
Hii imedhihirika baada ya mashabiki wa Justin Timberlake na Miley Cyrus walioko Finland kuondolewa wasiwasi kuwa wanamuziki hao wataendelea na ratiba yao ya kufanya shows kwenye kumbi ambazo zinamilikiwa na matajiri wakubwa wa Urusi.
Kwa mujibu wa Reuters, matajiri hao wanamiliki Hrtwall Arena ambako Miley Cyrus anatarajia kufanya show June mwaka huu, huku Timberlake akitajiwa kutumbuiza May mwaka huu katika ukumbi huo.
Matamasha hayo yalikuwa hatarini kukataliwa kwa kuwa matajiri hao ni marafiki wakubwa wa rais wa Urusi Vladimir Putin.