Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Hii ndio Tuzo ya heshima kwa staa huyu wa soka baada ya kukemea ubaguzi wa rangi..

$
0
0
etoIshu ya ubaguzi wa rangi kwa nchi za wenzetu bado imeendelea kuonekana kuchukua nafasi, hata katika soka matukio ya ubaguzi kwa baadhi ya wanasoka ambao ni weusi imeendelea kuchukua headlines.
Tukio la hivi karibuni la mashabiki wa Chelsea lilionyesha dhahiri kwamba bado hawana mapenzi na watu wa rangi nyeusi baada ya kumzuia shabiki mwenzao asipande ndani ya treni kutokana na kuwa mweusi.
etooMshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Etoo ameweza kutunukiwa tuzo ya kupambana na ubaguzi wa rangi juzi jumatatu na Shirika lisilo la kiserikali la usuluhishi linalojulikana kama The European Council on Tolerance and Reconciliation (ECTR).
Mchezaji huyo raia wa Cameroon amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kupambana na mambo yanayohusu ubaguzi kwa kipindi chote ambacho amekuwa akicheza katika klabu mbalimbali za soka na hivi karibuni alilaani kitendo cha mashabiki wa chelsea kumbagua shabiki mwenzao kutokana na kuwa ni mtu mweusi wakati wakitoka uwanjani.
raciEtoo ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Sampdoria alipewa tuzo hiyo ya heshima na Shirika lisilo la kiserikali la The European Council on Tolerance and Reconciliation (ECTR).
Chanzo:Millardayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles