Aliyekuwa muwakilishi wa Tanzania kwenye jumba la Big Brother Africa, Feza Kessy ataachia wimbo mpya hivi karibuni alioupa jina la ‘My Papa’ na umetayarishwa na Nahreel.
“And finally here it is”, ametweet mwimbaji huyo wa Amani ya Moyo. Tayari wimbo huo umeanza kupewa nafasi na baadhi ya watu maarufu ambao bila shaka wameshausikiliza.