya watu hata kidogo, sitoki candy and Candy hata waloge kwa waganga wote duniani. Kama walifikiri nimeumbuka, wajue watasubiri sana. Nikitoka kenya naenda Holywood tu!

Gauni La Mariah Carey Linaloteka Vichwa Vya Habari Ndio Hili.

$
0
0

Kwenye sherehe ya BET Ya mwaka 2014 yakushukuru wasanii na watu maarufu kwa mchango wao kwenye mambo
tofauti,red carpet ya shughuli hio ilipambwa na wasanii kama Ice Cube, Tamar Braxton, Jennifer Hudson na Ludacris.
Mitandao Marekani wameamka na hii story kuhusu gauni la Mariah Carey aliyovaa kwenye shughuli hio.
1 2 34

Taarifa Ya BBC Kuhusu Shabiki Wa Liverpool Aliyeuliwa Kenya.

$
0
0

Mwanamume raia wa Kenya anayeshabikia klabu ya soka ya Uingereza ya Liverpool amedungwa kisu na mwenzake wa klabu ya Arsenal na kufariki dunia katika eneo la Meru Mashariki mwa Kenya.

Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo wawili hao walianza malumbano baada ya mechi kati ya vilabu hivyo kumalizika hapo Jumamosi.

Wawili hao walikua katika baa moja iliyojaa mashabiki wa timu hizo mbili.
Shabiki wa Arsenal anayefanya kazi ya Boda Boda alijawa na hasira baada ya timu yake kukemewa na shabiki wa Liverpool kiasi cha kumdunga mwenzake kisu mara kadhaa, kabla ya kutoweka.
Watu waliokua karibu na eneo la tukio hilo walimsaidia mwathiriwa aliyetambuliwa kama Anthony Muteithia na kumpeleka katika hospitali kuu ya Meru ambapo alifariki dunia wakati akipokea matibabu.
Mkuu wa polisi eneo la Meru Tom Odero amesema wanamsaka shabiki huyo wa Arsenal ambaye amekwenda mafichoni.
Hapo Disemba mwaka jana shabiki wa klabu ya Manchester United nchini Kenya kwa jina Jimmy Macharia alijiua baada ya klabu hiyo kuendelea kuorodhesha matokeo mabaya.
Na mnamo mwaka 2012 Suleiman Alfonso Omondi shabiki wa Arsenal alijitia kitanzi baada ya timu hiyo kushindwa kwenye mechi. Ligi ya Premia nchini Uingereza huvutia ushabiki mkubwa nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Ja Rule aeleza kilichotokea baada ya kupanda ndege moja na 50 Cent.

$
0
0

Miezi kadhaa iliopita (mwaka jana), kulikuwa na habari ambazo zilithibitishwa na Ja Rule kuwa walijikuta wamepanda ndege moja na 50 Cent ambaye bado lile vuguvugu la uadui kati yao linaeleweka mitaani.

Member huyo wa zamani wa Murder Ink alifunguka katika interview aliyofanya Vibe kuhusu kile kilichotokea kwenye ndege hiyo.
Ja Rule alifunguka kuwa hakuna kilichotokea baada ya wawili hao kuwa ktika ndege moja zaidi ya kuonana na kusalimiana tu kisha kila mmoj akaendelea na mambo yake.
“We actually did share the same flight [laughs] which is crazy. Ain't nothing really to talk about it is what it was. He seen me, I seen him. We said what's up and we rode our flight and that was that.” Alisema Ja Rule.
Ja Rule, alisema kuwa kwa hivi sasa hawana uadui kwa kuwa wameshakuwa watu wazima na kwamba hayo yalikuwa ya zamani, lakini wakati huu wanaangalia pesa, familia na kile wanachokifanya sasa hivi.
Kwa upande wa 50 Cent, December mwaka jana aliulizwa swali hilo kwenye mahojiano waliyofanya live radioni na Dj wa G Unit, Dj Whoo Kid, aliyetaka kufahamu kutoka kwa 50 Cent kuhusu kilichotokea kwenye ndege hiyo, na kwa nini 50 Cent hakuiongelea.
“There wasn’t nothing to talk about man.” 50 Cent aliji na kucheka, hivyo ikapita kiaina.
Huenda wawili hao wakazika kabisa beef lao kama ilivyokuwa kwa Fat Joe na 50 Cent walioishia kushirikishwa kwenye wimbo mmoja ‘Free Again’, ama Rick Ross na Young Jeezy ambao hivi karibuni wameripotiwa kuingia booth kupika wimbo mmoja.

Utumiaji wa Facebook kupita kiasi huhamisha usaliti wa mapenzi, ushahidi wa Facebook waongezeka mahakamani kwa wanaodai talaka.

$
0
0

Mtandao wa facebook ambao ulianzishwa kama utani miaka 10 iliyopita (February 4, 2004) na mwanafunzi wa chuo kikuu cha Harvard, Mark Zuckerberg, imekuwa ni njia rahisi ya kuwasiliana ambayo imeunganisha dunia na kuwaongezea watu marafiki wapya, huku ikiwarudisha pamoja walipotezana.

Ukiacha mbali faida kubwa inayotokana na utumiaji wa facebook, faida ambazo ukizitaja unaweza kujaza kitabu kikubwa bila kuzimaliza huku zikiongozwa na faida moja kubwa ‘Kuunganisha Watu kirahisi’, zipo hasara kubwa ambazo zinatokana na utumiaji wa mtandao huu kupita kiasi.
Utafiti uliofanywa na Rusell B. Clayton, Alexander Nagurney na Jessica R. Smith, na kuchapishwa kwenye Journal ya ‘Cyberpsychology, Behaviour and Social Networking’,  umebaini kuwa utumiaji wa Facebook kupita kiasi humjengea mtumiaji tabia/hali ya kutokuwa muaminifu katika mahusiano ya mapenzi.
Katika utafiti huo, Dr. Ramadhani Rursavasula, mtaalam wa saikolojia na mahusiano, ameeleza kuwa watu wengi wameigeuza facebook kuwa mbadala au sehemu ya kukimbilia kutoka kwenye mahusiano yao ya ukweli, na mwisho huishia kudanganya na kusaliti wapenzi wao kwa kuanzisha mahusiano ya siri na wapenzi wao wa zamani ama watu waliokuwa na mahusiano ya kawaida hapo awali.
Katika utafiti huo ambao ulijikita zaidi katika mahusiano yaliyodumu kwa muda wa chini ya miaka 3, ulibaini kuwa mtandao wa Facebook pia unaweza kusababisha watu walio katika mahusiano kuwa na hali ya kutoaminiana kwa kiasi kikubwa na kukosa amani katika mapenzi yao.
Matokeo ya utafiti huu unaungana na mfano wa habari iliyowahi kuchapishwa kwenye mtandao wa CNN, July 6, 2010.
Mtandao huo ulichapisha habari kuwa, Ken Savage (38), alikuwa na mkewe aliyekuwa ametoka kwenye uathirika na msongo wa mawazo na matumizi ya dawa za kulevya, hivyo akaona ni vyema kumtafutia kitu cha kumpa kampani hususani rafiki zake wa zamani. Hivyo akamuunganisha na mtandao wa Facebook.
Lakini ghafla, Ken alianza kumuona mkewe akiwa anaficha screen ya computer pale jamaa anapoingia ghafla chumbani kwake. Mwishoni akagundua tayari alikuwa ameanza kutumia mtandao huo kuwasiliana mpenzi wake wa zamani.
Mbali na utafiti huo pale juu na mfano huo, miaka mitatu iliyopita kuna utafiti mwingine uliofanywa nchini Marekana na kundi la wanasheria (The American Academy of Matrimonial Lawyers).
Utafiti huo uliojikita katika mahusiano kati ya wana ndoa wanasheria (Attorneys), ulibaini kuwepo kwa ongezeko la kesi za kudai talaka kwa asilimia 81, zinazotumia mtandao wa kijamii hususani Facebook kama ushahidi wa usaliti uliofanywa na wenzi wao.
Utafiti mwingine uliofanywa na mtandao wa Divorcce-Online wa Uingereza, uliozipitia zaidi ya kesi 5,000 za madai ya talaka, na uligundua kuwa Facebook ilitajwa kwa asilimia 20 kama sababu ama kilelezo cha ushahidi wa usaliti wa wenzi wao.
Hata hivyo, mtandao huu umeweza pia kuzirudisha ndoa zilizokuwa zimevurugika kutokana na usaliti japo ni kwa kiasi kidogo na muda mwingine kiutani.
Kwa mfano, September mwaka jana, ndoa ya Ivan Lewis na Sonya Gore ilikuwa mashakani baada ya Ivan kumsaliti Sonya, na kupelekea wawili hao kutengana kwa miezi 10.
Lakini, Ivan aliamua kuandika kwenye karatasi kwa mkono wake na kupost picha hiyo kwenye facebook ikiwa na maandishi yanayokiri kuwa alimsaliti mkewe (I cheated on my wife!!!).
Mkewe alipoona hiyo post, alimwambia Lewis kuwa kama post hiyo ikipata likes 10,000 tu atamsamehe na kumrudia. Kwa bahati nzuri ilipata zaidi ya Likes 15,000, hivyo Likes za facebook zikaiokoa ndoa hiyo.
Kama wewe ni mtumiaji wa Facebook kupitiliza, kuwa makini na matumizi yako na uhusiano wako, isije kuwa sababu ya kukushawishi kusaliti kwa kuwa wamiliki wa mtandao huo hawahusiki na faida wala hasara utakazozipata kwenye mahusiano yako kupitia Facebook.
Msemaji wa Facebook, Andrew Noyes, aliwahi kusema kuwa mtandao huo hauhusiki kivyovyote na uharibifu wa ndoa unaojitokeza..

JAYDEE AOMBA USHAURI KUBADILISHA JINA LA BAND YAKE, HATAKI TENA MACHOZI.

$
0
0









Muimbaji wa kike wa muziki wa kizazi kipya nchini Lady Jaydee afikiria kubadilisha jina la band yake kutokana na machozi yaliyokuwa yakimliza kipindi hicho yameshafutika.


Amefikiria kubadilisha jina hilo la bendi yake na isiitwe Machozi Band kama ilivyozoeleka kutokana na sasa hatowi tena machozi kama ilivyokuwa hapo awali.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika hivi " Nafikiria kubadilisha jina la band sababu Machozi Machozi niliolia zamani yashafutika. Mnashaurije???" alitupia swali hilo kwa mashabiki wake.

Magazeti ya ufaransa yadai Obama ana uhusiano wa kimapenzi na Beyonce.

$
0
0

Kuna mgongano wa habari kati ya baadhi ya vyombo vya habari vya Ufaransa na vile vya Marekani kuhusu uhusiano uliopo kati ya Beyonce Knowles na rais wa Marekani, Barack Obama.

Gazeti la Ufaransa la Le Figaro liliripoti kuwa kuna uhusiano wa siri wa kimapenzi kati ya rais wa Marekani, Barack Obama na mwimbaji ambaye ni rafiki wa karibu wa familia ya Obama, Beyonce Knowles.
Habari hizo zilishindiliwa msumari na mpiga picha Mfaransa Pascal Rostain, ambaye ni rafiki wa mke wa rais wa zamani wa Ufaransa, Carla Bruni, aliyelieleza gazeti hilo kuwa habari hizi hivi karibuni zitaandikwa na waandishi wa habari wa Marekani na inaweza kuwa kama ile scandal iliyomtesa Bill Clinton, kuhusu Monica Lewinsky (1995/1996).
“Kuna kitu kikubwa kinachoendelea kati ya wawili hawa, tusisahau Marilyn (Monroe) au Monica Lewinsky. Unaweza kuwa rais wa nchi ya kwanza yenye nguvu duniani…hiyo haikufanyi usiwe mwanaume kamili.” Rostain aliliambia gazeti hilo.
Hata hivyo, ingawa Rostain alidai kuwa Washington Post lingeandika habari hiyo leo (February 11), Washington Post imeandika habari tofauti kabisa huku baadhi ya waandishi wakikanusha habari hizo.
“Sio kweli hata kidogo”, msemaji wa Post Kris Coratti ameiambia Poynter.com kwa njia ya barua pepe. 
Naye mwandishi wa wa New York Times, Dave Itzkoff ametweet kuhusu tuhuma hizo na kuonesha kutokubaliana kabisa na kilichoandikwa na gazeti la Ufaransa.
“It doesn’t seem plausible to me that the most powerful person in the world would have time for an affair with Barack Obama.”
Ni kama vyombo vya habari vya ufaransa vimeiwashia taa familia ya Obama kuhusu mahusiano ya mapenzi. Wakati gazeti la Le Figaro likiandika hayo, jarida la Gala la nchini humo limeandika kuwa Obama na mkewe Michelle wanaelekea kupeana talaka.
Familia ya Jay Z ni rafiki wa familia ya Obama, ambapo kuna wakati Michelle na Beyonce waliandikiana barua za wazi, huku familia ya Jay Z ikialikwa mara kwa mara katika ikulu ya Marekani.
Mwaka 2012, Beyonce alimuandikia Obama barua kwa mkono wake na kuipost kwenye tovuti yake, kumsapoti katika uchaguzi wa Urais.
“President Obama,
Everyday we see your heart and character, inspiring all of us to give more of ourselves.
You are the leader to take us from where are to where we need to be.
You are the reason my daughter and nephew will grow up knowing that they can truly be ANYTHING they want to be.
All my respect and adoration,
Beyoncé.” Inasomeka barua ya Beyonce kwa Obama.
Wakati hayo yote yanaandikwa, leo rais wa Ufaransa Francois Hollande ambaye amekuwa na matatizo katika ndoa yake, ameitembelea ikulu ya Marekani na kuzungumza na rais Obama.
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live