Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Mbunge wa Iringa Mjini asomewa mashtaka kwa tuhuma za kujeruhi.

$
0
0

 Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa akidaiwa kuhusika na uchochezi na kusababisha vurugu katika kampeni za udiwani Kata ya Nduli.
Mch. Msigwa alikamatwa jana jioni baada ya kutokea kwa vurugu hizo katika mkutano wa kampeni wa chama cha Chadema.
Mwandishi wetu aliyepo mahakamani hapo anasema hali ya ulinzi imeimarishwa  huku kukiwa na idadi kubwa ya wafuasi wa Chadema, ambao hata hivyo wamesimama mbali na eneo la mahakama huku eneo hilo likilindwa na askari wa kutuliza ghasia (FFU).
Baada ya kusomewa mashtaka yake amekana na ameachiwa huru kwa dhamana, kesi hiyo itatajwa tena Machi 10 mwaka huu
Mbunge wa Chadema kortin vurugu za kampeni
Shija Felician, Mwananchi
Kahama. Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki (Chadema), Sylvester Kasulumbayi na Diwani wa Kata ya Buselesele, Crispian Kagoma na watu wengine 14 wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kujeruhi katika vurugu zilizoibuka katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kasulumbayi na wenzake 15, ambao wanaaminika kuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama saa 8.00 mchana jana na kusomewa mashtaka sita kila mmoja.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Gadiel Mariki, Mwendesha Mashtaka Shukrani Madulu alisema washtakiwa wote kwa pamoja walitenda makosa hayo Februari 4, mwaka huu.
Madulu aliiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao wakiongozwa na mbunge huyo walitenda kosa hilo la kuwashambulia kwa mapanga wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za kuwania udiwani wa Kata ya Ubagwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.
Alisema mashtaka matano ni kushambulia na kujeruhi kwa mapanga, na moja la kuharibu mali, ikidaiwa kuwa katika vurugu hizo washtakiwa waliishambulia gari la CCM la wilaya hiyo na kuliharibu.
Washtakiwa wote walikana mashtaka yote na kuomba mahakama iwape dhamana ili waendelee na kampeni za kumnadi mgombea wao wa nafasi ya udiwani katika kata hiyo ya Ubagwe.
Credit:Mwananchi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles