
“Jay Z amekubali katika hatua za awali lakini ametoa sharti moja kuwa katika hali yoyote yeye, mkewe Beyonce na mtoto wao Blue Ivy wasioneshwe kwenye runinga katika sherehe hizo.” Mtu wa karibu wa Kim Kardashian ameiambia Daily Star.
Hata hivyo huu unaonekana utakuwa mtihani kwa Kanye West na Kim Kardshian kwa kuwa kituo cha runinga cha E! kitalipa mkwanja mrefu kwa ajili ya kuonesha ndoa hiyo itakayofanyika Paris, Ufaransa.
Na hiyo ingekuwa faida kwa reality show ya familia ya Kim Kardashian ‘Keep Up with The Kardashians’ kwa kuwa ingeteka watazamaji wengi duniani kufuatia tukio hilo.