Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Tanzania yapata tuzo mpya, 'Tuzo za Watu', zinawahusu mastaa wanaopendwa zaidi katika filamu, muziki na utangazaji.

$
0
0

Katika mwaka 2014, tasnia ya burudani Tanzania imepata kitu kipya kabisa ambacho kinaweza kuwa chachu katika kuendeleza tasnia hiyo hapa nchini na kuwafanya wadau wa tasnia hiyo kuongeza juhudi katika kile wanachokifanya kwa ajili ya watu.

Mtandao wa Bongo5 umeanzisha tuzo zinazojulikana kama Tuzo za Watu ama kwa kiingereza ‘Peoples Choice Awards’, ambazo zinalenga katika kuwatunuku wana michezo, wanamuziki na watangazaji wanaopendwa zaidi hapa nchini.
Mwenyekiti wa Bongo5 Media Group, Luca Neghesti amesema kuwa kampuni hiyo itawatunuku tuzo wale wanaopendwa zaidi, na kwamba mshindi ataondoka na tuzo pamoja na shilingi milioni moja za kitanzania.
 “Sasa hivi tumeshuhudia ukuaji katika tasnia mbalimbali na tumeona ni wakati muafaka wa kuwatunuku wale wanaopendwa na wananchi, kuwapatia tuzo pamoja na zawadi ya fedha taslimu milioni 1." Amesema Luca Neghesti.
Ameongeza kuwa alizisajili tuzo hizo mwaka 2009 lakini kutokana na mipango na malengo ya kampuni hiyo aliamua kuziweka hadi hivi sasa.
Ameeleza kuwa tuzo hizi zitahusu watu wa rika zote na kwamba hazilengi kuleta ushindani kwa tuzo zingine hapa nchini kwa kuwa zinalenga kuwatunuku watu kutokana na umaarufu wao na jinsi wanavyopendwa na wananchi, na sio ubora.
“Tuzo hizi hazileti ushindani na tuzo zingine kwasababu hazilengi tasnia moja tu. Tanzania imesifiwa kwa uhuru wa vyombo vya habari na tuzo hizi zinalenga kujumuika na tuzo zingine kuhakikisha watanzania wanaopendwa na kufanya vizuri wanatambuliwa.” Neghesti amefafanua.
Upigaji kura unaanza wiki hii katika vipengele 11 ambapo wananchi watachagua majina ya washiriki watakaoshindana kwenye vipengele hivyo.
Awamu ya kwanza ya upigaji kura itafungwa baada ya wiki mbili kutoka siku ya kwanza ya upigaji kura na majina ya watu watano waliotajwa zaidi kutoka kwenye kila kipengele watachaguliwa kama watajwa wa mwisho. Kuanzia hapo, upigaji kura wa wananchi utajikita tu katika orodha ya majina hayo matano kwenye kila kipengele kinachoshindaniwa.
Unaweza kupiga kura kupitia www.tuzozetu.com au kwa njia ya SMS kwa kutuma neno ‘Tuzo’ kwenda namba 15678 na kisha utaletewa Menu.
Tuzo za watu mwaka 2014 zitajumuisha vipengele 11:
- MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW1 na jina' kwenda
15678)
- KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW2 na jina' kwenda
15678)
-MTANGAZAJI WA TV ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW3 na jina' kwenda 15678)
-KIPINDI CHA TV KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW4 na jina' kwenda 15678)
- MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW5 na jina' kwenda 15678)
-MWANAMUZIKI WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW6 na jina' kwenda
15678)
-MWANAMUZIKI WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW7 na jina' kwenda
15678)
-WIMBO UNAOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye 'TZW8 na jina' kwenda 15678)
- MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW9 na jina'
kwenda 15678)
-MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW10 na
jina' kwenda 15678)
- FILAMU INAYOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye 'TZW11 na jina' kwenda 15678)

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles