baada ya jaji kuahirisha kesi hii ambayo imeonekana ina msuguano wa kisheria pande zote mbili,upande wa Chadema waliweka mawakili watatu Peter Kibatala,John Marya wakiongozwa na wakili wa Chadema Tundu Lissu
Upande wa Zitto Kabwe alikuwa na wakili mmoja tu ni Albert Gasper Msando ambaye pia ni diwani wa kata ya Mabogini kupitia Chadema huko 87.9 Moshi,millardayo.com imeongea na Tundu Lissu kama Wakili wa Chadema na hiki ndicho alichokisema.

‘Nafikiri tumeenda vizuri pande zote mbili zimepigana kwa ufundi mkubwa sana nafikiri Jaji ana kazi kubwa sana kesi imehairishwa mpaka Jumatatu kwa sababu masuala yaliyojadiliwa ni masuala mazito sana kisheria yanahitaji muda wa Jaji kufanya utafiti na kuyatafakari’
‘Nawaambia wanachadema chama chetu kipo imara hili wingu litapita lakini ni muhimu wanachama wafahamu mahali ambapo tumefika leo chama lazima kisafishe uchafu wote ndani ya chama utovu wote wa nidhamu uondolewe chama lazima kijisafishe vinginevyo hatutoweza kama tutaendekeza usaliti na kelele za aina hii,ujinga wa aina hii chama kitasamabaratika’
‘Mimi sidhani kama kuna makundi mawili,kwenye kamati kuu nzima wajumbe zaidi ya 30 wote wameungana na hicho ndio chombo cha juu kabisa cha kufanya maamuzi ya chama,kuhusu baraza kuu kikao cha mwisho kabisa cha mwaka jana januari.
‘Mwenyekiti wa chama ilibidi azime mjadala uliokua kwenye baraza kuu kumhusu mheshimiwa Zitto Kabwe,wajumbe wa baraza kuu walikua wanasema huyu mtu aondoke toka mwaka jana kwa hiyo haya maneno kuwa baraza kuu tunaenda kushinda ni maneno yale yale kwamba kwenye kamati kuu tupo wengi tuna akili nyingi hawatotugundua tumesoma hawa wengine hawajasoma akili ndogo’.
‘Suala la uanachama halipo baraza kuu suala la uanachama lipo kwenye kamati kuu kwenye baraza kuu anapeleka rufaa kwamba ameadhibiwa kimakosa amevuliwa nyadhifa zake kimakosa hivyo uanachama wake unajadiliwa kwenye kamati kuu’.