Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Twitter yapitisha utaratibu huu mpya kwa watumiaji wake.

$
0
0
newKasi ya matumizi ya mitandao ya kijamii imeendelea kukua kwa kasi kila siku na kupelekea kuongezeka kwa idadi kubwa ya watumiaji wa mitandao hiyo.
Mtandao wa Twitter umebadili sheria zake katika kuzuia watumiaji wake kuchapisha Picha na video chafu.
Sheria ya mtandao huu wa kijamii inasema ni ”Marufuku kuchapisha picha au video chafu zilizopigwa au kurekodiwa kisha kusambazwa bila ridhaa ya muhusika aliye kwenye video na picha hizo
Mwezi uliopita vitendo hivi vilitambulika kuwa makosa ya jinai nchini Uingereza na Wales.
Msemaji wa Kampuni ya Twitter amesema watumiaji watakaobainika kukiuka masharti mapya akaunti zao zitafungiwa.
Watumiaji wanaopeleka malalamishi Twitter kuhusu picha na Video zilizochapishwa watatakiwa kujitambulisha na kuithibitishia Kampuni kuwa hawakuwahi kutoa idhini ili kuchapisha picha au video mtandaoni na kuonekana hadharani.
Nchini Uingereza na Wales imeweka sheria ambayo mtuhumiwa atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka miwili gerezani.
Sheria hiyo inagusa picha zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii na Ujumbe mfupi huku majimbo kadhaa ya Marekani yameweka Sheria ya kupambana na vitendo hivi hasaCalifornia,Texas na Utah.

Chanzo:Millardayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles