
Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amekiri ni kweli jana alikuwepo kwenye
uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London na alifanya safari ya kuelekea nchini Hispania.Arsene Wenger amekiri suala hilo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano ambao ulizungumzia mchezo wa leo wa kombe la FA ambapo Arsenal watakuwa wenyeji wa Coventry City katika uwanja wa Emirates.
Wenger amesema jana alifanya safari ya kuelekea nchini Hispania lakini akashindwa kukiri wazi kama alikuwa mmoja wa walioshuhudia mchezo wa kombe la Mfalme kati ya Fc Barcelona dhidi ya Levante huku akakanusha taarifa za dhumuni ambalo linadaiwa kuwa kubwa katika safari yake ambapo inadaiwa alikwenda kumfuatilia kiungo wa FC Barcelona Sergi Roberto pamoja na mshambuliaji wa klabu hiyoCristian Tello.
Arsene Wenger amekuwa akihusishwa na mipango ya kutaka kuwasajili baadhi ya wachezaji katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo,lakini kila mara amekuwa akikanusha taarifa za wachezaji anaohusishwa nao