Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

BABAMZAZI POOL CLUB LEO LIVE NA MASHUJAA POOL CLUB.

$
0
0

Babamzazi Pool Club ambayo ni Club Mpya Kabisa leo itachuana na Wakongwe na Mabingwa wa POOL Mkoa wa Ilala 2013/2014 Mashujaa kwenye Uwanja wao wa Nyumbani Vingunguti Mashujaa Pub.

Mechi hiyo ya shika nikushike itaanza saa 7 mchana mpaka 10 jioni.
Timu ya babamzazi inaundwa na Vijana Chipukizi na pia ni Timu mpya na mechi ya leo ndio Mechi yao ya kwanza.
Pamoja na kwamba ni timu mpya na inaundwa na Vijana Chipukizi ila kwa kujiamini wameahidi kutoa kipigo Cha paka mwizi kwa Wakongwe Mashujaa.
Makamu Mwenyekiti wa babamzazi Hussein Baha amesema baada ya Mashujaa wiki ijayo watacheza na Mpo Afrika iliyoko Tandika na Baada ya Hapo ni Top land ambao ndio Mabingwa wa Tanzania 2013/2014.
Kauli mbiu ya babamzazi pool club ni Hapa Kazi tu Hatufagilii Majina.
Wote Mnakaribishwa kushuhudia mpambano huo Mkali Pale Vingunguti Mashujaa Kuanzia saa 7 mchana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles