Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Ditto azungumzia miradi aliyoianzisha kupitia muziki wake, kampuni ya kuandaa matangazo na mashamba.

$
0
0
Kwa kuzingatia hilo, msanii wa bongo flava, Lameck Ditto anaweza kuwa tajiri wa baadae kwa kile alichokifanya endapo Mungu atajaalia miradi yake iende sawa.
Mkali huyo wa ‘Tushukuru kwa Yote’ ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa ameutumia muziki kufungua miradi mbalimbali na mwisho kufungua makampuni mawili. Kampuni ya kwanza ni ile inaendana na msemo wa ‘Kilimo Kwanza’, na ya pili inatokana na uwezo wake wa kiubunifu kama msanii  ‘kutengeneza matangazo ya radio’.
 “Muziki ndio kila kitu katika maisha yangu yaani tangu naanza maisha mpaka sasa, kwa hiyo miradi tofauti niliyoianzisha inatokana na muziki wangu …kwa sasa nina kampuni (Green Lights Music) inayohusika na uandaaji ya matangazo ya radio, kuna baadhi ya matangazo tumeshaanza kutengeneza na yanachezwa katika vituo mbalimbali natumaini miaka mitatu ijayo nitaisajili na kuipa jina la (Creative Agents).” Amesema Ditto
“Pia nina kampuni nyingine inayojishughulisha na masuala ya kilimo ‘Tunda Jema’. Nina shamba kubwa lipo Bagamoyo tayari ninaanza kuvuna matunda kama Maembe na Mananasi.”
Ameongeza kuwa kwa sasa anafanya utafiti kuhusu ufugaji wa kuku na kwamba wakati wowote atakapojiridhisha ataanza kufuga kuku kwa kuwa ufugaji ni ndoto yake ya muda mrefu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles