Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live

KINGWEDU"NIMEJIPANGA VYA KUTOSHA KUINGIA BUNGENI 2015"

$
0
0

Mwigizaji wa Comedy (Futuhi) Anajulikana kwa Jina la kingwendu Amweka wazi Nia yake ya kuwania Ubunge katika kinyanganyiro cha 2015,
 
Amesema kwa sasa Amejipanga vya kutosha kuingia mjengoni , Kuhusu chama atakacho gombea kwa sasa ni siri yake ila atakitaja mambo yakikaribia....
UNAONAJE ATAWEZA AU NDIO ATAPELEKA BUNGENI VICHEKESHO? 

HICHI NDICHO ALICHOSEMA MADAM RITA JUU YA WANAUME WACHAFU.

$
0
0
Madam Rita Kaamua kufunguka kama hivi kwa wale wanaume wasio jua nini maana ya Utanashati..jisomee mwenyewe hapa chini.



UTAJIRI WA HUYU MSANII WA FILAMU ZA KIBONGO BAADA YA KUTOKA JELA IKO HAPA.

$
0
0
MIEZI tisa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kumhukumu staa wa filambu za
Bongo, Kajala Masanja kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi milioni 13 kwa kosa la utakatishaji fedha na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kumlipia hivyo kuwa huru, hali ya maisha ya msanii huyo imebadilika ghafla na sasa ameibuka katika utajiri wenye maswali na majibu.

Kajala Masanja.
Chanzo makini kimeliambia gazeti hili kwamba, Kajala ambaye alitoka mahabusu ya Segerea jijini Dar, Machi 25, 2013 akiwa hana mbele wala nyuma kiasi cha kutia huruma, sasa anazikamata za kutosha kiasi cha watu wake wa karibu kumshangaa.

MANUNUZI YAKE 
Chanzo kimebainisha kuwa, Kajala ameagiza kutoka China kontena lenye urefu wa futi 20 likiwa limesheheni  samani za ndani. Samani za ndani ni fenicha mbalimbali.

Wema na shosti wake Kajala.
“Hivi mnajua kwamba Kajala yuko juu. Naweza kusema ni tajiri kwa sasa, maisha yake ni poa. Hivi ninavyoongea kuna kontena la futi arobaini linakuja Dar, ndani mna samani tu,” kilisema chanzo hicho.

AMWAGA MILIONI 90 KUTENGENEZA FILAMU
Katika hali inayoendelea kutafsiriwa kuwa ni kuzidi kuonesha ukwasi alionao, msanii huyo ameshatumia shilingi milioni 90 kwa ajili ya kutengeneza filamu zake tatu, kila moja ikitumia bajeti ya milioni 30 za Kibongo.
Filamu ya Kajala ambayo iko njiani kutoka inaitwa Laana. Inadaiwa mpango wake ni kutengeneza filamu 10 ambazo atakuwa akiziuza kwa nyodo. Kama ni hivyo atatumia shilingi milioni 300 kwa filamu hizo kumi.

ATUMIA MILIONI 11 KUNUNUA VITO VYA THAMANI
Mbali na kuvaa magauni na viatu vya bei mbaya, hivi karibu staa huyo alitua Dar akitokea China ambapo alipigilia vito vya gharama ya maisha ya familia nzima.
“Juzikati Kajala katoka China na cheni ya dhahabu kainunua dola za Marekani elfu tatu, bangiri pia ya dhahabu ya dola elfu mbili na mia tano na hereni za gold (dhahabu) za dola elfu moja mia tano,” kilisema chanzo.
Kwa mahesabu ya sasa, kiasi hicho cha dola kikibadilishwa na shilingi ya Tanzania, Kajala alitumia kama milioni 11 kununua vito hivyo tu. 

ANAYEMPA JEURI ATAJWA
Inadaiwa mcheza filamu huyo amekuwa akipata jeuri hiyo kutoka kwa mwanaume bilionea wa Ghana aliyejulikana kwa jina moja la Safara ambaye walikutana nchini China. Inadaiwa Safara anaishi Marekani lakini ndiye anayeshika tenda ya kuinunulia serikali ya Ghana vitu mbalimbali.

MWISHO DESEMBA KUISHI NYUMBA YA KUPANGA
Habari zikazidi kumiminika kwamba, Safara amemwambia Kajala mwisho Desemba mwaka huu kuishi kwenye nyumba ya kupanga, mwakani mjengo wake utakuwa umekamilika.
Hata hivyo, haijaelezwa kama ameshapata kiwanja cha kujengea au la! Ingawa habari zinasema nyumba anayoishi sasa Kajala imeshalipiwa kodi ya mwaka mmoja na tajiri huyo wa Ghana.

MFADHILI WEMA
Ikazidi kudaiwa kuwa, katika ziara ya baadhi ya mastaa jijini Arusha hivi karibuni wakiongozwa na Wema ambako kulikuwa na shoo ya muziki wa Kizazi Kipya, Kajala alimsaidia Wema mambo mbalimbali zikiwemo pesa ili kufanikisha shughuli hiyo iliyohitaji umakini wa hali ya juu.
“Mbali na fedha hizo, Kajala wa zamani si huyu wa sasa, ila ninashomsifu bado anamheshimu sana Wema, anajua ndiye amechangia mafanikio yake, kama siku zile asingetoa zile milioni kumi na tatu Kajala angekuwa gerezani,” kilisema chanzo hicho.

ALIPOTOKA GEREZANI
Inadaiwa baada ya kutoka Segerea, Kajala aliishi maisha ya kuwa na shida hata shilingi elfu kumi ilimsumbua, Wema ndiye aliyekuwa akimbeba kwa vijisenti vya matumizi na baadaye alimwajiri kwenye kampuni yake ya filamu ya Endless Fame kama sekretari. Kampuni hiyo kwa sasa imesimama.

HUENDA CHINA KINYEMELA?
Baada ya kuona safari zake zimezaa matunda na kuhisi watu wanafuatilia nyendo zake, likiwemo gazeti hili, Kajala ambaye husafiri mara kwa mara, amekuwa akidai anakwenda Zanzibar licha ya hati zake za kusafiria kuoneshwa zimegongwa mihuri ya China na Dubai.

KAJALA SASA
Alipoulizwa kwa njia ya simu juzi kuhusiana na ukwasi wake kwa sasa, Kajala alisema anachojua yeye anaishi maisha ya kawaida, tafsiri kwamba amekuwa tajiri ghafla inafanywa na watu  wanaomuona.
“Mimi naishi kawaida tu, huo utajiri wanauona wao. Unajua haya ni maisha, leo unakuwa hivi, kesho unakuwa vile ndicho ninachoweza kukisema, siwezi kusimulia kila kitu,” alisema Kajala.

Imeandikwa na Musa Mateja na Imelda Mtema.

Shilole aeleza sifa za mwanaume atakayefunga nae pingu za maisha.

$
0
0

Linapokuja suala la mwenzi wa kufunga nae pingu za maisha, wengi hutaja sifa zinazotofautiana na sifa za boyfriend ama girlfriend wanaetaka kuwa naye.

 “Kuishi na mwanaume mwenye meno 32, hukutoka naye familia moja, sio rahisi.” Aliwahi kusema mchungaji ambaye pia ni mbunge mwanamke aliyeteuliwa na Rais.

Kwa kuzingatia hilo, mwimbaji wa kike ambaye pia ni muigizaji wa filamu za Kiswahili, Shilole aka Shishi Bybee, alipiga story na tovuti ya Times Fm katika kipengele cha Times Q & A, na kuelezea sifa za mwanaume ambaye atafaa kuwa mumewe wa ndoa.
“Mimi nampenda mwanaume mchapakazi, anayempenda Mungu. Mwanaume mweusi, mwembamba lakini asiwe mwembamba sana…kawaida.” Shilole amefunguka.
Hata hivyo, Shilole ambaye ana watoto wawili amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuolewa.
“Watoto tayari ninao wawili, sina mpango wa kuolewa. Kuolewa ni maamuzi ila bado sijaamua, nikiamua ntaolewa tu.”
Shilole ambaye mwaka jana alifanikiwa kupata show nchini Uingereza, ameachia wimbo wake unaoitwa ‘Chuna Buzi’ na mashabiki wa muziki wake wanaonesha kuulewa.

Credit:Times fm

Nyota wa Filamu za Ngono Kufanya Mapenzi na Wanaume 23 Siku Atakapotimiza Miaka 23.

$
0
0
Msanii chipukizi wa wa filamu za ngono Heidi Van Ho'rny ana mpango wa kufanya pati ya kipekee kwenye siku yake ya kuzaliwa ndani ya Montreal.


Kwa watu wengine huwa ni mishumaa na keki, na kwa baadhi ya watu huwa ni misosi, mitungi na shots za hapa na pale.

Ila kwa msichana huyu chipukizi wa filamu za ngono yeye binafsi ana mpango wa kuwaalika wanaume waliowahi kuwa wapenzi wake 23 kwa ajili ya kuwaenzi siku hiyo kwa tukio hilo la kipekee atakapokuwa akitimiza miaka 23.

Mbunge wa Iringa Mjini asomewa mashtaka kwa tuhuma za kujeruhi.

$
0
0

 Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa akidaiwa kuhusika na uchochezi na kusababisha vurugu katika kampeni za udiwani Kata ya Nduli.
Mch. Msigwa alikamatwa jana jioni baada ya kutokea kwa vurugu hizo katika mkutano wa kampeni wa chama cha Chadema.
Mwandishi wetu aliyepo mahakamani hapo anasema hali ya ulinzi imeimarishwa  huku kukiwa na idadi kubwa ya wafuasi wa Chadema, ambao hata hivyo wamesimama mbali na eneo la mahakama huku eneo hilo likilindwa na askari wa kutuliza ghasia (FFU).
Baada ya kusomewa mashtaka yake amekana na ameachiwa huru kwa dhamana, kesi hiyo itatajwa tena Machi 10 mwaka huu
Mbunge wa Chadema kortin vurugu za kampeni
Shija Felician, Mwananchi
Kahama. Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki (Chadema), Sylvester Kasulumbayi na Diwani wa Kata ya Buselesele, Crispian Kagoma na watu wengine 14 wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kujeruhi katika vurugu zilizoibuka katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kasulumbayi na wenzake 15, ambao wanaaminika kuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama saa 8.00 mchana jana na kusomewa mashtaka sita kila mmoja.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Gadiel Mariki, Mwendesha Mashtaka Shukrani Madulu alisema washtakiwa wote kwa pamoja walitenda makosa hayo Februari 4, mwaka huu.
Madulu aliiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao wakiongozwa na mbunge huyo walitenda kosa hilo la kuwashambulia kwa mapanga wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za kuwania udiwani wa Kata ya Ubagwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.
Alisema mashtaka matano ni kushambulia na kujeruhi kwa mapanga, na moja la kuharibu mali, ikidaiwa kuwa katika vurugu hizo washtakiwa waliishambulia gari la CCM la wilaya hiyo na kuliharibu.
Washtakiwa wote walikana mashtaka yote na kuomba mahakama iwape dhamana ili waendelee na kampeni za kumnadi mgombea wao wa nafasi ya udiwani katika kata hiyo ya Ubagwe.
Credit:Mwananchi.

Aamka asubuhi na kukuta miguu imekatika.

$
0
0

Mmkazi wa Ludewa, Mkoani Njombe, Yohana Nkwera (54) anadai kukatika miguu katika hali ya kushangaza.
Yohana anasema katika maisha yake amekuwa ni mwenye hofu kubwa baada ya kukumbwa na tukio hilo la aina yake la kukatika miguu akiwa usingizini. Anasema hadi sasa haelewi namna hasa tukio hilo lilivyomtokea, kwani hakuhisi maumivu yoyote .
Anasema tukio hilo la aina yake lilimtokea mwaka 1992, lakini halikuwahi kuandikwa wala kutangazwa, badala yake ni watu wachache waliokuwa wakilifahamu.
Anasema siku hiyo usiku alikwenda kulala kama ilivyo kawaida, alipoamka asubuhi alikuta miguu yake imekatika.
Kilichomshangaza zaidi ni kwamba hapakuwa na damu wala jeraha lilionekana. Palionekana pana kovu, kana kwamba alikatika mguu muda mrefu uliopita.
Anasema mara ya kwanza ulianza kupotea mguu wa kulia, hiyo ilikuwa ni mwezi Machi, 1992. Kutokana na tukio hilo, ndugu zangu walifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufanya maombi katika nyumba mbalimbali za ibada, huku wengine wakienda kwa kuwaona waganga wa jadi.
“Kama binadamu wa kawaida ilichukua muda sana kuamini kilichotokea ndani ya maisha yangu na mguu wangu,” anasema.
Mwezi mmoja baadaye yaani mwezi Aprili mguu wa kushoto nao ulikatika katika mazingira yaliyo sawa na yale ya awali.Inaweza kuwa vigumu kuamini lakini ulimwengu ndivyo ulivyo.
Anakumbuka mazingira ya kukatika kwake yanahusishwa na imani za kishirikina kwa sababu siku chache zilizopita kabla ya kukumbana na dhahama hiyo aliwahi kukorofisha na mtu katika vilabu vya pombe za kienyeji anayesadikiwa kufanya tendo hilo.
Baada ya miaka saba kupita Yohana alipelekwa Hospitali Teule ya Ikonda wilayani Makete kupata huduma za tatizo lake. Alifanikiwa kupata msaada wa baiskeli ya magurudumu, ambayo aliitumia kwa miaka mitano.
Kwa sasa baiskeli hiyo haifanyi kazi kutokana na watu wanaosadikiwa kuwa ni wezi kuiba matairi na vyombo muhimu vinavyoiwezesha baiskeli hiyo kufanya kazi.
Pamoja na kupewa baiskeli hiyo na wasamaria wema, Yohana anakiri pia kuchongewa viatu na hospitali hiyo ambavyo vinamuwezesha angalau kutembea umbali mfupi.

Wauza ‘unga’ sasa wabuni mbinu mpya.

$
0
0

Wasafirishaji wa dawa za kulevya wamebuni mbinu mpya baada ya Kikosi cha Polisi cha Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kukamata kilo 3.5 za heroini zikiwa zimefungwa kwenye vifurushi zikipelekwa Monrovia, Liberia.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Kikosi cha Wanamaji cha Polisi kukamata jahazi likiwa na kilo 201 za heroini wakati likisafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar.
Mkuu wa Upelelezi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Hamad Hamad alisema jana kuwa kifurushi hicho kilikamatwa Jumatatu saa tisa alasiri, kwenye uwanja huo.
Hamad alisema mmiliki wa kifurushi hicho kilichokuwa kinasafirishwa na Kampuni ya Kusafirisha na Kupokea Mizigo (DHL) hajafahamika.
Kwa mujibu wa Hamad, mmiliki wa mzigo huo alikuwa ametumia jina la bandia pia maelezo ya mzigo ule yalikuwa ya uongo.
Hamad alisema dawa hizo zilikuwa zimeingizwa ndani ya kandambili huku zikiwa na vifurushi vingine kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Liberia.
“Kampuni ya DHL walipewa kazi ya kusafirisha mzigo huo na kujitetea kuwa hawakuelewa kulikuwa kitu ndani,” alieleza Hamad.
Hamad alisema kuwa polisi waliutilia shaka mzigo ule wakati ukipitishwa na kuamua kuukagua, ndipo wakakuta ni heroini.
Katika hatua nyingine, Kamishna wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema bado wanaendelea kuwahoji watu 12 raia wa nchi za Iran na Pakistan waliokamatwa juzi na kilo 201 za heroini.
Alisema pia wanaendelea kumchunguza raia wa Kenya, Abdulrahman Salim, ambaye alikamatwa na kete 142 za dawa za kulevya aina ya cocaine kwenye Uwanja wa JNIA.
Salim alikamatwa akitokea Brazil akiwa amepanda ndege ya Shirika la Ndege Ethiopia.
Mbinu zaidi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba ameelezea mbinu mbalimbali zilizobuniwa na wasafirishaji wa dawa za kulevya, zilizobainika baada ya watu saba walikamatwa katika matukio saba tofauti.
Dk Tizeba alisema hata vitabu vimekuwa vikitumika ambapo wahusika wamekuwa wakikata katikati ya vitabu hivyo na kuweka kete za dawa za kulevya kabla hawajavisafirisha nje ya nchi. Hata hivyo jambo hilo sasa wamelishtukia na udhibiti umeongezwa katika viwanja vya ndege.
“Hivi karibuni tumekamata kitabu cha somo la baiolojia kikisafirishwa kwenda Liberia na kilitiliwa shaka na kilipofunguliwa kilikutwa na kilo mbili za dawa za kulevya,” alisema.
Alisema wameamua kusafarisha kwa njia hiyo baada ya kuona mpango wa kumeza umedhibitiwa na hadi sasa wahusika wa matukio hayo saba wamekamatwa, na mmoja bado ila huenda akatiwa mbaroni wakati wowote.

“Saba tunao kwa mahojiano na mwingine ambaye anahusika na kitabu hicho cha baiologia anafuatiliwa,” alisema.

Mchungaji afungwa kwa ubakaji.

$
0
0

Kiongozi wa kanisa moja nchini Zimbabwe amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa kosa la kuwabaka wanawake watatu na kukutwa na vifaa vya kuchochea kujamiiana.
Kiongozi huyo, Martin Gumbura (57) wa Kanisa la RMG Independent End Time Message alitiwa hatiana katika makosa manne ya ubakaji kwenye mahakama ya mjini Harare. Gumbura ana wake 11 na watoto 30 na aliiambia mahakama kwamba alikuwa akitarajia kupata watoto 100 katika maisha yake.
Wake zake wote walikuwa wakihudhuria mahakamani hapo wakati wa kesi hiyo na walikuwa wakijumuika na watu wengine waliokuwa wakihudhuria makahamani hapo hadi siku hukumu ilipotolewa.
Alihukimiwa kifungo cha mika 50 jela lakini miaka 10 imepungizwa katika adhabu hiyo baada ya kuonyesha tabia njema wakati wa kesi hiyo.
Hukumu nyingine ya kifungo cha miaka minne jela kwa kukutwa na vifaa vya kuchochea kujamiiana itatumikiwa sambamba na hukumu hiyo ya kifungo cha miaka 40. Waendesha mashtaka waliiomba mahakama kwamba Gumburu anatakiwa ahukumiwe kifungo cha miaka 25 jela kwa kila kosa, lakini hakimu alieleza kwamba hana mamlaka ya kutoa hukumu ya kifungo cha muda mrefu namna hiyo.
Hakimu huyo alimwelezea Gumbura kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo ambaye amekuwa akiwaghilibu waumini wa Kanisa hilo.
“Mahakama imejaribu kutoa adhabu ambayo itawatendea haki wote, malalmikiwa na walalamikaji. Mtuhumiwa hutu ni kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo,” alisema.
“Msingi wa huduma ya Kanisa ni kumwabudu Mungu na si kuzini na mabinti na wanawake na kuwatishia kwamba kwa kutofanya hivyo watapatwa na balaa,” aliongeza hakimu huyo.
Alisema ni wajibu wa wachungaji na wasimamizi wa kanisa kujua kuhusu madhila yanayowakumba waumini wao, pia kujua udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia unaowakumba wanawake na kutafuta namna ya kuukemea.
Awali Gumbura alikuwa akikabilwia na mashtaka tisa ya kuwalaghai na kuwabaka wanawake sita lakini alifutiwa mashtaka manne yaliyowahusisha wanawake watatu kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.
Hivi karibuni, mtu mwingine mjini Harare alihukumiwa kifungo cha miaka 290 jela kwa kosa la kuwadhalilisha na kuwabaka wanawake 13. Mtu huyo, Thomas Chirembwe (30) alitiwa hatiani kwa makosa 21 ya ubakaji na ujambazi wa kutumia silaha baada ya mfululizo wa matukio yaliyoutikisa mji wa Harare.
Kwa mujibu wa takwimu za polisi, zaidi ta watoto 400 walibakwa na wanawake 392 walinyanyaswa kijinsia mwaka 2013, ambapo wanawake walibakwa wakiwa njiani na watoto wengi walibakwa na majirani au watu wao wa karibu.

TAHADHARI:SIKU HIZI KUNA BIASHARA ZA MAFUMANIZI...WANAUME KUWENI MAKINI.

$
0
0

Nawatahadharisha,
kuna rafiki yangu baada ya kupigika na maisha toka mwaka juzi akapata wazo la kuanzisha biashara ya mafumanizi.


Ameajiri wadada 5 kinachofanyika anawatumia hao wadada kuandaa mafumanizi. Mkikubaliana na wadada yeye anakuja na watu wacamera na mabaunsa 2 kufumania pia watakutaka utoe pesa.

Ukitoa pesa anazotumia kulipa mishahara kwa kila mwezi kama faida yake hakosi million 5.

Huu ni mwaka wa pili sasa hivi amejenga na ana gari 2 za kutembelea pia ameoa.

Elimu yake ni kidato cha nne tu na wana ofisi kabisa. Makazi yao ni Dar lakin uwa wanasafiri adi mikoani.

Uwa wanatoza pesa kulingana na mtu alivyo. Wanatoza kuanzia laki 5 adi million 10.

Mbaya zaidi wanakupiga na picha hivo lazima utatoa pesa.

Mnaopenda wanawake wa barabaran kazi kwenu.

Source:Jamii Forums

MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AMUUA ASKARI POLISI KWA JIWE WAKATI AKIMPELEKA MAHABUSU.

$
0
0

Askari polisi F. 5264 PC Sabato (37) wa Kituo cha Polisi cha Longido, wilayani Monduli, ameuawa kwa kupigwa jiwe na mtuhumiwa aliyekuwa akimpeleka mahabusu katika Gereza la Kisongo.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema mauaji hayo yamefanywa na mtuhumiwa aliyekuwa akipelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya kuvunja na kuiba.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, kesi hiyo iko katika Mahakama ya Wilaya ya Longido.

“Baada ya kufika njia panda ya Gereza la Kisongo, mtuhumiwa alimwomba PC Sabato amfungue mkono ili ajisaidie haja ndogo, lakini alipofunguliwa, ghafla aliokota jiwe na kumpiga askari huyo kwenye paji la uso, akaanguka na kuzimia,” alisema Kamanda Sabas.

Kamanda Sabas alisema kwa mujibu wa waendesha bodaboda walioshuhudia tukio hilo, baada ya askari kuanguka chini, mtuhumiwa alitumia pingu aliyokuwa amefungwa mkononi, kuendelea kumshambulia kabla ya kutimua mbio.

Alisema hata hivyo waendesha bodaboda waliamua kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Kamanda huyo alisema kitendo hicho kilifuatiwa na kutoa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege na baada ya muda, askari walifika na kumchukua pamoja na majeruhi ambaye hata hivyo, alifariki dunia usiku wa kuamkia jana, katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.

Kwa mujibu wa Sabas, polisi wanaendelea kumhoji mtuhumiwa kabla ya kupandishwa kizimbani kwa shitaka la mauaji. 


Credit:Udakuspecially.

KIGAUNI CHA MSANII LULU CHALETA SHIDA..

$
0
0
Siku za karibuni Lulu Alionekana mitaa ya Sinza na Kigauni hicho iliyopelekea watu kujiuliza Maswali kama kweli Bi Dada Amebadilika kama alivosema..


Utata huo umekuja baada ya watu kuhoji kama kweli amevaa nguo ya ndani ...Ebu Mdau Angalia hiyo picha vizuri na Wewe uniambie hiyo staili ni Aje? 

MTEGO WA KUJIUZA WAMBADILI BABY.

$
0
0

BAADA ya mwanamuziki Baby Joseph Madaha kunaswa na mtego wa kujiuza uliotegwa na gazeti
hili hivi karibuni, mdada huyo anaonekana kubadilika na anadai mgogoro uliojitokeza kati yake na meneja wake, Joe Kairuki kutokana na tukio hilo umekwisha.


Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni msanii huyo ambaye ni kati ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri alisema, tukio lile limefanya ajifunze kitu na kubadilika kwake kumesababisha bosi wake amsamehe na waendelee kupiga mzigo.

“Kweli nimejifunza kutokana na makosa maana kunaswa kwenye ule mtego kumenigharimu sana lakini nashukuru nimesamehewa na mkataba ninaendelea nao, yale yamepita na sasa ni kazi tu,” alisema Baby Madaha a.k.a The Queen of Swaga.


Credit:GPL

KIFO CHA KANUMBA-LULU KESI UPYAA.

$
0
0

Stori:RICHARD BUKOS
KAZI inaanza tena! Supastaa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anapanda katika kizimba cha Mahakama Kuu ya Tanzania kwa yale
madai ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa nyota wa muvi nchini, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Risasi Jumamosi limeambiwa.

Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, mtoa habari ambaye aliomba hifadhi ya jina alisema kuwa, Februari 17, mwaka huu, staa huyo atatakiwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake kuanza huku akisema, kuna mabadiliko kidogo katika kusikilizwa kwa kesi hiyo.

ITAKUWAJE?
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, Lulu mwenye umri wa miaka 18, atasomewa upya mashitaka dhidi yake ambapo atatakiwa kujibu tena kama anakubali aliua bila kukusudia au la!
“Elizabeth (Lulu) atasomewa upya mashitaka ya kumuua Kanumba bila kukusudia. 
“Ataulizwa ni kweli au si kweli? Atatakiwa kujibu swali moja kati ya hayo mawili, kama ni kweli atasema kweli kama si kweli atasema si kweli,” kilisema chanzo hicho huku kikisisitiza jina lake lisichorwe gazetini.

MUDA WA KESI SIKU 730
Habari zaidi zikadondokea Dawati la Risasi Jumamosi na kusema kwamba, kesi hiyo itaendeshwa kwa siku mia saba na thelathini (730), kwa maana ya miaka miwili hadi hukumu itakapotolewa.

NI NDANI YA SHERIA MPYA
Katika Siku ya Sheria Duniani iliyoadhimishwa jijini Dar es Salaam, Februari 3, mwaka huu, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman alisema kuanzia sasa kesi zote za jinai zitatakiwa kumalizika katika kipindi cha miaka miwili.
Kesi ya Lulu nayo ni ya jinai na kwa sababu hiyo, hadi Februari ya mwaka 2016 itatakiwa iwe imemalizika.

WAKILI WAKE
Chanzo hicho kililithibitishia gazeti hili kwamba, Lulu atatetewa na yuleyule wakili wake mwenye ‘ngekewa’ ya kuwatetea watu maarufu nchini, Peter Kibatala.

Kibatala ameshawahi kuwa wakili wa Mbongo Fleva, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ katika kesi ya madai ya kuiba ‘power window’ za gari la msanii mwingine wa Bongo Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.

Pia aliwahi kumwakilisha wakili mwezake, Mabere Nyaucho Marando kwenye kesi ya Mbongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ alipoburuzwa kortini na uongozi wa Clouds Media Group baada ya Marando kuwa na udhuru.

Ilibaki kidogo awe wakili wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu katika kesi ya kumpiga makofi meneja wa hoteli moja (jina tunalo) iliyopo Kawe Beach, Godluck Kuyumbu lakini akakosa sifa baada ya shauri hilo kusiklizwa Mahakama ya Mwanzo Kawe, Dar.

HAWA HUENDA WAKAITWA
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, katika kesi hiyo huenda wakaitwa watu ambao watasaidia kutoa ushahidi.
Watu hao ni wale waliokuwa na ukaribu na marehemu, hasa siku ya tukio au kushirikishwa kwa namna moja au nyingine kwa jinsi ambavyo waendesha mashitaka wataona.

DOKTA KIDUME
Aliyekuwa akimtibu Kanumba, Dokta Kidume anaweza kufika mahakamani hapo kwa sababu ndiye aliyekuwa mtu wa pili  kufika kwenye chumba cha marehemu mara baada ya kuanguka.

ETH BOSCO
Huyu ni ‘mdogo’ wa marehemu Kanumba, yeye siku ya tukio alikuwa nyumba moja na marehemu, ila vyumba tofauti. Ndiye aliyemwona Kanumba akiwa katika hali mbaya baada ya kutoelewana na Lulu na kukimbia kumwita Dokta Kidume.  

Hawa wote walishahojiwa na Jeshi la Polisi Tanzania katika Kituo cha Oysterbay, Dar, mara baada ya kifo hicho. Seth alihojiwa mara tano.

TUJIKUMBUSHE
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam. Kifo chake kilidaiwa kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa na hivyo kuufanya ubongo kutikisika (brain concussion).

Hata hivyo, baadaye ilifahamika kuwa, sehemu ya maini na majimaji ya machoni vilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kulikuwa na sumu au kitu kingine katika mwili wa Kanumba. Majibu hayajatoka hadi leo.

WAKILI KIBATALA
Risasi Jumamosi lilimsaka Wakili Kibatala kwa njia ya simu ili kumsikia alichonacho kufuatia kesi ya mteja wake kuanza kusikilizwa ambapo alisema:
“Tutakutana mahakamani jamani, kwa sasa niko bize sana.”

LULU
Juzi, simu ya Lulu ilipigwa kwa muda mrefu lakini haikupokelewa huku baadhi ya watu wake wa karibu wakisema kuwa, staa huyo ameasisi tabia mpya ya kutopokea simu zenye namba ngeni machoni mwake.
Source:Global Publishers

STEVE NYERERE UENYEKITI WA BONGO MOVIES WAANZA KUMTOKEA PUANI.

$
0
0

Steve Nyerere Amesema Inamuwia vingumu kufanya kazi kutoka na kukosa ushirikiana kutoka kwa wana bongo Movies wenzake.


Amehabarisha kuwa kuna baadhi walio mchagua kuwa mwenye kiti wao ili wamzalilishe na kuona kama ataweza , na hilo analiona sasa kwani kuna baadhi waliomchagua wananyima ushirikiano.... 

WEMA SEPETU SASA ARUHUSU MATUSI,ASEMA HATA UMTUKANE VIPI HAUMII,SO KEEP ON.

$
0
0
Mchumba wa Diamond Platnumz Wema Sepetu Ameamua kuwatolea makavu wale wote wanao penda kumtukana kwenye mitandao hasa Instagram
...Jisomee Mwenye Alicho Andika hapa chini ..Kama wewe ni mmoja wapo basi Ukomeeeezzz.......lol



Jamaa Huyu Ana Miaka 29 na Tayari Ana Mjukuu.

$
0
0

Jamaa mwenye umri wa miaka 29 aitwaye Shem Davies ni mtu ambaye hana kazi kwa sasa, ila ameweka historia ya kuwa mtu kijana zaidi kuwahi kupata mjukuu kwenye historia ya Uingereza, mara baada ya mtoto wake wa kike mwenye miaka 14, Tia Davies,  mapema mwezi huu kujifungua mtoto wa kike na mpenzi wake, Jordan Williams, ambaye ana mika 15 tu.
Picha zaidi angalia hapo chini....

Wazazi wapya Tia, Jordan na mtoto Gracie

Familia yenye furaha: Jordan, kushoto chini,  Tia na Gracie,
sambamba na babu na bibi Shem na Kelly

Baba Amrusha Mtoto Wake wa Kike Toka Gorofa ya 3 Baada ya Kumfuma na Mvulana Chumbani Kwake.

$
0
0
Baba mmoja mwenye hasira, Deji Kamoru, hivi sasa yupo kwenye mtatizo makubwa kutokana na kitendo chake cha kumrusha mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 14, Aishat toka gorofa ya tatu mara baada ya kumfuma akiwa na mpenzi wake kwenye chumba chake cha kulala.


Imeelezwa, mwanzoni aliifunga kwa kamba mikono ya Aishat, kumtesa na mwisho kumtupa toka kwenye gorofa ya tatu nyumbani kwao Mtaa wa Oroyinyin, Kisiwa cha Lagos, Jimbo la Lagos, kusini magharibi mwa Nigeria.

Vyanzo viligundua kwamba wakati Aishat alipotua chini, aligonga kichwa chake kwenye kitu chenye ncha kisha akapoteza fahamu.

Binti huyo alikimbizwa Hospitali ya Lagos Island General iliyopo jijini Lagos ambapo kwa sasa yupo chumba cha watu mahututi.

Ikulu ya Marekani Chini ya Ulinzi Mkali Mara Baada ya Kukamatwa kwa Jamaa Aliyejaribu Kuruka Uzio Wake.

$
0
0
Ikulu ya Marekani imekuwa chini ya ulinzi mkali mara baada ya mtu asiyetambulika alipokamatwa akijaribu kuruka uzio wa Ikulu hiyo mnamo siku ya Ijumaa mchana.

Maafisa wa usalama wa nchi hiyo walimkamata jamaa huyo na hivi sasa yupo ndani. Mtu huyo inasemekana alikuwa amebeba mabegi mawili makubwa ila maafisa hawajatoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo.

Balotelli Kwenye Mtindo Mpya wa Nywele.

$
0
0
Mchezaji wa timu ya taifa ya Italia na mshambuliaji wa timu ya AC Milan, ambaye hivi karibuni alikuwa
akihusishwa na uhamisho wa kurudi tena kucheza kwenye Premier League juzi kati kupitia ukurasa wake wa Instagram alionyesha mtindo wake mpya wa nywele.

Mario sio mtu wa kuwa nje ya vyombo vya habari kwa muda mrefu maana hata vituko na hata aina ya mitindo ya nywele zake ni habari tosha kwa jamii.

Mcheki zaidi kwenye picha hapo chini....






Viewing all 2632 articles
Browse latest View live