↧
Bwana Misosi ft Mataaluma-Happy Day Iko Hapa.Aja Kivingine Baada ya Kimya Kingi.
↧
TFF Wanataka kubadili jina la Taifa Stars.

Katika kipindi cha maswali na majibu kilichofanyika jumanne iliyopita, TFF kupitia Raisi wake ilisema kwamba taratibu za mwanzoni tayari zimeanza.
Utaratibu mzima utahusisha jamii. Umma utatumika katika kutoa mawazo ya jina jipya kupitia SMS.
Suala la kutaka kubadili jina kwa hakika litaleta mjadala kwenye jamii. Kwa muda mrefu kumekuwepo na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiliponda jina hilo wakisema limekaa kitaratibu na halitishi.
↧
↧
WASTARA AFUNGUKA NA KUSEMA 'NIKIKUMBATIWA NAKUWA HOI''

Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu, Wastara Juma amefunguka kuwa starehe yake kubwa duniani ni kukumbatiwa na anapofanyiwa kitendo hicho na mtu wa jinsia yoyote huwa hoi.
Akistorisha na paparazi wetu, Wastara alisema: “Mimi napenda sana kukumbatiwa au kukumbatia, awe ni mwanaume au mwanamke, ndugu yangu au hata kama siyo ndugu yangu, tukikumbatiana tu najisikia raha sana.
“Unajua kila mtu anakuwa na kitu anachokipenda duniani sasa mimi starehe yangu ndiyo hiyo hata marafiki zangu wanajua kwamba mimi napenda kukumbatiwa.
Source:Global Publishers
>>Gonga Like Yako Hapa Kwa Mastory Kibao>>
↧
JACK WOLPER"TOKA NIWE NA HUYU MCHUMBA MPYA NIMEKUWA NA FURAHA MUDA WOTE"
Na Mayasa Mariwata
THE Ijumaa Sexiest Girl 2012, Jacqueline Wolper amesema kuwa, ana imani kubwa na mpenzi wake wa sasa aliyemtambulisha kwa jina la G Modo
akiamini atampoza machungu aliyoyapata kutoka kwa mpenzi wake wa zamani, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ huku akiwatahadharisha mashosti zake kutoleta shobo (kuwa mbali naye)
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Wolper alisema anafikia hatua ya kusema hayo kwa kuwa muda mfupi aliokuwa naye amegundua ni mwanaume anayejitambua na anayeheshimu mapenzi ila akawataka mashosti zake kutomsogelea.
“Tangu niwe na huyu kijana nimekuwa ni mwenye furaha kubwa, nasahau hata yale machungu niliyopata kwa mpenzi wangu wa zamani. Lakini najua wapo wanaomtolea macho, tusitafutane ubaya, kila mtu na maisha yake,” alisema Wolper.

KILIO CHA MAMA WA MAREHEMU SHARO MILIONEA KWA WAANDAJI WA MOVIE BONGO.
Ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu kufariki kwa Sharo Milionea,Mama mzazi wa Marehemu Sharo Milionea amekuja na ombi kwa ajili ya waandaaji wa Movie za kitanzania hapa nchini.
Ombi hili ni juu ya kazi mbalimbali alizowahi kufanya marehemu Sharo Milionea na hazikutoka enzi ya uhai wake ambapo mama ameomba kuzisimamisha kazi zote ambazo hazijatoka na marehemu Sharomilionea alishiriki,mpaka wawasiliane na familia hiyo.
Mama mzazi wa marehemu Sharo Milionea ameingia Dar es salaam jumapili,January 26 akitokea nyumbani kwake Kijiji cha Msanga wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga mahsusi kwa ajili ya kuipromote movie itakayoonyesha maisha ya Sharo Milionea.
Wahusika kwenye movie hiyo ni pamoja na Mama mzazi huyo pamoja na wanafamilia wa Sharo Milionea ambapo ndani ya movie hiyo ya maisha ya Sharo Milionea wameigiza tangu amezaliwa hadi alipofariki November 26 2012 kwenye ajali ya gari.

HUYU NDIO MTANGAZAJI WA RADIO ALIYEFARIKI LEO.

Marehemu Kenneth Kidago Lyanga enzi ya uhai wake.
Mbunifu Msaidizi na Mtangazaji wa Habari za Michezo wa East Africa Radio Kenneth Kidago Lyanga amefariki dunia nyumbani kwake Mwenge Mlalakua, Jijini Dar es Salaam.
Mipango ya mazishi ya Kenneth Lyanga inafanywa na familia yake. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Kenneth Kidago Lyanga Mahala Pema Peponi, Amina.
↧
MWANAUME ALIYEDAIWA KUFARIKI "AMEFUFUKA" NA KISHA KUFARIKI TENA.

MARAFIKI wa mwanamume ambaye alikuwa amedaiwa kufariki walipigwa na butwaa na kutoroka baada ya mwanamume huyo kugunduliwa kuwa alikuwa hai katika ufuo wa Machakos Level Five leo adhuhuri.
Polisi walikuwa wamepata mwili wa mchuuzi huyo anayedaiwa kuwa wa umri wa miaka 45 katika mtaro kwenye kituo cha mabasi cha Machakos.
Walifululiza hadi kwenye mochari wakiandamana na marafiki zake lakini wahudumu walipouchunguza ‘mwili’ wakagundua kwamba mchuuzi huyo alikuwa anapumua.
Wahudumu hao walimkimbiza hadi kwenye wodi iliyo karibu na akawekwa mirefeji ya kupumua, kupewa dawa na kuongezwa maji mwilini. Madaktari walisema alikuwa amedhoofika kiasi kwamba hangeweza kupata tena fahamu. Baadaye alifariki mwendo wa saa nane.
Marafiki zake walijawa na huzuni mwili wa mchuuzi huyo ulipokuwa ukipelekwa kwenye mochari mara ya pili. Jina la mwanamume huyo halikutolewa, huku madaktari wakisema wanasubiri jamaa zake wafahamishwe rasmi kuhusu kifo chake.
Marafiki zake waliohojiwa na KNA walisema marehemu alipokuwa hai alikuwa amelalamika kwamba alikuwa anahisi maumivu makali kifuani. Walisema mchuuzi huyo alikuwa ameonywa dhidi ya kunywa pombe kupindukia kwa sababu alikuwa na matatizo ya kiafya.
Walisema alikuwa amelala mtaroni kwa zaidi ya masaa sita baada ya kunywa pombe.
↧
Wimbo mpya wa Ngwair 'Alma' kuachiwa rasmi siku ya Valentine mwaka huu, una story ya kweli.

Akiongea na tovuti ya Times Fm, Muro ambaye ni moja kati ya wasimamizi wa kazi za Albert Mangwea ambaye anaisimamia project ya wimbo huo, amesema kuwa wimbo huo uliorekodiwa ndani ya AM Records chini ya producer Manecky utaachiwa rasmi siku ya Valentine na kwamba anaendelea kuwasiliana na familia yake kuhusu mapato ya wimbo huo ambayo atapewa mama yake Ngwair.
“Yeye alitaka kuitoa ngoma hiyo siku ya Valentine mwaka jana, kwa hiyo na mimi nimeamua kuitoa siku hiyo hiyo. Niliongea na Familia Morogoro, na ntawapigia tena ili tuangalie tunachofanya kwa sababu kuna vitu vingi vya kuconsider, kuna mambo ya ringtones na nini na nataka nizungumze pia na makampuni ya simu. Kwa sababu kila alichotakiwa apate yeye (Ngwair) inabidi apate mama yake.” Muro ameiambia tovuti ya Times Fm.
Muro ameeleza kuwa wimbo huo wenye ujumbe wa mapenzi unazungumzia story ya kweli na ulikuwa maalum kwa mtu wa karibu wa marehemu Ngwair, “Kila kitu alichokuwa anakiimba kilikuwa cha ukweli, ni true story.”
January 16, 2013, Ngwair mwenyewe alitangaza kuwa ataachia wimbo huo siku ya Valentine (February 14, 2013) ambao alidai ni zawadi ya Valentine kwa fans wake na wimbo huo ulikuwa kwenye album yake iitwayo MIMI 3, lakini baadae aliahirisha na kuachia wimbo wa ‘Beef’ akiwa na TID.
Muro amesema kuwa kuna matatizo yalitokea wakati huo ambayo marehemu Ngwair hakupenda kuyazungumzia ambayo yalisababisha yeye kuahirisha kutoa wimbo huo.
Usikose kusikiliza kusikiliza The Jump Off ya 100.5 Times Fm leo kwa undani wa habari, ambapo utamsikiliza Muro akifafanua.
↧
ASKARI POLISI WATANO WAFARIKI DUNIA PAPO HAPO KWA AJALI YA GARI MKOANI DODOMA.
Gari hilo lililopata ajali na kuua askari hao.
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Askari polisi watano mkoani dodoma wafariki dunia papohapo katika ajali ya gari iliyotokea 31/01/2014 majira ya 23.45 hrs katika barabara kuu ya Dodoma – Morogoro eneo la Mtumba Center, Kata ya Mtumba Tarafa ya Kikombo Manispaa ya Dodoma, ambapo gari namba T.770 ABT Toyota Corolla lililokuwa likiendeshwa na Askari namba H. 3783 PC DEOGRATIUS wa Polisi Wilaya ya Kongwa likitokea Dodoma mjini likielekea Wilayani Kongwa liligongana uso kwa uso na gari namba T.997AVW Scania Bus mali ya Kampuni ya Mohamed Trans lililokuwa likiendeshwa na JUMA s/o MOHAMED, miaka 38, Mkazi wa Mwanza, likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma na kusababisha vifo kwa askari watano papohapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewataja Askari hao waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni:-
1. D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye miaka 51, Mgogo.
2. F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye miaka 34, Muha.
3. H.3783 PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
4. WP.10337 PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
5. WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye miaka 20, Mhehe.
Wote ni askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.
Kamanda MISIME amesema chanzo cha ajali hiyo kulingana na uchunguzi wa awali ni mwendo kasi kutokana na uharibifu uliotokea kwa gari dogo walilokuwa wamepanda askari na jinsi lilivyoburuzwa na basi kwa umbali wa mita 56 kisha kwenda kusimama umbali wa mita 97, kwa hali hiyo umbali kutoka eneo walipogongana hadi basi liliipoenda kusimama ni mita 152.
Dereva wa Bus alitoroka mara baada ya ajali hiyo kutokea, juhudi za kumtafuta zinaendelea. Miili ya maerehemu imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya mkoa Dodoma.
Aidha Kamanda MISIME ametoawito kwa madereva kila mara wawe na udereva wa tahadhari na na kuzingatia sheria za usalama barabarani.
CREDIT : VIJIMAMBO BLOG
CREDIT : VIJIMAMBO BLOG
↧
↧
HUYU NDIO MTANGAZAJI WA RADIO ALIYEISABABISHIA KITUO CHAKE KUPIGWA FAINI.
Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) imekitaka kituo cha Radio Times FM ya Dar es salaam
kuomba radhi mfululizo siku tatu na kumlipa tsh 500,000 msanii wa Taarab, Karya Temba baada ya mtangaji wake, Dida kupitia kipindi cha ‘Mitikisiko ya Pwani’ kumshambulia binafsi msanii huyo.
Kamati imesema mtangazaji Hadija Shaibu maarufu Dida aligeuza kipindi anachorusha redioni hapo kuwa cha ugomvi binafsi kati yake na mlalamikaji ambaye ni Karya na kwamba alichochea wasikilizaji kutuma meseji za kejeli kwa mlalamikaji jambo ambalo sio lengo la usajili wa kituo hicho.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo wakati akifafanua juu ya malalamiko ya msanii huyo akidai kipindi hicho kilimdhalilisha na kumharibia sifa kama mwanamuziki.
Jaji Mihayo alisema baada ya kamati kusikiliza pande hizo mbili, inaagiza redio hiyo kumwomba radhi mlalamikaji kupitia kipindi hicho katika vipindi vitatu mfululizo kuanzia Februari 5 na maudhui ya radhi hiyo yataridhiwa na MCT.
Alisema kituo hicho, pia kimlipe mlalamikaji Sh 500,000 kama gharama za kutayarisha malalamiko na kimuandikie barua ya kumwomba radhi ndani ya wiki moja kuanzia jana na nakala kutumwa MCT. Katika shauri hilo namba 28, 2013, Temba analalamika kushambuliwa, kukashifiwa na hata kubaguliwa na mtangazaji huyo katika kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani anachokirusha redioni hapo.
Vile vile Kamati hiyo imesema redio hiyo ilikiuka maadili ya utangazaji kwa kurusha kipindi kinachoshutumu watu kwa kutumia kabila lao na kilikuwa na maudhui ya udhalilishaji wa kijinsia, kinyume cha maadili na kanuni bora za uanahabari.
Chanzo:Udakuspecially.

MARLOW ALIA NA VYAMA ZA SIASA.ADAI KUSHUKA KIMUZIKI NA PIA KUAPA KUTOSHIRIKI TENA KATIKA KAMPENI ZA KISIASA.

Msanii aliyepata kuvuma sana kabla ya mwaka 2010 alimaarufu kwa jina la Marlaw, amejutia uamuzi wake
wa kukipigia kampeni chama cha ccm kwani kimemporomosha kimuziki.
"Unajua mimi mwaka 2010 nimeburudisha ktk kampeni za ccm lakini nimeambulia kushuka kimuziki sijui ni siasa imehusika au la kwa sababu toka hapo nimetoa nyimbo nyingi lakini hazivumi tena, sasa sitaipigia ccm tena labda chama kingine si unajua vijana wako wapi mzee ha ha haaa si kwamba nimejitoa ccm hapana mi ni msanii naburudisha watu wote"
Mwananchi lilipotaka kujua ni chama gani amekilenga kukipigia kampeni kwa malipo alisema bado muda wa kukiweka hadharani.
Wasanii someni alama za nyakati msije jikuta mko njia panda kimuziki huu ni mfumo wa vyama vyama vingi.
chanzo:Mwananchi.
↧
MAMA JOHARI AMFUMUA RAY NA KUMCHAMBUA KAMA KARANGA.

Kwa mara kwanza mama mzazi wa mwigizaji mkongwe Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ambaye
hakupenda jina lichorwe gazetini ameibuka na kumfumua staa wa filamu ‘mbia’ wa mwanaye, Vincent Kigosi ‘Ray’, Risasi Jumamosi lina cha kushika.
Akizungumza na mapaparazi wetu katika mahojiano maalum nyumbani kwake, Ubungo External, Dar, wiki hii, mama Johari alifunguka kuwa hamjui wala hajawahi kumuona Ray ambaye ni mkurugenzi mwenza wa Johari. Ndiyo wamiliki wa kampuni ya kufyatua filamu ya RJ Productions.
Mama Johari ambaye pia ana makazi yake mkoani Shinyanga alisema alitua jijini Dar kwa matibabu ya presha.
Baada ya kumjulia hali, mapaparazi wetu walitaka kujua mama huyo anamzungumziaje Ray ambaye amekuwa akifanya kazi kwa karibu na bintiye na kwamba ilishasemekana ni wapenzi.
Ndipo mama huyo alipokuja juu akisema huyo Ray mwenyewe hamjui na hajawahi kumtia machoni zaidi ya kumsikisikia tu kama wengine.
“Mimi simjui huyo Ray na wala sijawahi kutambulishwa wala kuonana naye, kwanza siishi hapa nitamuonea wapi, nimekuja zangu kutibiwa tu kutokana na matatizo yangu ya presha na kisukari.”
“Kwanza mwanangu hana muda wa kukaa na kumuumizia kichwa huyo Ray kwani yeye ni baba yake?
“Hata siku moja (Johari) hawezi kuishi kwa kumtegemea yeye (Ray),” aliongeza mama huyo.
Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, mama huyo alisema kamwe hawezi kuumiza kichwa kuingilia mambo ya mwanaye, kwa kuhofia maradhi aliyonayo na kujitia matatizoni kwa mambo asiyoyajua undani wake.
Alisema anamshukuru Mungu kutokana na hali ya mwanaye aliyekuwa anaumwa kupata ahueni na kundelea na kazi zake.
Alipotafutwa Ray ili kuelezwa kile alichokisema mama Johari, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Source:Global Publishers
↧
Afande Selle Aunga Mkono Kauli ya Obama Kwamba Kuvuta Bangi ni Salama Kuliko Kunywa Pombe.
Afande Sele ameungana na Rais wa Marekani Barack Obama katika kuunga mkono kauli yake ya kwamba bangi ni salama kuliko pombe kwa afya ya binadamu.
Akiongea na kipindi cha Milazo XP kinachorushwa na TBC fm, Afande Selle, mbali na kuunga mkono pia alizungumzia umuhimu wa bangi kama zao linaloweza pia kuwa na manufaa kwa uchumi wa nchi kama litatumiwa kwa usahihi.

KIJANA WA MIAKA 28 ALIYEFUNGA NDOA NA MBUNGE WA MIAKA 60 AELEZEA SABABU 7 ZA KUAMUA KUIVUNJA NDOA HIYO.
YULE ‘hendsam’boi’ Michael Christian (28) ambaye mwaka jana aliitikisa medani ya siasa Bongo kufuatia kufunga ndoa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila (60) na miezi michache mbele ndoa ikavunjika, ameibuka na kuanika siri 7 zilizomfanya aamue kuivunja ndoa hiyo na mheshimiwa huyo.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar, juzi, Michael alibainisha mambo hayo huku akisema anajuta kwa tukio lile ambalo bado halijamtoka kichwani hadi sasa.

SIRI YA KWANZA
Kijana Michael aliianika siri ya kwanza kwamba ni kuchekwa na marafiki zake wa Bagamoyo mara baada ya kugundua amefunga ndoa na mbunge huyo ‘mzee’.
“Marafiki zangu walianza kunicheka, walisema nimefunga ndoa na mbunge mzee, mama mtu mzima. Nikaanza kujisikia vibaya jambo ambalo sikulipenda hata kidogo,” alisema kijana huyo ambaye ni yatima.
SIRI YA PILI
Akizungumza kwa hisia kali, Michael aliye na taaluma ya uuguzi, aliiweka wazi siri ya pili ya kuamua kuivunja ndoa yake na mheshimiwa huyo kuwa ni kitendo cha kutokuwepo kwa tangazo la ndoa la siku 21 kama sheria ya nchi inavyotaka.
Kuna kifungu cha sheria kinachotaka wachumba wanapotaka kufunga ndoa kutolewa tangazo la siku 21 kwenye mamlaka za kufungisha ndoa hiyo ili kama mmoja wa wahusika ana ndoa inayoishi (halali) aweze kuwekewa pingamizi la kufungishwa ndoa.

SIRI YA TATU
Kijana huyo aliendelea kwa kuifunua siri ya tatu kuwa ni kitendo cha kufungishwa ndoa bila kuwepo na mashahidi wa pande zote mbili (matroni na patroni) walioandaliwa zaidi ya kuitwa papohapo.
Alimtaja kwa jina moja Mchungaji Mtetumo wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God ‘Mlima wa Moto’ kuwa ndiye aliyesimamia kufungwa kwa ndoa hiyo, Septemba Mosi, 2011 ndani ya ofisi huku milango ikiwa imefungwa.
Alisema pia kwamba, suala la ndoa aliligundua siku hiyohiyo baada ya kufika kwenye kanisa hilo ambapo maandalizi mengine yote yalishafanyika akiwa hajui.
SIRI YA NNE
Siri zilizidi kubanjuliwa, Michael alisema sababu ya nne ambayo pia ilimsukuma kuamua kubatilisha ndoa yake na mama Kasikila ni baada ya kubaini kwamba, hataweza kupata uzao kwa mke huyo kwa sababu ana watoto wakubwa kiumri kuliko yeye.
“Nilijua sitapata watoto, hakukubali kuzaa na mimi kwa sababu tayari ana watoto wakubwa, mimi mdogo, ingekuwa vigumu. Kifupi haikuwa ndoa halali kwangu,” alisema kijana huyo.
SIRI YA TANO
Michael: “Alianza kunibana sana, kila hatua ya miguu yangu alitaka kujua inakwenda mpaka wapi! Hii hali nikaiona inanipiga pingu, nikagundua kuwa kumbe mimi sijaoa, bali nimeolewa. Yule mama alinioa mimi, si kwamba mimi nilimuoa yeye, nikasema ili niwe na amani ya moyo ni lazima ndoa ivunjike.”
SIRI YA SITA
Kijana huyo hakuona sababu ya kubakiza siri hata moja, akaendelea kuzianika:
“Jambo jingine ambalo pia lilichangia kuamua kuivunja ndoa ile ni baada ya kukumbuka historia ya kukutana kwetu.
“Wakati nipo Hospitali ya Bagamoyo na yeye akiwa pale kama muuguzi mkuu, tulizoeana. Kuna siku aliniita kwake akasema anasafiri anaomba nimwangalizie nyumba, nilikuwa na rafiki yangu tukawa tunalala pale mpaka aliporudi.
“Kuzoeana kuliendelea, mwishowe tukawa wapenzi mpaka ndoa. Nilipokumbuka hivyo tu nikagundua kuwa aliniingiza mapenzini kwa hila au mbinu, hilo pia sikulipenda,” alisema Michael.
SIRI YA SABA
Michael alisema sababu ya saba ambayo pia ilimshinikiza kuivunja ndoa hiyo ni kupwaya ndani ya nyumba.
Alisema kutokana na umri wake, ndani ya nyumba alijiona ni mtoto na si mume kama wanaume wengine walivyo.
“Hata uwezo wangu wa mawazo kwake haukuwa wa mume na mke, ni wa mtoto na mama. Kifupi haikuwa ndoa halali,” alisema.
SIKU ALIPOIVUNJA NDOA
Kijana huyo alisema ndoa yake na mheshimiwa huyo aliivunja mbele ya Mchungaji wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God, Dk. Getrude Rwakatare walipokwenda kusuluhishwa ili waende wakaishi kwa amani.
Alisema kabla ya usuluhishi alimfungukia mama Rwakatare kuhusu manyanyaso anayoyapata ndani ya ndoa hiyo ndipo aliposimama na kuivua pete kisha kuitupa chini huku akisema katu hawezi kurudi kwa mkewe huyo na ndoa imevunjika, akaondoka zake.
ANATAKA KILIO CHAKE KIFIKE KWA JK
Kijana Michael alisema kilio chake kikubwa kwa sasa ambacho angependa kifike hadi kwa Rais Jakaya Kikwete ni kitendo cha mkewe huyo kuzuia vyeti vyake ambavyo vingemsaidia kutafutia kazi sehemu mbalimbali.
“Amezuia vyeti vyangu vyote, kila nikimwambia navitaka nikienda ananifanyia visa, nawaomba Watanzania wanisaidie kwa hili.
“Mimi kwa sasa nataka vyeti tu, sitaki cha ndoa wala nini? Lakini hataki kunipa,” alisema Michael.
MSIKIE MBUNGE SASA
Akijibu tuhuma hizo, Mheshimiwa Kasikila alikiri kuwa na vyeti vinavyolalamikiwa na mumewe huyo, lakini alikanusha kwa nguvu zote juu ya maneno kuwa yeye ameoana na mtoto mdogo, akirejea vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinavyomtaja mtoto kama ni mtu wa namna gani.
Mbunge: “Mwandishi, unafahamu mtoto kwa katiba yetu ni mtu wa namna gani?”
Mwandishi: “Ni mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane.”
Mbunge: “Sasa Michael ni mtoto? Ana miaka 28 unamuita mtoto?”
AWAWEWESEKEA WANASIASA
Alisema anajua suala hilo lina shinikizo la kisiasa, kwani hivi karibuni baadhi ya wanasiasa walikwenda jimboni kwake wakiwa na nakala ya gazeti moja lililoandika habari zake na kijana huyo na kuwaambia wapigakura wake kuwa mbunge wao ameoa kitoto, lakini wapigakura wake waliwapuuza kwa kuwaambia hilo haliwahusu kwani wanachojua anawawakilisha vizuri bungeni.
“Kama kweli ninyi mnampenda huyo Michael, muelekezeni sehemu sahihi ya kwenda kupeleka madai yake. Ngoja nikupe mfano, mimi nikiwa wizara ya afya, mtu akija na malalamiko kuhusu pembejeo za kilimo, kwa kumsaidia, nitamuelekeza aende wizara ya kilimo, kwa kuwa pale (afya) siyo sehemu yake, sasa nyinyi muelekezeni huyo sehemu sahihi ya kupata haki yake, siyo huko magazetini,” alisema mama huyo.
MAMA RWAKATARE BWANA
Kwa upande wake, Mchungaji Rwakatare alipopigiwa simu kwa lengo la kumsikia chochote kuhusu ishu hiyo, alianza kulalamikia habari iliyoandikwa miezi miwili nyuma na kukata simu.
HABARI HII KWA MUJIBU WA GPL
↧
BINADAMU AFUNGA NDOA NA MBWA, SHUHUDIA TUKIO HILO HAPA.
Mnamo siku ya Jumatatu historia iliwekwa katika kanisa la Our Lady huko Presidio Francisco jimboni California nchini Marekani.
Mtu mmoja aitwaye Paul Horner pichani mwenye umri wa miaka 35 akiwa amevalia suti yake nadhifu alifunga ndoa na mbwa wake mwaminifu aitwaye Mac.
Mchungaji aliyefungisha ndoa hiyo Father McHale alionyesha kufurahishwa kwake na kitendo cha yeye kufungisha ndoa hiyo ya kihistoria nchini Marekani.

MASKINI MTOTO HUYU AZALIWA AKIWA NA SURA MBILI.
![]() |
MADAKTARI wa Hospitali ya Holy Family (HFH)wanapigania maisha ya mtoto aliyezaliwa Septemba 25, mwaka huu akiwa na sura mbili na uzito wa kilo 3.2. |
Mtoto huyo ni wa tatu kuzaliwa kutoka kwa Bi. Shahida Perveen na mumewe Khalil Ahmed. Msajili wa hospitali hiyo, Dk. Qaisar Aziz ameliambia The Express Tribune kwamba mtoto huyo amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (Intensive Care Unit) katika wodi ya watoto na atakuwa katika uangalizi wao.
Hata hivyo, madaktari wameonesha kukata tamaa na kusema kuna uwezekano mdogo kwa mtoto huyo kuendelea kuishi na kukua. “Kumlisha kwa kutumia mdomo haiwezekani kwa sasa, tunamlisha kwa kutumia mipira maalum (Naso-gastric tube). Sura hizi mbili zinafanana,” alisema Dk Qaisar.
Mtoto huyo ana macho manne, pua mbili, midomo miwili na masikio manne, kwa maana kwamba ana sura mbili.
Habari zinasema mama wa mtoto huyo alipopimwa na mashine maalum, (Ultrasound) alionekana hana matatizo yoyote na alikuwa na afya njema.
Baadhi ya wananchi waliotoa maoni yao kufuatia tukio hilo, walisema dunia imetikisika kufuatia kuzaliwa kwa mtoto huyo wa ajabu na kuongeza kuwa hiyo ni ishara kwamba imefika mwisho.
>>Gonga Like Yako Hapa ili Upate Habari Kwa Wakati>>
↧
KUTANA NA MTU MWENYE MIGUU MIREFU KULIKO WOTE DUNIANI.
![]() |
↧
↧
PENZI LA DIAMOND NA WEMA SASA NI MOTOMOTO.WENYE WIVU WAMEZE WEMBE.
↧
KANISA KATOLIKI LAISHUKIA TASNIA YA BONGO MOVIE.
Stori: Jelard Lucas KANISA la Romani Katoliki limeishukia tasnia ya filamu Bongo (Bongo Movies) kutokana na matendo maovu yanayofanywa na wasanii katika sinema zao hususan suala zima la kuheshimu imani za watu.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi amewaonya wasanii kuwa maigizo yao yasilenge kuchafua umma ama kikundi chochote kwani wanaweza kuleta mgawanyiko katika taifa.
Akizungumzia msimamo wa kanisa kuhusiana na filamu ya Sister Maria ya mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambayo kanisa hilo liliipinga kutokana na madai ya kukiuka maadili, Askofu Ruwa’ichi alisema hawakubalini nayo kwani mavazi ya masista yaliyotumiwa na wasanii hao, yalitumika vibaya hivyo hawakubaliani nayo.
Akifafanua zaidi kuhusiana na filamu hiyo, kiongozi huyo wa kiroho alisema alisononeshwa na kazi hiyo ambayo ilikuwa na dosari za kuingilia imani ya kikatoliki kwani mavazi ya kanisa yalitumika kuvaliwa bila staha.
“Ile filamu ilikuwa na lengo la kuhatarisha jamii, kamwe isiendelee kwani ni hatari kwa watu ama mtu binafsi anayechukizwa na tatizo hilo,
“Maigizo yanayofanywa yanaweza kuwa na lengo la kutumbuiza, lakini kutumbuiza kokote kule, hakupaswi kuhatarisha lengo la kulea ama kuvuruga mambo ya watu fulani, kulinda heshima ya watu binafsi ama taasisi, nidhamu inahitajika kwa kila jambo wanalolifanya,” alisema.
Askofu huyo alisema taifa lina mambo mengi na linajivunia kwa amani ya muda mrefu, hivyo waigizaji hao wanapoigiza maigizo ambayo yanagusa imani au jamii ya watu wengine linaweza kuwa tatizo kubwa huko mbele.
“Hakuna haja ya maigizo kuchafua watu wengine, heshima kwa wote ni jambo jema ambalo linaweza kuongeza upendo kwa kila jambo ufanyalo kwa jamii nyingine.
“Wakifanya kazi zao kwa ufasaha bado taifa litawaheshimu, hakuna mtu ama kundi ambao wangependelea kutokee vurugu eti kwa sababu ya maigizo ya mtu fulani, haiwezi kuungwa mkono,” alisema askofu huyo.
CHANZO: GPL
>>Gonga Like Yako Hapa ili Upate Story Za Nguvu>>
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi.
Akizungumzia msimamo wa kanisa kuhusiana na filamu ya Sister Maria ya mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambayo kanisa hilo liliipinga kutokana na madai ya kukiuka maadili, Askofu Ruwa’ichi alisema hawakubalini nayo kwani mavazi ya masista yaliyotumiwa na wasanii hao, yalitumika vibaya hivyo hawakubaliani nayo.
Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
“Ile filamu ilikuwa na lengo la kuhatarisha jamii, kamwe isiendelee kwani ni hatari kwa watu ama mtu binafsi anayechukizwa na tatizo hilo,
“Maigizo yanayofanywa yanaweza kuwa na lengo la kutumbuiza, lakini kutumbuiza kokote kule, hakupaswi kuhatarisha lengo la kulea ama kuvuruga mambo ya watu fulani, kulinda heshima ya watu binafsi ama taasisi, nidhamu inahitajika kwa kila jambo wanalolifanya,” alisema.
“Hakuna haja ya maigizo kuchafua watu wengine, heshima kwa wote ni jambo jema ambalo linaweza kuongeza upendo kwa kila jambo ufanyalo kwa jamii nyingine.
“Wakifanya kazi zao kwa ufasaha bado taifa litawaheshimu, hakuna mtu ama kundi ambao wangependelea kutokee vurugu eti kwa sababu ya maigizo ya mtu fulani, haiwezi kuungwa mkono,” alisema askofu huyo.
CHANZO: GPL
>>Gonga Like Yako Hapa ili Upate Story Za Nguvu>>
↧
LIBYA WAIBUKA MABINGWA CHAN 2014.
TIMU ya taifa ya Libya imetwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2014 baada ya kuifunga Ghana
kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana Jumamosi Uwanja wa Cape Town.
Ushindi huo ni sawa na Libya kulipa kisasi kwa Ghana baada ya kufungwa kwa penalti 7-6 miaka 32 iliyopita kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
>>Gonga Like Yako Hapa>>