Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Louis akanusha taarifa za kujiunga na klabu ya Tottenham.

$
0
0
Louis van Gaal amezikana taarifa hizo baada ya kuhusishwa nazo kwa muda wa juma moja lililopita ambapo baadhi ya vyombo vya habari vya nchini Uingereza vilidai kwamba huenda kocha huyo mwenye umri wa miaka 62,angejiunga na Spurs mara baada ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambazo zitafanyika nchini Brazil.
Van Gaal amesema ana hakika uzushi huo wa vyombo vya habari huenda umeibuka kutokana na mkataba wake wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kutarajia kufikia kikomo mara baada ya fainali za kombe la dunia,lakini hakusita kukiri wazi kwamba suala hilo lina ukweli.
Amesema pamoja na kutoitarajia kuendelea kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi bado haijalishi kama atajiunga na klabu ya Spurs,kutokana na mipango yake aliyojiwekea ya kutaka kuishi nchini Ureno ambapo ndipo alipowekeza maisha yake kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo Louis van Gaal amesema angependa mara baada ya kuachana na timu ya taifa ya Uholanzi akarejea tena kufanya kazi ya kufundisha moja ya klabu kubwa nchini Uingereza,lakini hakuwa tayari kuitaja licha ya kutania mbele ya waandishi wa habari kwa kusema huenda ikawa Tottenham Hotspurs ama la.
Louis van Gaal kabla hajakabidhiwa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi  mwaka 2012 aliwahi kuwa meneja wa klabu kubwa kama FC Barcelona pamoja na FC Bayern Munich huku klabu za nyumbani kwao Uholanzi alizobahatika kuzifundisha ni AZ Alkamar pamoja na Ajax Amsterdam.
Kama itakumbukwa vyema uongozi wa Tottenham Hotspurs umekua ukihangaika kumsaka mbadala wa mkuu wa benchi la Ufundi tangu walipomtimua meneja kutoka nchini Ureno Andre-Villas Boas japo kwa sasa kitengo hicho kimekuwa kikiongozwa na Tim Sherwood aliyesainishwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles