Mwanasoka anayetajwa kuwa bora kuliko wote waliowahi kutokea duniani, mbrazil Pele ametumia fursa ya kombe la dunia kutambulisha biashara ya kumuingizia kipato zaidi.Kwa kutumia nywele zake mbrazil huyo ametengeneza almasi kutokana na mchanganyiko wa carbon inayopatikana kwenye nywele pamoja na almasi yenyewe.
Kutokana na mchanganyiko huo zimepatikana almasi 1283 zenye thamani ya $7,500 – namba ya idadi ya alamsi ni sawa na idadi ya magoli aliyofunga pele katika maisha yake ya soka la kulipwa.Almasi zitauzwa wakati wa michuano ya kombe la dunia itakayoanza mwezi June.