
Mwaka 2014 umeingia mwezi wa pili huku mashabiki wa muziki wakipata nyimbo mpya kadhaa kutoka kwa wasanii wanaowakubali.
Lakini mwezi February ndio kama umewasha green light tena kwa mwimbaji wa Tanzania ambaye ameyazoea mashavu ya kimataifa, Ambwene Yesaya aka AY, ambapo anatarajia kuachia wimbo mpya aliupa jina la Asante, February 10 mwaka huu.
“Where there is love there is life.. #ThanksForTheLove STAY TUNNED... 10TH FEBRUARY 2014.” AY ameandika kwenye Instagram.
Ay amemshirkisha Dela katika wimbo huo uliopikwa ndani ya MJ Records na Marco Chali, na tayari umeanza kuzungumziwa vizuri na watu ambao bila shaka wameusikiliza na wameanza kuutaja kama wimbo mkali unaokuja ‘hit’.
“Ya'll get ready fi dis one...Major Hit....Major Artist.... Asante @aytanzania @timesfmtz @mwanafa.” Hermy B, producer na CEO wa B’Hitz Music Group ameandika kwenye Instagram na kupost artwork ya wimbo huo.