Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Brendan Rodgers, asema msimu huu si wa Liverpool kutwaa ubingwa.

$
0
0
Brendan Rodgers, ameendelea kushikilia msimamo huo, huku akisema ni heshima kwa klabu yake kuwekwa katika kundi la kufikiriwa huenda ikatwaa ubingwa msimu huu, lakini kwake ataendelea kupingana na suala hilo kutona na kuamini msimu wa kufikiriwa kuwa mabingwa unakaribia na sio huu wa sasa.
Rodgers amepingana na waandishi wa habari katika suala hilo, alipokua akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea katika mchezo wa kesho wa ligi ya nchini Uingereza, ambapo The Reds watapambana na Sunderland katika uwanja wa ugenini.
Amesema kwa sasa ikitokea anatwaa ubingwa, itakua kama bahati kubwa kwa Liverpool, kutokana na kuamini bado kikosi chake hakijaiva sawa sawa katika hatua ya kufikia mafanikio hayo, na ndio maana amebainisha kwamba msimu wao wa kufanya hivyo upo njiani unakuja.
Amesema kwa hakika mashabiki wa Liverpool wanatamani iwe msimu huu, kutokana na kusubiri kwa muda mrefu taji la nchini Uingereza, ambalo kwa mara ya mwisho walilichukua mwaka 1990 lakini ameendelea kuwataka kuwa na subra.
Hata hivyo meneja huyo kutoka Ireland ya kaskazini amekipongeza kikosi chake kwa kazi nzuri waliyoifanya mpaka sasa, na pia anaamini mazuri yataendelea kuonekana kadri siku zinavyoendelea kusogea.
Endapo Liverpool watafanikiwa kushinda katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Sunderland, wataendelea kuisogelea Chelsea iliyo kileleni kwa sasa kwa tofauti ya point nne.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles