
Yusuph Manji amesema maamuzi ya kutowania tena nafasi ya uongozi ndani ya klabu hiyo ni yake mwenyewe na kwamba anaamini hatua hiyo itatoa nafasi kwa wana chama wengine kuiongoza klabu hiyo.
Manji ameongeza kuwa haoni aibu kutangaza uamuzi huo, ikiwa ni siku chache zimepita tangu kutangazwa kwa taarifa ya hasara iliyopatikana katika klabu hiyo.
Amesema pamoja na taarifa hiyo kutolewa,bado ana muda mwingine wa miezi saba wa kuhakikisha anaiacha Yanga katika hali nzuri kifedha kwa kuzingatia mazungumzo kati ya uongozi wa Yanga na wadhamini pamoja na shirikisho la soka chini 'TFF' kuhusu mkataba wa Azam TV.