
Taarifa ya kuokolewa kwa watoto 80 katika kambi ya kundi la Boko Haram huko Cameroon imedaiwa kwa sasa hawawezi kukumbuka tena majina yao kwa mujibu wa afisa aliyewatembelea.
Watoto hao wenye umri wa miaka 5 hadi 18 hawawezi kuzungumza lugha yoyote ile kulingana na maelezo ya Christopher Fomunyoh,ambaye ni mkurugenzi wa kitaifa wa taasisi ya National Democratic Institute {NDI}.
Watoto hao walipatikana katika kambi Kaskazini mwa Cameroon mnamo mwezi Novemba mwaka jana.
Kundi la Boko Haram kutoka Nigeria limepanua mashambulizi yake hadi nchini Cameroon na wapiganaji hao wanajaribu kusimamisha taifa lenye uongozi wa kiislamu kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Hivi karibuni kundi hilo liliahidi kuiga mfano wa kundi la Islamic State ambalo limeteka eneo kubwa la Syria na Iraq.
Chanzo:Millardayo.