Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Malkia Elizabeth II afikisha umri wa miaka 88, sherehe kufanyika June 14.

$
0
0
Malkia Elizabeth II wa Uingereza jana (April 21) alifikisha umri wa miaka 88 huku akionekana mwenye afya tele.

Siku moja kabla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa (April 20) ilikuwa Jumapili ya Pasaka na malkia Elizabeth II pamoja na familia yake walihudhuria ibada katika kanisa la St. George jijini London.
Ingawa April 21 ndio siku aliyo zaliwa Malkia Elizabeth II,  sherehe rasmi za siku yake ya kuzaliwa hufanyika katika kipindi cha majira ya joto (June).
Kwa mwaka huu sherehe za kitaifa ya  kuzaliwa Malkia Elizabeth II zitafanyika Jumamosi ya June 14 jijini London zikiambatana na gwaride la kijeshi ,kupiga risasi hewani  sambamba na kurusha ndege za kivita.
Hiyo huitwa ‘Official birthday’.
Sherehe hizo zitaoneshwa moja kwa moja kupitia BBC.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles