Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Nahodha wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania asema mafanikio yao yalitokana na mazoezi makali na hali ya kujituma.

$
0
0

Nahodha wa timu ya watoto wa mitaani ya hapa Tanzania iliyonyakua kombe la dunia jumapili amesema mafanikio yao yalitokana mazoezi makali na hali ya kujituma. 
Nahodha huyo kwa jina Deogratius amesema michuano hiyo iliwafanya kudumisha umoja katika kambi ya mazoezi na kujitolea kikamilifu kwa ajili ya kunyakua kombe hilo.
Kwenye fainali, Timu hiyo iliilaza Burundi magaoli 3-1 mjini rIo De Janeiro nchini Brazil.Hata hivyo rais wa kituo kinachowalea watoto hao Altaf Hirani amesema juhudi zaidi zinahitajika katika kuwasaidia watoto wa mitaani.Timu hiyo imeundwa na kituo cha michezo ya watoto wa mitaani kinachofanya kazi na watoto 300 wa mitaani TSCSA .Mabao ya timu hiyo yalipachikwa wavuni na Frank William.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles