
Fareed Kubanda aka Fid Q amefunguka kuwa mitindo aka fashion kwa lugha ya kigeni ndio
ambao unauhitaji zaidi muziki ili tasnia hiyo iweze kuendelea, na kwamba muziki hauhitaji mitindo.Ngosha The Swag Don ametoa mtazamo wake alipokuwa akifanya mahojiano na jarida la FAS Jumatano, December 18.
“Mwanamuziki anaweza kuvaa kitu chochote na kikageuka kuwa mtindo siku inayofuata.” Fid Q aliliambia jarida la FAS.
“Mitindo inahitaji muziki zaidi ya jinsi ambavyo muziki unahitaji mitindo kwa sababu muziki unajitegemea zaidi. ‘Catwalk’ bila muziki haifurahishi. Unaweza kuunganishwa na muziki kupitia radio bila kufahamu muimbaji amevaa nini.” Fid Q ameeleza.