Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

David Moyes; kushindwa kuwajibika kwa wachezaji, kumeitoa Man Utd kwenye michuano ya Ulaya.

$
0
0
Meneja wa klabu ya Man Utd David Moyes, amesema makosa ya kipuuzi yaliyofanywa na wachezaji wake wakati wa mchezo wa dhidi ya FC Bayern Munich yaliwagharimu na kujikuta wakikubali kufungwa mabao matatu kwa moja.

David Moyes, ametupa lawama hizo kwa wachezaji wake kwa kigezo cha mabao yaliyofungwa na wapinzani wao ambayo yalionekana kuwa mepesi zaidi ya bao lililotangulia kufungwa na beki wa pembeni wa Man Utd Patrice Evra.
Moyes, amesema kukosekana kwa umakini kulichangia kwa kiasi kikubwa kwa Man utd kutupwa nje ya michuano hiyo, hali ambayo amekiri haikumpendeza, kutokana na mchezo ulivyokua, ambapo ilionekana walikua na nafasi nzuri ya kupata ushindi katika uwanja wa ugenini.
Meneja huyo kutoka nchini Scotland amesema kulikua hakuna sababu kwa wachzaji wake kubweteka, baada ya kuongoza kwa bao moja lakini matokeo ya udhaifu huo yalinekana sekunde kadhaa kutokana na FC Bayerrn Munich kupata bao la kusawazisha lililofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Croatia Mario Mandzukic, ambae aliumalizia kwa kichwa mpira uliokuwa umepigwa na mshambuliaji wa pembani kutoka nchini Ufaransa Franck Ribery.
Hata hivyo David Moyes hakuishia hapo katika hatua ya kuchambua makosa yaliyofanywa na wachezaji wake, hususana wa safu ya ulinzi ambao bado waliendelea kuoonyesha umakini kwa kushindwa kuzuia ipasavyo mpira uliokuwa umepigwa kutoka pembeni na Arjen Robben kabla ya Thomas Muller kufunga kwa urahisi tena akiwa kati kati ya mabeki wa mashetani wekundu.
Kwa upande bao la tatu, Moyes ameendelea kuilaumu safu yake ya ulinzi kutokana na kitendo cha kumuachia huru winga kutoka nchini Uholanzi Arjen Robben kutokana na kitendo cha kuukokota mpira kwa kipindi cha sekunde kadhaa kabla ya kufanya maamuzi ya kupiga langoni na kusababisha bao lililowamaliza kabisa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles