Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Ibra Cadabra awataka waandishi wa habari wasahau mpango wa kumshindanisha na Cristiano Ronald.

$
0
0
Zlatan Ibrahimovic amefikisha ujumbe huo baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari mara baada ya kuisaidia klabu yake kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Olympiacos ambao walikubalia kulala mabao mawili kwa moja katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambao uliochezwa usiku wa kuamkia jana Novemba 28.
Ibrahimovic amesema anajitambua yeye ni mwenye kipaji anapokua uwanjani na wala haitaji tuzo am ubingwa kuthibitisha ubora wake, kama inavyokua kwa wachezaji wengine duniani kote.
Amesema lengo lake kubwa alilojiwekea ni kuisaidia klabu yake kufikia malengo yalikusudiwa tangu mwanzoni mwa msimu huu na si kufikiria nafasi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ambapo hafla yake itafanyika mwanzoni mwa mwaka 2014.
Suala la kushindanishwa kwa Zlatan Ibrahimovic *Ibra Cadabra* dhidi ya  Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro lilianza mara baada ya nchi za Ureno na Sweden kupangwa pamoja katika mchezo wa hatua ya mwisho ya kuwani kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia ukanda wa barani Ulaya.
Hata hivyo mjadala huo ulionekana kufungwa baada ya Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro kufanya shughuli kubwa ya kuisdaidia nchi yake kufuzu katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kwa jumla ya mabao manne kwa mawili.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles