
Mimi ni mzaliwa wa kijiji cha Hoyoyo Mkuranga kwa sasa hari yangu sio nzuri kutokana na Maradhi ya Macho nikimaanisha ni Kipofu tangu mwaka 2008,
lakini hapo kabla nilikuwa ni mzima na Matatizo yalinianza kutokana na matatizo na Mke wangu {Rukia Ally} na Mwanangu {Mwanaidi Said} mfanyakazi wa uwanja wa ndege FRAMINGO,Na maisha na familia yangu yalikuwa kama ifuatavyo.
Hapo yupo katika godolo lake analopumzikia wakati wa usiku
Nilioa mwaka 1977 na nikaishi na mke wangu Buguruni Malapa hadi mwaka 2004 na tukauza nyumba yetu ya Buguruni na nikampa mke wangu shilingi miilioni moja akanunue kiwanja Mbagala na akafanyikiwa kununua kiwanja cha shilingi laki sita fedha nyingine Yule mama alificha na hati za kiwanja pia kwa kushirikiana na kaka yake{SelemanAlly} na mwanangu. Sikujali hayo yote nikatoa fedha yangu na nikajenga nyumba katika kile kiwanja na tukaamia , ila Yule mama tena akaficha hati za nyumba .
Hivi ni vyombo anovyotumia mzee huyu
Kufika 12/11/2008 mke wangu aliondoka bila kuniaga na nguo aliamisha zote na nisijue zimeenda wapi? Ndipo anakuja mwanangu mkubwa na kuniuliza mama yupo wapi? nikamjibu sijui nae akasema kuwa leo anakuja mganga kuzindika nyumba , nikamuuliza mbona miye sina taarifa?Mida ya saa sita mchana mganga akaingia hadi ndani , nikaamua kuchukua uamuzi wa kwenda kumuchukua mjumbe na majirani wawili ambao wakaja na wakanisaidia kumfukuza mganga , alipoondoka mganga mke wangu na mwanangu wakaondoka pia kufika muda wa saa tatu usiku mke wangu alirudi na akaanza kudai taraka ndipo nikaamua kwenda kwa mjumbe na mjumbe alishauri tuongee na tuyamalize lakini mke wangu alikataa nikampa taraka japo kuwa macho yangu yalikuwa na maumivu makali sana na kuanzia siku hiyo sikuweza kuona tena hadi sasa naona giza nikimaanisha kipofu.
Tangu mwaka 2008 hakuweza kuona tena
Baada ya muda kupita yule mama alikuja na akanifukuza katika nyumba hiyo mpya niliyojenga Mbagala na nikaamua kupangisha chumba, nikajalibu kumtumia wajumbe wamwambie tuuze nyumba na tugawane fedha ila aliwatukana na kuwafukuza na akamua kunishitaki polisi ila polisi walitupilia mbali mashitaka yake walipo nisikiliza na wakanishauri nifungue kesi.
Hiyo ni net na godoro lakeHiyo ni hali halisi ya chumba chake