
Chege alisema kwamba, “Nimetumia kama millioni 12 kuandaa video yangu ya Binadamu ambayo nimefanya na Ogopa videos na mipango ni kuitoa baada ya wiki moja tangu video ya Chapa nyingine itoke”.
Kuhusu kutoa video mbili kwa wakati mmoja badala ya kuzipa nafasi Chege alisema,”Wimbo na video ya Binadamu ni tofauti kabisa na Chapa nyingine, Binadamu inavionjo vya reggae na hii nai-push zaidi kwenye channel za kimataifa ndio maana nimeweka pesa nyingi kwenye hii video”.
Aliendelea na kusema,”Hizi video na nyimbo zenyewe zote ni tofauti kwa hiyo hakuna moja itakayoifunika nyingine kutokana na utofauti wake”.