
KIZUNGUMKUTI!!
Wewe ni mjomba wake Anna, Anna ni mwanafunzi wa shule moja jijini Arusha.
Lakini Anna ana mahusiano ya kimapenzi na kijana aishiye jijini Mwanza.
Anna anabanwa sana na wazazi wake hivyo hapati nafasi kabisa ya kuonana na mpenzi wake.
Siku moja baada ya kufungua shule badala ya kwenda shule akafunga safari kwenda Mwanza na wewe mjomba ndiye mtu pekee aliyekwambia.
Wazazi wakatambua kuwa ameenda Arusha ila wewe unajua ameenda Mwanza.
Akiwa njiani kwenda Mwanza akapata ajali na kupoteza uhai!!
Wazazi hawana wasiwasi wanajua mtoto ameenda Arusha lakini wewe mjomba unajua kila kitu.
Kwa jinsi alivyoharibika anashindwa kutambulika upesi hivyo serikali inaamua kuwa itamzika.
Je? Utakubali azikwe na serikali ama utawaeleza wazazi wake kila kitu??
Kumbuka wazazi wa Anna wanakuheshimu sana!!!
Kizungumkuti ! Utafanyeje?
Hiki Kipengele Cha Kizungumkuti Ipo Kwenye Papapo Kila Siku.Hivyo Tunazijadili Kwa PAMOJA Kwa Radio TBC fm.Plz Nipe Kizungumkuti Chako ILI Nitumie Leo Kwa PAPASO plz na nitathamini Sana Mchango Wako.Nitumie Kwa email babamzazionline@gmail.com Tuma nyingi Kama Unavyo!