
Ukiwa shabiki namba moja wa babamzazi.com utakuwa ulisikia kuhusu Mchumba wake Msanii Shakira kusema hataki mpenzi wake afanye video na mwanaume yoyote tena kwenye maisha ya muziki wake.
Mpenzi wa Shakira ambaye ni beki wa klabu ya FC Barcelona ‘Gerard Pique, ilisemekana amempiga marufuku Shakira kufanya video na model wa kiume na wanasema tamko hilo lilihamasishwa na video nzuri waliyotengeneza Shakira na Rihanna kwenye wimbo wao “Cant Remember to Forget You” .
Shakira amebadilisha tamko lake na kusema kuwa kwenye mahojiano aliyofanyiwa, alisema kwa utani kuwa amekatazwa kufanya video na male models ila sio issue serious sana na hatarudia tena.