
Makamu Mwenyekiti alisema ‘nimepokea hati ya makubaliano ya muungano na ni certified copy na sasa nampa dakika mbili Mh. Wassira atoe maelezo ya hati hii’
Mh Wassira akaanza >> 1. Juzi nilisimama katia bunge hili na kusema kwamba hati ya muungano iliyokua inapigiwa kelele sana, ipo katika hali nzuri na ndani ya siku mbili itafikishwa bungeni.
- Sisi wote tumeapa na mwisho wa kiapo chetu tukasema ewe Mungu nisaidie, Mungu wa madhebu yote ni Mungu wa ukweli na uongo ni kazi ya shetani, wamegawana kabisa Mungu wa ukweli na Shetani wa uongo.
- Baada ya hati kupatikana jana Tundu Lissu na wenzake wamekutana wakazungumza kwamba sasa tusema sahihi ya Karume sio sawa, tunaipeleka wapi Tanzania? yani kila siku uongo unataka utawale Tanzania na ukweli upuuzwe?
- Watanzania tujihadhari sana na Mawakala wa shetani maana Mungu anatumia Wanadamu kufikishia ujumbe wake kwa Wanadamu wengine na Shetani anatumia Wanadamu pia, lazima tukwepe mamlaka ya shetani na Mawakala wao.
- Mh. Tundu Lissu amewakashifu waasisi wa taifa Mzee Karume na Mwl. Nyerere Mungu awaweke mahali pema, anasema ni madikteta na waongo…. mimi nasema heshima ya viongozi wetu waasisi hailindwi na vyama, italindwa na Watanzania wote, wajibu wa kulinda heshima yao ni wa wote.
- Hatuzuii mtu kusahihisha sera lakini huwezi kusema viongozi wetu wale walikua ni waongo na Madikteta, hatuna haki ya kuwakashifu, namwambia rafiki yangu Tundu Lissu, ulinzi wa heshima ya viongozi hawa ni wa Watanzania na utalindwa kwa gharama yoyote.