Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Mwizi Apitiwa na Usingizi Nyumbani Kwa Mtu Alipoenda Kuiba!

Image may be NSFW.
Clik here to view.
Israeli Army Raids Gaza And Nablus
Jamaa mmoja amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuingia kwenye nyumba moja kwa lengo la kufanya uhalifu japo hakufanikiwa kukamilisha lengo lililomuingiza kwenye nyumba hiyo.
Matthew Waters alikutwa kwenye chumba cha spare akiwa amelala kwenye kitanda kilichopo kwenye chumba hicho huku pembeni yake kukiwa na kopo tupu la Ice Cream  ambayo inaonekana aliilamba kabla ya kupitiwa na usingizi.
Matthew aliamka kwa mshtuko baada ya mwenye nyumba hiyo Julie James aliporudi kutoka kazini na kufungua mlango wa chumba hicho ambacho ana kawaida kukikagua kila mara akirudi toka kazini.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Matthew Waters
Matthew Waters
Baada ya kushtuka, Matthew alikimbia lakini alikamatwa baada ya sura yake kuonekana kwenye camera za CCTV, Mahakama ilimkuta na hatia baada ya mpelelezi wa makosa ya jinai kugundua kuwa amekuwa akiishi kwa kuvamia nyumba za watu na kuhukumiwa kifungo cha miezi nane jela na kumlipa Julie paundi 100 (sawa na Tshs 270,000/-)

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles