
Shirikisho la soka duniani FIFA bado linaendelea kukabiliwa na changamoto ya kuwa nje ya muda wa kukamilika kwa maandalizi ya fainali za kombe la dunia ambazo kwa mwaka huu zimepangwa kufanyika nchini Brazil kuanzia June 12 - July 13.
Katibu mkuu wa shirikisho hilo Jerome Valcke, amesema mpaka sasa viwanja viwili ambavyo vitatumika kwenye fainali hizo havijakamilika kutokana na sababu mbali mbali, huku sababu kubwa aliyotajwa na mkuu huyo ni vifo vya wafanyakazi vilivyotokea katika viwanja hivyo husika.
Jerome Valcke, amesema pamoja na kukabiliwa na changamoto hiyo ambayo inawafanya wenyeji kuwa nje ya muda wa kumaliza maandalizi ya fainali za kombe la dunia, bado shughuli nyingine zinaendelea na wana hakika ratiba ya fainali za kombe la dunia za mwaka huu zitafuatwa kama kawaida.