Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

MB Dog aeleza vitu anavyomiss Tip Top Connection.

$
0
0
Akiongea na tovuti ya Times Fm, MB Dog amesema kuwa kikubwa alichokimiss kutoka kwenye kundi hilo ni ‘sikio’ la boss wake Abdu Bonge katika kusikiliza na kuzitabiri hits kwa kumsikia tu mwimbaji akifanya mitindo huru ‘freestyle’.
“Kule kitu kimoja nilichokuwa nakimiss…ujue nikikaa na boss wangu Bonge, na Madee kichaa wangu alikuwa sana, ninapofanya hata freestyle ya uongo tu…Bonge unajua anasikio sana la kutaka kujua kitu gani ambacho unakifanya, unaweza ukaimba ngoma ambayo unaipenda akakwambia ‘daah hiyo sio hebu ile nyingine ile’.” Amesema MB Dog.
“Kwa hiyo yeye anamasikio sana ya kusikia kitu kizuri kabla watu hakijawafikia. Kwa hiyo hicho kitu kimoja ambacho huwa nakaaga nakifikiria kwamba daah, yule mchizi alikuwa ananipiga tafu…lakini kwa sasa sina mtu wa kuniambia hivyo, so hivyo ni vitu waga nakaa navimiss.”
Katika hatua nyingine, MB Dog ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa tayari ameshakaa na uongozi wa Tip Top connection na wamemaliza tofauti zao, na kwamba Abdu Bonge amemuahidi kumsaidia tena kuzisimamia kazi zake japokuwa hayuko Tip Top Connection.
“Kwa sasa niko chini ya kampuni ya QS niko na jamaa mwingine anaitwa Ngonyani. Jamaa walikaa wakawaza ‘daah huyu jamaa mwanetu tulikuwepo naye’, kama kuna sehemu walikuwa wanakwamisha wanaijua wamefikiria unajua, na kinachowaumiza kwa nini mimi niko kimya halafu kimya changu kimezidi.
“Sasa kuna vitu wanavyovipata kwenye mioyo yao, wakanisogelea ‘bana eeh inakuwa vipi’, na kwa sababu hii ni kazi na haya ni maisha wakaona sio vyema. Ndio maana sasa hivi naweza kusema nina back up kubwa kutoka kule kwa sababu Bonge mwenyewe alisema bana tufanye kazi mwanangu nisimamie, kama kuna hivi na hivi pia tutajua tunafanya nini.” MB Dog ameeleza.
Msanii huyo amesema hivi sasa anamiliki studio yake na ameiboresha zaidi hivi sasa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles