Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Baraza la Sanaa na Idara ya Uhamiaji wazungumzia biashara ya ngono inayofanywa na wasanii wanaotoka nje ya nchi.

$
0
0
Hali hiyo imebainika baada ya Idara ya uhamiaji kubaini kuwa kuna baadhi ya maofisa wa idara hiyo wanaodaiwa kupokea rushwa na kuusaidia mtandao unaojihusisha na biashara hiyo.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wasichana wanaofanya biashara hiyo wakiwa na nembo ya usanii ili wapete kibali kiurahisi, wanatoka India, Nepal, Pakistan na Bangladesh. Wasichana hao mbali na kujihusisha na biashara ya ngono hujihusisha pia na biashara haramu ya binadamu.
Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mnengereza ameiambia Maskani ya 100.5 Times Fm kuwa waliwahi kuwa na taarifa hizo lakini katika siku za hivi karibuni hawajapokea taarifa kama hizo.
Mnengereza amewataka watu wanaojihusha na biashara ya kuleta wasanii nchini kuwa makini na kwamba watakapobainika kuwa wamekiuka masharti ya vibali vilivyotolewa watachuliwa hatua kali za kisheria.
Hivi karibuni, msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Abbas Irovya alitoa taarifa ya kuwepo kwa biashara hiyo inayokiuka masharti ya vibali vya kuingia nchini na kujihusisha na biashara ya ngono.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles