Waziri Mkuu wa Australia, Tonny Abbot amesema kuwa maafisa walioko kwenye zoezi la utafutaji wameona vitu viwili ambavyo vinahusishwa na vinaaminika kuwa vya ndege hiyo. Ameeleza kuwa vitu hivyo vimegundulika kusini mwa bahari ya Hindi
"Taarifa mpya na ya kuaminika imeanza kuonesha nuru kwenye utafutaji wa meli ya Malaysia kusini mwa bahari ya Hindi." Amesema Tonny Abbot.
"Kwa kufuata upembuzi wa wataalam kupitia taswira za satellite, vitu viwili vinavyohusiana na msako huo vimetambulika." Ameongeza.
Hata hivyo waziri wa usafiri wa Malaysia amesema kuwa bado hawajaiona taswira ya vitu hivyo, kwa hiyo hawawezi kuzungumza moja kwa moja hadi watakapothibitisha.
Ndege hiyo iliyopotea na kusini mashariki mwa Asia mapema mwezi huu ikiwa na abiria 239.
Jana ndugu na jamaa wa abiria wa China waliokuwa kwenye ndege hiyo walitishia kugoma kula chakula endapo Malaysia haitatoa taarifa mahususi kuhusu upoteaji wa ndege hiyo.