
Ndauka aliyejifungua mtoto wa kike Desemba 29 katika hospitali ya taifa Muhimbili amesema kwa muda mfupi tangu ajifungue anajiona amebadilika kihisia.
"Hakuna raha kama kuwa mama. Napatwa na hisia za ajabu, huwezi amini mimi nilikuwa mlalafi mno, lakini sasa hivi pindi mtoto wangu anapoamka hata kabla hajalia naamka ghafla na kumsaidia au kumnyonyesha nashangaa inakuwaje nina hisia za ajabu kuhusu mtoto wangu akili tu siwezi fanya kitu kingine jicho langu lote linatua kwake," Ndauka ambaye amezaa na muimbaji wa kundi la TNG Squad, Malick Bandawe aka Chiwa Man ameliambia gazeti la Mwananchi.