Kocha wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Zanzibar na Azam fc, Sterwart John Hall
WAKATI ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa wakati wa magharibi kwa maana ya lala salama, aliyekuwa kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes na klabu ya Azam fc mpaka mwishoni mwa mzunguko wa kwanza msimu huu wa 2013/2014, Mwingereza Sterwart John Hall amesema msimu huu una ushindani mkubwa zaidi ya msimu uliopita.
Katika mahojiano maalumu na mtandao huu, Hall alisema imekuwa jambo zuri kuibuka kwa timu ngumu kama Mbeya City, lakini bado kuna timu dhaifu nyingi kitu ambacho si kizuri katika ligi.
“Nikiwa kocha wa mpira, lazima nisema ukweli, msimu huu umekuwa bora zaidi, lakini nadhani yanahitajika maboresho zaidi kwa klabu ili kupunguza udhaifu wa timu nyingi”. Alisema Hall.
Kocha huyo aliongeza kuwa imekuwa ikishangaza sana na ni jambo zuri pale timu ndogo zinapotoa changamoto kubwa uwanjani dhidi ya timu kubwa za Simba, Yanga na Azam fc.
“Zinahitajika timu nyingi zenye ubora kama Mbeya City, hapo utaona ligi bora. Kuna timu za chini, hakika zimekuwa zikionesha kiwang duni sana na kuharibu utamu wa ligi”. Alisema Hall.