
Lulu amepost Instagram picha iliyochukuliwa kwenye filamu aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba, iliyopata umaarufu sana ‘Family Tears’.
“TBT-Family Tears”, Lulu ameandika kwenye post hiyo.
Shabiki wake anaetumia jina la julianatz kwenye instagram aliandika kumtia moyo, kutokana na mengi yanayozungumzwa mtaani kuhusu yeye na Kanumba na kunyooshewa vidole.
“I have always had empathy for you @hotlulumichael always remember when people point one finger at you. Three fingers are left pointing back at them selfs keep on taking care of your mother and brother and close your ears to the negativity."
Katika hatua nyingine, Lulu amelalamika kupitia akaunti yake ya twitter:
Dah nilijua mtu ukikaa kimya labda watu wanaweza kukusahau,lkn inaonekana ndo nimewapa nguvu za kuzusha na kutafuta mambo yangu kwa undani..— Elizabeth Michael (@hotlulumichael)