
Diego Maradona amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake mwenye miaka 23 Rocio Oliva baada ya kugundua wanategemea mtoto wao wa kwanza.
Rocio ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa mpira wa miguu ameanza mahusiano na Maradona mwaka jana na hivi karibuni alivalishwa pete kwenye sherehe ndogo ndani ya hoteli ya Rome kwenye Valentines Day. Hii ilikuwa siku mbili tu baada ya binti mwingine aliyewahi kuwa na Maradona kusema kuwa anaujauzito wa star huyo, Binti huyu anaitwa Ojeda.
Maradona amekanusha uvumi huo na kusema sio baba wa mtoto huyo. Fahamu Maradona anatambua watoto wake wawili na aliyekuwa mke wake Claudia Villafane na mtoto wake wa kiume Diego na mwingine wa kike anaitwa Jana aliyezaliwa mwaka 1996.