Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Queen Darleen Na Video Mpya “Wanatetemeka” Kuzinduliwa Jumapili hii ya Tarehe 06.04.2014.

$
0
0

Video “WANATETEMEKA” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa msanii QUEEN DARLEEN ambaye pia ni dada wa Diamond Platnumz sasa itazinduliwa siku ya jumapili hii tarehe 06 April, 2014 Club Bilicanas.


Video hiyo iiyoandaliwa kwa kiwango kikubwa, inategemewa  kuleta mapinduzi makubwa sana katika tasnia ya video za muziki wa Bongo Flava hasa kwa ubunifu wake na kiwango kikubwa cha picha yenyewe kwa muonekano.
Kwenye video hiyo  wamo wasanii SHILOLE na DIAMOND PLATNUMZ, tena kwa mara ya kwanza Kaka na Dada (QUEEN na DIAMOND) watokea kwenye video moja ambayo imetengenezwa hapa hapa nchini Tanzania na muandaaji wa video JERRY MUSHALA.
Wasanii watakao msapoti QUEEN DARLEEN siku hiyo ya tarehe 06 April, ni pamoja na WAKAZI, BARNABA, MWASITI, AMINI, NASRY, VJ PENNY, RECHO, CINDY RULZ, PIMP SITTA, HERO na wasanii wenginge wengi utawaona kama Surprise, pia Bongo movies artists kama WOLPER, RADO na wengine kibao kwenye RED CARPET.
Kiingilio kitakuwa TZS. 10,000/- tu mlangoni pale Bilicans siku hiyo ya tarehe 06. Hii si shoo ya kukosa.
IMG-20140310-WA0029IMG-20140310-WA0037IMG-20140310-WA0047

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles